Kisa cha Aliyekuwa Polisi Sajenti Rashid Zahaki na
Mauaji ya Mwembechai Ijumaa 13 Februari 1998
Mauaji ya Mwembechai Ijumaa 13 Februari 1998
![]() |
| Rashid Zahaki Baada ya Kufukuzwa Jeshi la Polisi
Tunatengeneza habari za Rashid Zahaki...
Kisa chake ni cha kusikitisha...
Fatilia ukurusa huu.
Sikupata kabla kumjua Rashid
Zahaki hadi aliponipigia simu nikiwa Tanga na hapo ndipo tulipofahamiana. Kwa
ufupi aliniambia kuwa ana habari muhimu kuhusu kuuliwa kwa Waislam Mwembecha
ambazo angependa kunifahamisha. Tukapanga miadi kuwa nikija Dar es Salaam
nitampigia simu tuonane na anipe hicho kisa. Mauaji ya Mwembechai yalikuwa
mashuhuri na ni moja katika matokea ya kusikitisha na kuhuzinisha katika
historia ya Waislam wa Tanzania. Hakika nilimkaribisha Rashid Zahaki nyumbani
kwangu na akanielza mkasa mzima wa nini kilikuwa kimepangwa hadi yakatokea
mauaji yale.
![]() Wakati ule yeye Rashid Zahaki alikuwa katika Jeshi la Polisi. Kanda ile niliyorekodi nilimpa Dk. Hamza Mustafa Njozi na yeye kufuatia umuhimu wa taarifa ile alitumia mazungumzo yangu kwenye moja ya kitabu chake,''Muslims and the State in Tanzania.'' Kabla ya kukutana na mimi kwa muda mrefu alipita katika vyombo vya habari tofauti akijaribu kuwaeleza ukweli wa kile kilichotokea Mwembechai na kusababisha mauaji lakini hakuna hata mhariri mmoja aliyekuwa tayari kumsikiliza na kuchapa taarifa yake. Kipindi kile alinieleza Zahaki kuwa kilikuwa kipindi kigumu sana katika maisha yake licha ya kuwa hana tena njia ya kuendesha maisha yake bali aliona kwa dhahiri yake nguvu ya Mfumokristo katika Tanzania. Ndipo hapo baadhi ya watu wakamuelekeza kukutana na mimi labda ningeweza kusikiliza kisa chake na kukiweka bayana kwa Waislam kukifahamu. Wakati namsikiliza Rashid Zahaki ilinijia picha katika kitabu cha Muhammad Ali ''The Greatest My Own Story,'' ambacho kuna sura inayoeleza kuwa siku moja katika miaka ya 1970 baada ya Ali kushinda kesi ya kufungiwa kupigana, muda mchache kabla hajapanda ulingoni aliletwa kijana wa Kinegro ambae Klu Klux Klan walikuwa wamemhasi, yaani wamemkata sehemu zake za siri na kuzinyofoa kabisa kwa chuki ya rangi. Yule kijana kwa muda mrefu alikuwa anatafuta nafasi ili amuone Ali na kumwelezea kisa chake akiamini Ali alikuwa na uwezo na ujasiri wa kueleza dunia mkasa wake. Zahaki tukiwa nyumbani kwangu sauti iliyokuwa ikinijia ilikuwa ya kinasa sauti changu kikizunguka na sauti ya upole ya Zahaki akieleza chuki iliyokubuhu katika jeshi la polisi dhidi ya Waislam. Hii ilikuwa zaidi ya miaka 10 iliyopita. Muongo mmoja. Hali ikoje hivi sasa? Nilimfananisha Zahaki na yule kijana wa Kinegro aliyefika mbele ya Ali kumueleza dhulma aliyofanyiwa na Wazungu wabaguzi wa rangi. Fuatilia ukurusa huu kwa habari zaidi...In Sha Allah utamsoma Zahaki kwa maneno yake mwenyewe anaeleza aliyoyaona katika jeshi la polisi... Nakutaka radhi kwa usumbufu huu:
Ndugu yangu msomaji tafadhali
ruka haya mabandiko hapo chini na nenda mbele zaidi utakuta kurasa kama hizi
ambazo zimepangika sawasawa.
.
l HAMZA MUSTAFA NJOZI
Soma Hii hapa Chini: ********************************************************************************
Anza kusoma hapa habari za Rashid Zahaki
|


No comments:
Post a Comment