Showing posts sorted by relevance for query dome budohi. Sort by date Show all posts
Showing posts sorted by relevance for query dome budohi. Sort by date Show all posts

Thursday, 26 December 2013



Katika kitabu changu ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1928) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism'' London 1998,  ambacho kilikuja kufasiriwa na kuitwa ''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes Historia iliyofichwa  Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza'' Nairobi 2002 nimeandika maneno hayo hapo chini kuhusu Dome Budohi:

''Familia yangu ilifahamiana na Dome Budohi, mmoja wa wanaharakati kutoka Kenya. Wakati ule wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika alikuwa akiishi Dar es Salaam. Budohi alikuwa mmoja wa wazalendo walioasisi TANU na kadi yake ya uanachama ni nambari sita aliyopewa Julai 1954. Mwaka 1955 alikamatwa na serikali ya kikoloni kwa tuhuma ya kuwa mmoja wa askari wa Mau Mau harakati za wazalendo takriban wengi wao wakulima wadogo waliokuwa wakipigana na ukoloni wa Waingereza nchini Kenya. Ninazo kumbukumbu nyingi za utoto nikimtembelea Budohi ndani ya selo yake Kituo Cha Kati cha Polisi. Hivi sasa jengo hilo ni Makao Makuu ya Shirika la Reli la Tanzania. Wakati huo mimi nilikuwa mtoto, si zaidi ya miaka minne hivi. Jambo la kwanza ninalokumbuka kuhusu Budohi ni kuwa kila mara tulipokwenda kumtembelea tulimkuta anasoma gazeti. Baadae Budohi alihamishiwa Kenya na aliwekwa kizuizini katika kisiwa cha Lamu. Alipofunguliwa toka kizuizini mwaka wa 1963 miezi michache kabla ya uhuru wa Kenya, Budohi alikwenda Uganda na akaajiriwa na gazeti la Uganda Argus. Hivi sasa ninaelewa kwa nini siku zile kila mara nilikuwa namkuta amezama ndani ya gazeti kila tulipokwenda kumtembelea pale rumande mjini Dar es Salaam. Niliweza kwa msaada wa rafiki yake Maxwell aliyelowea Tanganyika, kumpata Budohi mjini Nairobi mwaka 1972. Nilimtembelea mjini Nairobi wakati huo alikuwa akiishi Ruiru maili chache kutoka Nairobi mjini. Budohi alikuwa ametundika picha ya Nat King Cole sebuleni kwake. Mwaka 1974 nilimtembelea tena, safari hii katika nyumba yake ya Ngei Estate. Budohi alikuja kuwa mtu wa kwanza kabisa kunipa habari kuhusu historia ya harakati za Tanganyika dhidi ya ukoloni wa Waingereza. Hata hivyo wakati ule nilikuwa bado sijapata hamu wala kuwa na hamu ya kuandika kitabu kuhusu uhuru wa Tanganyika.

Kulikuwepo na wazalendo kutoka nchi jirani ya Kenya kama vile Dome Okochi Budohi na Patrick Aoko ambao walikuwa wanajua vyema siasa za walowezi za kupora ardhi za  wananchi. Kutoka kwa wazalendo kama hawa, Abdulwahid alipata usikivu wa mawazo yake ya kuigeuza TAA kuwa chama cha siasa chenye nguvu. Lakini mara tu baada ya kuundwa kwa TANU wazalendo hawa wa Kenya wakakamatwa na serikali. Kwa miezi sita walihojiwa na kuwekwa rumande Central Police Station huku wamefungwa minyororo. Budohi na Aoko walikuwa wakifuatwa na makachero (Special Branch) toka mwaka wa1952 baada ya hali ya hatari kutangazwa Kenya. Inasemekana Dome Budohi aliponzwa na barua iliyotoka Kenya ambayo ilikamatwa na makachero. Barua hii ilikuwa inamuhusisha Budohi na Mau Mau. Inasemekana Budohi alisalitiwa na Mkenya mwenzake aliyeitwa Martin[1]ambaye alikuwa pamoja naye katika Blackbirds. Martin alikuwa akipuliza tarumbeta.

Askari waliokuwa wakiwalinda kule rumande walitoa habari kwa TANU kuwa kulikuwa na mpango wa kuwapa sumu wafungwa wale, Budohi na mwenzake Aoko. Baadaye wafungwa hawa walihamishiwa Handeni ambako kulikuwa na kambi ya kuwafunga watuhumiwa wa Mau Mau. Kawawa alikuwa amehamishiwa hapo kutoka Dar es Salaam. Baadhi ya wafungwa walikuwa wananachama wa TAA na baada ya kuundwa TANU wakawa wanachama wa TANU. Kawawa alikuwa akifahamiana na wengi kati ya wafungwa wale. Budohi na Aoko waliwahi kuwa  viongozi wa TAA. Kawawa aliwaangalia wafungwa hawa kwa moyo wa huruma akijaribu kupunguza shida zao pale kambini kila alipopata mwanya wa kufanya hivyo. Budohi aliwahi kucheza senema ya Kiswahili na Kawawa iliyoitwa Mgeni Mwema iliyokuwa imetayarishwa na Community Development Department. Idara hii ilitengeneza filamu kadhaa ambazo Kawawa alicheza kama nyota wa mchezo. Katika senema zote alizocheza, iliyopata umaarufu na kupendwa zaidi ilikuwa Muhogo Mchungu ambalo ndiyo lilikuwa jina la Kawawa katika filamu hiyo.

Minongíono ilikuwa ikisikika kutoka kanda ya ziwa kuwa kiongozi wa wapiganaji wa Mau Mau, Dedan Kimathi alikuwa anaonekana mjini Mwanza. Wakati ule pale Mwanza kulikuwa na Wakikuyu wengi wakifanya biashara sokoni. Ilivumishwa kuwa Dedan Kimathi alikuwa akiwasiliana na Wakikuyu wenzake na wao walikuwa wakimkusanyia fremu za baiskeli za zamani ili zitumike kutengenezea magobole ili zitumiwe misituni dhidi ya majeshi ya Waingereza. [1]  Mapigano yalipoonza kati ya Mau Mau na Waingereza kulikuwa na Wakikuyu kama elfu kumi na sita wakiishi na kufanya kazi kaskazini ya Tanganyika. Kama tahadhari, Wakikuyu wachache walioonekana kuunga mkono Mau Mau, walikamatwa na kupelekwa Kenya ambako waliwekwa kizuizini katika kambi mbali mbali. Wakati Budohi na Wakenya wengine walipopita Korogwe wakati wakirudishwa Kenya kupitia Taveta, Ally Sykes, ambaye alikuwa amehamishiwa Korogwe, alikwenda hadi stesheni ya reli kuwaaga. Watuhumiwa hawa wa Mau Mau walikuwa wametiwa katika mabehewa ya kubebea ng'ombe huku wamefungwa minyororo. Dome Budohi na wazalendo wengine waliwekwa kizuizini kwa miaka saba.

Katika wale walioasisi TANU, ni wale tu aliokuwa makao makuu ya TAA ndiyo wanaoweza kueleza historia ya kweli ya  chama hiki. Hawa ni John Rupia, Dossa Aziz, Tewa Said Tewa, Julius Nyerere, Dome Budohi, Abdulwahid na Ally Sykes.

Miaka mingi baada ya kutoka kizuizini kisiwa cha Lamu, Budohi bado alikuwa ma mfundo na Martin na kila alipozungumza kuhusu yeye na mwandishi,alionyesha chuki ya kupindukia.

Wazalendo wa Kenya waliokuwa katika harakati nchini Tanganyika hawakuwa na uhusiano na TANU baada ya uhuru na wala chama hakikufanya juhudi kuwasiliana nao. Dome Budohi alijaribu mara nyingi kuomba kukutana na Nyerere alipozuru Nairobi lakini ilishindikana. Budohi hafahamu kama maafisa wa serikali ya Tanzania walimzuia wao tu au walifanya hivyo kwa amri ya Nyerere. Hadi anafariki Dome Budohi hakuwahi kuonana na Nyerere ambae wakati wa enzi za TAA na TANU walikuwa wakifahamiana vizuri.

Kadi nambari 1 ilitolewa na Ally Sykes kwa rais wa TANU, Julius Kambarage Nyerere na Ally aliweka sahihi yake kama afisa aliyeitoa. Ilipendekezwa kwamba kadi chache za mwanzo lazima zipigwe mnada na fedha zitakazokusanywa zitiwe  kwenye hazina ya chama. Abdulwahid, Ally, Dossa Aziz, Rupia na wengine walipanda dau kununua kadi hizo. Ally alimshinda kaka yake Abdulwahid kwa bei akapata kadi ya TANU nambari 2; Abdulwahid alipewa kadi nambari 3; Dossa Aziz kadi nambari 4; Phombeah kadi nambari 5; Dome Okochi, mmoja wa wale wazalendo kutoka Kenya katika TANU alipata kadi nambari 6 na Rupia kadi nambari 7. Bibi Titi kadi nambari 16; Iddi Tosiri kadi nambari 25.

Mwezi June 1953, makao makuu ya TAA yalitangaza kamati yake ya utendaji: J. K. Nyerere, Rais, Abdulwahid Sykes, Makamu wa Rais; J. P. Kasella Bantu, Katibu Mkuu; Alexander M. Tobias na Waziri Dossa Aziz, Katibu wa pamoja wa muhtasari; Wajumbe wa kamati: Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said Tewa, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo na Patrick Aoko.[1]Muundo wa uongozi katika TAA unaonyesha ule mshikamano wa Afrika ya Mashariki uliokuweko wakati wa harakati za uhuru. Wazalendo wa Kenya walichaguliwa kama viongozi wa TAA bega kwa bega na Watanganyika.'' 

Nimenyanyambua vipande hivyo kutoka sehemu tofauti ya kitabu changu ili kutoa picha na kujaza habari katika historia ya TANU na harakati za kudai uhuru. Mengi ya haya hayajulikani na wengi na hivyo kuathiri sana kufahamika na kuheshimu historia ya uhuru wa Tanganyika na mashujaa wake.

 

Wednesday, 14 February 2018

Dedan Kimathi
''Minong’ono ilikuwa ikisikika kutoka kanda ya ziwa kuwa kiongozi wa wapiganaji wa Mau Mau, Dedan Kimathi alikuwa anaonekana mjini Mwanza. Wakati ule pale Mwanza kulikuwa na Wakikuyu wengi wakifanya biashara sokoni. Ilivumishwa kuwa Dedan Kimathi alikuwa akiwasiliana na Wakikuyu wenzake na wao walikuwa wakimkusanyia fremu za baiskeli za zamani ili zitumike kutengenezea magobole ili zitumiwe misituni dhidi ya majeshi ya Waingereza. 

Mapigano yalipoonza kati ya Mau Mau na Waingereza kulikuwa na Wakikuyu kama elfu kumi na sita wakiishi na kufanya kazi kaskazini ya Tanganyika. Kama tahadhari, Wakikuyu wachache walioonekana kuunga mkono Mau Mau, walikamatwa na kupelekwa Kenya ambako waliwekwa kizuizini katika kambi mbali mbali. Wakati Budohi na Wakenya wengine walipopita Korogwe wakati wakirudishwa Kenya kupitia Taveta, Ally Sykes, ambaye alikuwa amehamishiwa Korogwe, alikwenda hadi stesheni ya reli kuwaaga. Watuhumiwa hawa wa Mau Mau walikuwa wametiwa katika mabehewa ya kubebea ng'ombe huku wamefungwa minyororo. Dome Budohi na wazalendo wengine waliwekwa kizuizini kwa miaka saba. 

Dome Okochi Budohi TANU kadi no. 6

Kulikuwepo na wazalendo kutoka nchi jirani ya Kenya kama vile Dome Okochi Budohi na Patrick Aoko ambao walikuwa wanajua vyema siasa za walowezi za kupora ardhi za  wananchi. Kutoka kwa wazalendo kama hawa, Abdulwahid alipata usikivu wa mawazo yake ya kuigeuza TAA kuwa chama cha siasa chenye nguvu. Lakini mara tu baada ya kuundwa kwa TANU wazalendo hawa wa Kenya wakakamatwa na serikali. Kwa miezi sita walihojiwa na kuwekwa rumande Central Police Station huku wamefungwa minyororo. Budohi na Aoko walikuwa wakifuatwa na makachero (Special Branch) toka mwaka wa 1952 baada ya hali ya hatari kutangazwa Kenya. Inasemekana Dome Budohi aliponzwa na barua iliyotoka Kenya ambayo ilikamatwa na makachero. Barua hii ilikuwa inamuhusisha Budohi na Mau Mau. Inasemekana Budohi alisalitiwa na Mkenya mwenzake aliyeitwa Martin ambaye alikuwa pamoja naye katika Blackbirds. Martin alikuwa akipuliza tarumbeta.

Askari waliokuwa wakiwalinda kule rumande walitoa habari kwa TANU kuwa kulikuwa na mpango wa kuwapa sumu wafungwa wale, Budohi na mwenzake Aoko. Baadaye wafungwa hawa walihamishiwa Handeni ambako kulikuwa na kambi ya kuwafunga watuhumiwa wa Mau Mau. Kawawa alikuwa amehamishiwa hapo kutoka Dar es Salaam. Baadhi ya wafungwa walikuwa wananachama wa TAA na baada ya kuundwa TANU wakawa wanachama wa TANU. Kawawa alikuwa akifahamiana na wengi kati ya wafungwa wale. Budohi na Aoko waliwahi kuwa  viongozi wa TAA. Kawawa aliwaangalia wafungwa hawa kwa moyo wa huruma akijaribu kupunguza shida zao pale kambini kila alipopata mwanya wa kufanya hivyo.''


***


''Mara tu baada ya kuundwa kwa chama cha TANU Wakenya walikamatwa na kurudishwa Kenya ambako waliwekwa kizuizini Manyani na katika kisiwa cha Lamu. Wazalendo wa Kenya waliokuwa katika harakati nchini Tanganyika hawakuwa na uhusiano na TANU baada ya uhuru na wala chama hakikufanya juhudi kuwasiliana nao. Dome Budohi alijaribu mara nyingi kuomba kukutana na Nyerere alipozuru Nairobi lakini ilishindikana. Budohi hafahamu kama maafisa wa serikali ya Tanzania walimzuia wao tu au walifanya hivyo kwa amri ya Nyerere. Hadi anafariki Dome Budohi hakuwahi kuonana na Nyerere ambae wakati wa enzi za TAA na TANU walikuwa wakifahamiana vizuri.''
(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes)


Thursday, 29 September 2016


Nyaraka kutoka  kwa  Kavazi la Mwalimu Nyerere ikionesha nyaraka kutoka jalada za Ally Sykes
Angalia uongozi wa TAA 1953 pamoja na Mwalimu Nyerere yuko Abdulwahid Sykes, Dome Budohi,
John Rupia, Dossa Aziz na Ally Sykes

Kushoto: Dossa Aziz, Julius Nyerere, Abdulwahid Sykes na Lawi Sijaona 
Arnautoglo Hall 1957

Kulia: Zuberi Mtemvu, Julius Nyerere na John Rupia
Waliosimama nyuma ni Bantu Group wa pili kulia waliosimama ni Ali Msham
picha hii ilipigwa nyumbani kwake Magoeni Mapipa ambako alifungua tawi TANU, 1955
...Ally Sykes alimniruhusu nisome majalada yake binafsi, barua zake, shajara na kumbukumbu nyinginezo za ukoo wa Sykes. Ally Sykes alinifahamisha kuwa kumbukumbu hizi zilikuwa ndani ya sefu ambayo haikupatwa kufunguliwa kwa zaidi ya miaka therathini. Nikiyapitia majalada yake nilishangazwa na utaratibu wa Ally Sykes wa kupanga kila kitu na kila kipande cha habari mahali pake hata kingekuwa kidogo namna gani wakati ule wa harakati. Ally Sykes ana barua ya mwaka 1954 iliyoandikwa kwa penseli toka kwa Zuberi Mtemvu kwenda kwake akimtaarifu juu ya mazungumzo aliyokuwanayo (Mtemvu) na Nyerere kuhusu yeye na TANU; stakabadhi ya hundi ya posta toka kwa Ally Sykes kwenda kwa Japhet Kirilo wakati wa Mgogoro wa Ardhi ya Wameru; nakala ya barua isiyokuwa na tarehe kutoka TAA kwenda kwa Malkia Elizabeth iliyotiwa saini na viongozi wote wa TAA: Rais Julius Nyerere, Makamu wa Rais Abdulwahid Sykes, Katibu Mkuu Dome Okochi, Naibu Katibu Dossa Aziz, Mweka Hazina John Rupia, Naibu Mweka Hazina Ally Sykes ikimpongeza Malkia kwa kutawazwa; barua ya mwaka 1952 toka kwa Rashid Mfaume Kawawa kutoka Bukoba kwenda kwa Ally Sykes ikimfahamisha juu ya hali ya siasa katika Kanda ya Ziwa; barua ya mwaka 1963 toka kwa Lady Judith Listowel, Kenneth Kaunda, Julius Nyerere, Kasela Bantu, Chifu Thomas Marealle ...orodha haina mwisho. ..


Kleist Sykes na wanae kulia pembeni yake ni Abbas, nyuma kulia ni Abdulwahid na Ally
Chief Thomas Marealle

Kulia: Abdulwahid Kleist Sykes na Ally Kleist Sykes
Burma Infantry Vita Kuu ya Pili
Baadaye nilipofnya utafiti kuhusu maisha ya baba yake, Kleist Sykes, nilikuja kufahamu kwamba tabia hii ilirithiwa kutoka kwa baba yake ambae alikuwa akiweka ndani ya jalada kila kipande cha karatasi kilichokuwa na habari iliyostahili kukumbukwa. Ni jambo la kuhuzunisha kwamba sikuweza kupewa shajara za Abdulwahid ambazo nilielezwa kwamba baadhi ziko katika hati-mkato na hadi leo hazijafasiriwa. Shajara hizi nimezioana kwa macho yangu lakini kwa kukosa idhini sikuweza kuzifungua na kuzisoma. Vilevile sikuweza kupata kumbukumbu halisi za Vita Kuu ya Kwanza zilizoandikwa na Kleist Sykes kwa mkono wake mwenyewe. Hapana shaka yoyote kwamba nyaraka hizi ni hazina zenye thamani isiyo na mfano wake. Ni matumaini yangu kwamba siku moja nchi yetu itakubali na kuthamini mchango wa Abdulwahid katika taifa la Tanzania na nyaraka hizi kama kielelezo cha harakati dhidi ya ukoloni, zitakubalika na zitawekwa chini ya hifadhi ya Nyaraka za Taifa kwa faida ya vizazi vijavyo.

Kasella Bantu

Dome Okochi Budohi
Kulia ni Dome Okochi Budohi na kushoto ni Mwandishi Ruiru,
Nairobi 1972
Familia yangu ilifahamiana na Dome Budohi, mmoja wa wanaharakati kutoka Kenya. Wakati ule wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika alikuwa akiishi Dar es Salaam. Budohi alikuwa mmoja wa wazalendo walioasisi TANU na kadi yake ya uanachama no. 6 aliyopewa Julai 1954. Mwaka 1955 alikamatwa na serikali ya kikoloni kwa tuhuma ya kuwa mmoja wa askari wa Mau Mau harakati za wazalendo takriban wengi wao wakulima wadogo waliokuwa wakipigana na ukoloni wa Waingereza nchini Kenya. Ninazo kumbukumbu nyingi za utoto nikimtembelea Budohi ndani ya selo yake Kituo Cha Kati cha Polisi. Hivi sasa jengo hilo ni Makao Makuu ya Shirika la Reli la Tanzania. 
Hili jengo mkonno wa kushoto ni Railway Station, jengo la mbele yake ndiyo
ilikuwa Central Police Station wakati wa ukoloni

Wakati huo mimi nilikuwa mtoto, si zaidi ya miaka minne hivi. Jambo la kwanza ninalokumbuka kuhusu Budohi ni kuwa kila mara tulipokwenda kumtembelea tulimkuta anasoma gazeti. Baadae Budohi alihamishiwa Kenya na aliwekwa kizuizini katika kisiwa cha Lamu. Alipofunguliwa toka kizuizini mwaka wa 1963 miezi michache kabla ya uhuru wa Kenya, Budohi alikwenda Uganda na akaajiriwa na gazeti la Uganda Argus. Hivi sasa ninaelewa kwa nini siku zile kila mara nilikuwa namkuta amezama ndani ya gazeti kila tulipokwenda kumtembelea pale rumande mjini Dar es Salaam. Niliweza kwa msaada wa rafiki yake Maxwell aliyelowea Tanganyika, kumpata Budohi mjini Nairobi mwaka 1972. Nilimtembelea mjini Nairobi wakati huo alikuwa akiishi Ruiru maili chache kutoka Nairobi mjini. Budohi alikuwa ametundika picha ya Nat King Cole sebuleni kwake. Mwaka 1974 nilimtembelea tena, safari hii katika nyumba yake ya Ngei Estate. Budohi alikuja kuwa mtu wa kwanza kabisa kunipa habari kuhusu historia ya harakati za Tanganyika dhidi ya ukoloni wa Waingereza. ...

(Kutoka Kitabu Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924 - 1968)...

Mwandishi na Mzee Maxwell 1997

Saturday, 1 March 2014








The Author With Poster of  The Book at Islamic Propagation Centre
International (IPCI) Durban, South Africa 2006

MUSLIM NATIONALISTS IN TANGANYIKA:
The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924–1968): The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika. By MOHAMED SAID. London: Minerva Press, 1998. Pp. 358. £11.99, paperback (ISBN 0-75410-223-8).
http://journals.cambridge.org/action...line&aid=72179


Msikilize Mwandishi: http://www.youtube.com/watch?v=k_1056Uk8Vo

Pieces from ''Acknowledgement''
The Sykes Letters

...this work would not have been possible if it were not for the moral and material assistance I received from Ally Sykes. Ally Sykes allowed me to interview him on many occasions in spite of his busy schedules managing his business from his city center office. He allowed me to consult his own private files, personal letters, diaries and other family records. These records were kept in a safe which I was informed remained untouched for over thirty years. Going through the files I was amazed by Ally Sykes’ obsession with record keeping. Every piece of paper with information was kept, however trifling it may have seemed during the struggle-a 1954 pencil note from Zuberi Mtemvu to Ally Sykes, informing him of a discussion he had with Nyerere about him and TANU; a 1953 money order receipt from Ally Sykes to Japhet Kirilo during the Meru Land Case; an undated copy of the letter from the TAA to Queen Elizabeth signed by the entire executive (the President, Julius Nyerere, Vice-President Abdulwahid Sykes, General Secretary Dome Okochi, Assistant Secretary Dossa Aziz, Treasurer John Rupia, Assistant Treasurer Ally Sykes) congratulating Her Majesty on her coronation; a 1952 letter from Rashid Mfaume Kawawa  from Bukoba to Ally Sykes informing him of the political situation in the Lake Region; a 1963 letter from Lady Judith Listowel; letters from Kenneth Kaunda, Julius Nyerere, Kasella Bantu, Thomas Marealle... the list is endless...

Dome Okochi Budohi

My family was acquainted with one Dome Budohi, a Kenyan nationalist who was in Dar es Salaam during the struggle. Budohi helped in the founding of TANU and his membership card was no.6 issued to him in July, 1954. He was arrested in 1955 by the colonial government on charges of being a member of Mau Mau, a peasant uprising in Kenya against the British. I have many recollections of visiting Budohi in his cell at the Central Police Station building which now houses the headquarters of the Tanzania Railway Corporation (TRC). 

For more information on Dome Budohi:
http://www.mohammedsaid.com/2013/12/walioacha-alama-katika-historia-ya-tanu.html

  1. MemberArrayYericko Nyerere's Avatar













    Join Date
    Jan 2014













    Posts
    83
    Rep Power
    1

    Kurejea kwa chama cha kidini cha AMNUT kwamlango wa nyuma wa ACT

    Mnamo mwaka 1958 kundi la waasi/wasaliti likiongozwa na Katibu mkuu wa TANU ndugu Mtemvu na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la TANU Shekhe Suleiman Bin Amir walifukuzwa baada tu ya uchaguzi wa chama hicho mjini Tabora ambapo wagombea wa nafasi ya rais wa chama alikuwepo Julius Nyerere na Abdul Skys, na mshindi alikuwa ni Julius Nyerere,

    Ikumbukwe uchaguzi huu ulikuwa ukiwakutanisha wagombea hao kwa mara ya pili kufuatia uchaguzi wa 1953 pale ukumbi wa Anatouglo Mnazimmoja chama kikiwa bado kinaitwa TAA.

    Naaam baada ya uchaguzi wa 1958, mitazamo ya kidini ilizidi kuchipuka hasa kwa kundi la waliofukuzwa kutaka chama kiwe na mlengo wa kidini,

    Walipofukuzwa walianzisha chama chao kiitwacho AMNUT, kikiendesha shughuli zake za kisiasa kwa mbeleko ya udini, lakini Watanganyika wote wa kipindi hicho walikikataa chama hicho na hivyo kikaishia mifukoni tu mwa akina Mtemvu, Shehe Amir na baadhi ya walioendelea kuwa ndani ya TANU.

    Sasa leo 2014, chama hicho kimeibu kwa jina la ACT, Njia za usakaji wafuasi zinalandana na AMNUT, Mitazamo na hulka za viongozi waanzishi wa chama hiki wanalandana kwa kila kitu na chama cha AMNUT,

    Juzi chama hicho kilifanya kazi ya uenezi mkoani mwanza na kigoma na watu wadini tofauti na mlengo wa AMNUT hawakuruhusiwa kujiunga hapohapo, waliambiwa kuna fomu maalumu kwaajili yao inayotakiwa kuiridhia kwa kiapo,

    Mimi kwakuangalia umoja na mashirikiano yetu, ninawaasa watanzania wawe waangalifu na chama hiki, na pia nimuase Msajili wa vyama vya siasa kutafakari upya kabla hajakipa usajili wa kudumu.

    Kwa wale ambao hamkuijua AMNUT, tembeleeni uzi huu hapa chini, tuliijadili kwa mapana yote,

    http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la...-zanzibar.html
    "Kuna watu wasipokuelewa maneno na matendo yako, mshukuru Jah, wewe bado unafikra chanya, wakianza kukuelewa jichunguze ni wapi umeanguka maana umeanza kuwaza kama wao"
    Quick reply to this messageReply   Reply With QuoteReply With Quote   Multi-Quote This Message      
  2. #26
    Senior MemberArray













    Join Date
    Feb 2014













    Posts
    124
    Rep Power
    1

    Re: Kurejea kwa chama cha kidini cha AMNUT kwamlango wa nyuma wa ACT

    Quote Originally Posted by PM2013 View Post
    Samahani Mkuu. lkn naona Yericko anamwaga data na anajibu hoja zako kwa nakshi kabisa
    PM2013,
    Labda nikuulize ''data'' iweje ili iwe ''data?''
    Edit / DeleteEdit Post   Quick reply to this messageReply   Reply With QuoteReply With Quote   Multi-Quote This Message    
  3. #27
    PM2013 is offline
    MemberArray













    Join Date
    Dec 2013













    Posts
    69
    Rep Power
    1

    Re: Kurejea kwa chama cha kidini cha AMNUT kwamlango wa nyuma wa ACT

    swali kwa mohamed Said.
    Upi ulikuwa mchango wa bibi Titi katika kupigania uhuru? na nini kilichomsibu hadi kukwaruzana na mwalimu?
    Quote Originally Posted by PM2013 View Post
    Shukran kwa kutueleimisha wanajamvi wengi. kwani baadhi yetu tulikuwa hatuijui historia hii


    - - - Updated - - -

    Shukran kwa kutueleimisha wanajamvi wengi. kwani baadhi yetu tulikuwa hatuijui historia hii
    Quick reply to this messageReply   Reply With QuoteReply With Quote   Multi-Quote This Message      
  4. #28
    Junior MemberArray













    Join Date
    Feb 2014













    Posts
    5
    Rep Power
    0

    Re: Kurejea kwa chama cha kidini cha AMNUT kwamlango wa nyuma wa ACT

    Quote Originally Posted by Mohamed Said View Post
    Wanaukumbi,
    Kuna makosa mengi.

    Kwanza
    Dk. Kyaruzi hakuwa daktari wa kwanza Tanganyika.

    Daktari wa kwanza alikuwa Joseph Mutahangarwa na hili nimelieleza katika
    kitabu cha Abdu Sykes, ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes...''

    Na hili nilielezwa na Dossa Aziz.

    Pili Dk. Kyaruzi hakuhamishiwa Kahama bali Kingolwira kisha Nzega na
    sababu za uhamisho huu nimezieleza katika kitabu cha Abdu Sykes.

    Tatu Nyerere hakumshinda Abdu kwa kishindo.
    Nyerere alimshinda Abdu kwa kura chache.

    Ushahidi wa uchaguzi huu uko katika kitabu cha Lady Judith Listowel,
    The Making of Tanganyika Chato and Windus, 1965.

    Nne Nyerere hakupelekwa UNO 1955 na Wakatoliki.

    Kisa cha safari ya Nyerere ni maarufu na nimeileza safari ile kwa kirefu
    katika kitabu cha Abdu Sykes.

    Mkutano wa Tabora wa 1958 hapakuwa na uchaguzi wa Abdu Sykes na Nyerere na
    mwaka huo aliyefukuzwa TANU ni Sheikh Suleiman ''Makarios'' Takadiri peke
    yake wengine walijitoa wenyewe kama Hamisi Hunde, Ramadhani Mashado Plantan,
    Abdulwahid Abdulkarim, Abdallah Mohamed na wengine.

    Katika TANU hapakuwa na Shehe Selemani Amiri.

    Kulikuwa na Mufti Sheikh Hassan bin Amir na huyu ndie ilikuwa nguzo ya Nyerere
    na TANU yenyewe.

    Kisa Cha Sheikh Hassan bin Amir na Nyerere nimekieleza kwa kirefu sana
    katika kitabu cha Abdu Sykes.

    Haya mimi nayajua kwa undani kwani wengi katika hao ni wazee wangu na
    nikiwajua katika udogo na tukakutana mie nikiwa na fahamu zangu.

    Naamini nimeweka yote sawasawa.

    Atakae kusoma zaidi kuhusu historia hizi na aingie katika website yangu:

    www.mohammedsaid.com.
    Maalim Mohamed Said nakupa hongera sana kwa hakika simulizi zako za kweli za historia ya nchi yetu zimewakimbiza wateteo historia uwongo. Yuko wapi sasa mzee Yusuph Halimoja aliyekuwa mstari wa mbele kujibu kila post na chapisho ulilokuwa ukiandika, sasa hivi yuko kimya, Maprofesa wengi wamejaribu kupima kina cha maji yako kwa majina bandia na wamegundua kuwa kina chako ni kirefu na chenye maji yaendayo kasi kiasi kwamba kuogelea wameshindwa.

    Sasa amebaki Yericko mwanapropaganda wa chadema.Sisi vijana tunakufuatilia kwa ukaribu sana kwa ajili kujifunza na kustafidi na elimu maridhawa uitoayo kupitia chapisho zako pamoja na post mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii.Tuko pamoja toka mwanzo tumejifunza mengi Kutoka kwako.Mwenyezi mungu akuzidishie kwa kutoa elimu kwa mamilioni ya watanzania na ulimwengu kwa ujumla.

    Sasa tunataka tukuingize bungeni Maalimu wetu ukawape darasa kidogo, maana toka alipotoka Kighoma Malima na Kitwana Kondo waislam wamekuwa kama wamekosa msemaji huko. Naamini siku ukiingia huko kwajinsi unavyotoa fact kila utakapoongea itabidi wakate umeme nchi nzima ili fact isisambae nchi nzima.