Monday, 17 February 2014

Serikali Mbili Zilizoboreshwa ni Jitihada ya Kutoharisha Najis

CCM inatapatapa.
Imekuja na jambo jipya la ajabu na kustaabisha.

Kwa Waislam haitakuwa tabu kuelewa kwa kuwa usafi wa mwili na nguo
ndiyo msingi wa swala.

Bila nguo na mwili kuwa tohara huwezi kusimama mbele ya Allah kumuabudu.
Lazima uwe tohara mavazi na mwili wako.

Nguo ikipata najis lazima itoharishwe ili ifae kuvaliwa na mja kuweza kuswali.

Nini najis?

Kwa mfamo wa haraka, ''mkojo'' ni najis na nguo ya mja ikiingia mkojo ni lazima
itoharishwe.

Kinachotoharishwa hapa ni ile nguo na hutoharishwa kwa maji safi.

Leo serikali mbili zilishanajisika miaka mingi na imekuwa sababu ya malalamiko 
mengi sana kutoka kwa Wazanzibari.

Tume ya Katiba ya Jaji Warioba ishasema wananchi wengi wanataka serikali 
tatu.

CCM leo imekuja na fikra ya ''Serikali Mbili Zilizoboreshwa.''
Huku ni kutaka kuitoharisha najis.

Ukweli ni kuwa najis haiwezi kutoharishwa.
Najis ni hiyo serikali mbili wanayoililia CCM.

Ni sawasawa na mkojo ambao wao wanataka kuotoharisha badala ya kutoharisha 
nguo.

No comments: