Utangulizi

Katika mambo yaliyosaidia sana kuiweka vyema historia ya Zanzibar ni vitabu vilivyoandikwa na Wazanzibari wenyewe ambao walipigania uhuru wa Zanzibar. Historia iliyokuwa ikipewa nafasi ni historia ya mapinduzi peke yake ilhali Wazanzibari walipigania uhuru wao kutoka kwa Muingereza wakaupata na baada ya hapo kiasi cha mwezi mmoja tu yakatokea mapinduzi yaliyosababisha umwagaji mkubwa wa damu na madhila mengi. Baada ya Ali Muhsin Barwani kuandika kumbukumbu zake: ''Conflicts and Harmony in Zanzibar,'' ambayo kwa hakika ni historia ya kudai uhuru wa Zanzibar na historia ya vyama vilivyopigania uhuru wa Zanzibar - Zanzibar Nationalist Party (ZNP) au Hizbu, Afro Shirazi Party (ASP) ya Abeid Aman Karume na Zanzibar and Pemba Peoples Party (ZPPP) ya Mohamed Shamte picha mpya ikajitokeza. Lakini ilikuwa kalamu ya Aman Thani katika kitabu chake: ''Ukweli ni Huu,'' ndiyo iliyokuja na historia ya kutisha. Haya hivyo kitabu cha Dr. Harith Ghassany: ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,'' utafiti huu ulishinda tafiti zote za kigeni na ndicho kilichokuja kuweka historia ya Zanzibar katika mawanda ya dunia. Yale yaliyokuwa yamefichwa sasa yakawa yapo uwanjani peupe yanasomwa, na wengi wa wasomaji hao ni vijana waliozaliwa baada ya mapinduzi. Matokeo ya mwamko huu mpya ndiyo haya tunayoshuhudia hivi sasa. Bahati mbaya badala ya kusikitishwa na yaliyotokea na kujaribu kuleta umoja pamezuka watu wanakejeli waliouawa kwa dulma katika mapinduzi yale. Waliouawa wameacha watoto na wajukuu wapo kwa sasa, wamesimama kupinga kila aliyekuwa anaonyesha kufurahishwa na historia ile iliyowapotezea wapendwa wao.
Mpenzi msomaji soma hapo chini kwa taarifa zaidi:
Mohamed SaidVerified User ✅
Pasco,
Ni tabu kukuelewesha chochote katika historia ya Zanzibar.
Mohamed SaidVerified User ✅
Simplemind,
Makomredi hawakuwa katika mpango wa mapinduzi.
Makomredi waliingia mtaani siku ya pili ya mapinduzi
kuweka mambo sawa baada ya kudhnihiri kuwa yapo
mauaji mengi yaliyokuwa yaakifanywa na Okello na
Wamakonde kutoka Kipumbwi.
Mkuu
Mohamed Said
, ni kweli ni ngumu sana kunilisha urongo, kama shuhuda wa Mapinduzi yale Matukufu amesema jambo hili lilikuwa hivi, nitamuamini, na kamwe sitauamini urongo wa simulizi za Kipumbwi!.
Pasco
Pasco. Simulizi za kipumbwi unasema za urongo je simulizi za mzee aman thani na ali barawani nk nazo ni za urongo.?
Samahani kwa kumjibia mzee muhamed naishia hapo mzee muhamed endelea tafadhal..
Mohamed SaidVerified User ✅
Pasco,
Kipumbwi ilikuwapo kambi ya mamluki wa Kimakonde na Victor Mkello
kathibitisha hilo.
Lakini kama hili linakutisha sana kiasi unataka kuwa bora lisingekuwapo
mimi naelewa.
simplemindJF-Expert Member
Hili limenitazi kweli confirmed Mzanzibari hasahau asili.
Mohamed SaidVerified User ✅
Sahimtz,
Umefanya sawa kaka yangu.
Kitu ninachokiona kwa Pasco ni kutokujua ukweli wa mauaji
ya dhulma waliofanyiwa watu Zanzibar katika na baada ya
mapinduzi.
Ana
Yeye hajui anapotumia maneno ''mapinduzi matakatifu,'' nk. nk.
kuna watoto wa waliouliwa na wajukuu zao wanasoma maneno
haya na maini yanawakata.
Hajui Pasco nini kuuliwa kwa mtoto wa miaka saba nane bila
sababu ndani ya msikiti.
Hajui Pasco nini kuuliwa kwa mama au baba au rafiki nk.
Walikuwa wakiwa jela baadhi ya wafungwa kutoka Zanzibar
walikuwa wakihitimisha walikuwa wakiwaombe Mungu hata wale
waliofanya ubaya ule.
Inaweza isimshangaze Pasco kama nikimweleza kuwa Sheikh Ali
Muhsin Barwani na wenzake ambao walifungwa Bara kwa miaka
10 walikuwa wakihitimisha wanalitaja jina la Hanga walipojua kuwa
kauawa na wakimuombea maghufira kwa Allah.
Namweleza Pasco mara kadhaa kuwa asome kwanza kabla ya kuja
barazani kujadili.
Namaliza kwa kumueleza Pasco kitu kimoja.
Mauaji yalipokuwa yanakithiri mama yake Adam Mwakanjuki alitoka
mtaani kwake akapiga kelele na kusema, ''Jamani hebu acheni kuua
watu hawa Hizbu kwetu walikuwa kama watani wetu haya ya kuua
ya nini?''
Anaependa kujua zaidi katika historia ya mapinduzi aingie hapa:
Tujikumbushe: Sheikh ali muhsin barwani mmoja wa wapigania uhuru wa zanzibar
Anaweza kusoma pia kitabu cha Ali Muhsin Barwani: ''Conflicts and Harmony in Zanzibar,''
kinapatikana Ibn Hazm Media Centre Bookshop Msikiti wa Manyema na Msikiti wa Mtoro.
Pia kitabu kinapatikana Tanzania Publishing House, Samora Avenue.
Mkuu
sahimtz
, mimi ni mwafunzi wa somo la fasihi, ambapo kuna fasihi simulizi na fasihi andishi!, tunapokuja kwenye authenticity, kitu ambacho ni authentic ni kile mtu unachokisikia kwa masikio yako kutoka kwenye source, "from the horses mouth". Ile fasihi andishi ambayo inaandikwa kutoka fasihi simulizi, mara nyingi sio authentic, na inawezekana kabisa msimulizi akasema kitu hiki, lakini mwandishi akapotosha kwa makusudi ili kutimiza malengo yake, kama mwandishi mmoja alivyowahi kuandika kuwa asili ya Waarabu ni Bara la Afrika ndipo wakaenda Arabuni!.
Bandiko hili ni masimulizi ya fasihi simulizi niliyo isikia kwa masikio yangu mwenyewe!. Aliyeandika simulizi za Kipumbwi ni fashi andishi aliyosimuliwa kisha akaandika!, bahati nzuri mimi sikuwahi kuisikia hiyo simulizi ya Kipumbwi kutoka wengi wa waandishi wa historia ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar!.
Sasa kinapoibuka kitu kipya ambao huko nyuma hakikusemwa, tuna haki ya kukita ni urongo, vinginevyo tuthibitishiwe kwa fasihi simulizi kutoka kwa "horses mouth" sio watu mhadithiane, kisha mje mtuandikie kile mlichohadithiwa!.
Pasco
Mkuu Maalim Mohamed Said hii mada ya ni mada ya fasihi simulizi kwa niliyoyasikia mimi kwa masikio yangu ndipo nikaiweka kwenye fasihi andishi!. Sasa hiyo story ya Victor Mkello alipothibitisha hilo, alirekodiwa wapi sound track nasi tumsikilize tuamini!, haya ya mtu kuhadithia watu kisha hao waliohadithiwa ndipo waje watuandikie wanavyotaka wao, ndiko huku wengine wenu tunapogoma kulishwa urongo!.
Pasco
Pasco..mm nipo na ww nadhani ww unataka kujua kama mm ninavyo takakujua nisilolijua.
kibumpwini unaita ya urongo mm nimekuuliza simulizi za mzee Aman Thani na Ali Barwani nk nazo nizaurongo?
Huja yangu hapa sio kumtafuta mshindi hoja yangu ni kuelimika na kueleweshana.
Mkuu Maalim Mohamed Said, kwanza pole kwa kukumbuka machungu ya yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964!. Aliyeyaita Mapinduzi yale Matukufu sio, wanayaita hao wenyewe waliofanya mapinduzi hayo tena kuna kibwagizo kule cha "Mapinduzi Daima!".
Wakati waliopindua waliyaita Mapinduzi Matukufu, waliopinduliwa wanayaita Mauaji ya Halaiki ya 1964!, wakati wengine wakishangilia na kuita huo ni ukombozi, wengine wanagumia kwa machungu ya mapinduzi yale na umwagaji damu mkubwa kivile kwa vijisiwa vidogo kama vile!, hizi kauli ni parallel lines and will never meet!, ili kuzikutanisha hizi kambi mbili, nilisisitiza lazima kufanyike tume ya peace and reconciliation, kupooza machungu, kwanza muambiane, kisha mjutie, msameheane ndipo msonge mbele!.
Wakati wa uchaguzi sio mara moja wala mbili nimewauliza humu, jee mnajua kuwa siku zote ni "ni kweli 'fulani' ndio huwa anashinda uchaguzi lakini hatangazwi?!", nikasema bila Wanzanzibari kujiuliza sababu za kwa kwanini mshindi huwa hatangazwi, then kama sababu hizo bado zipo, kipi kitakachomfanya akishinda safari hii atangazwe?!. Hakuja aliyejishughulisha kujua sababu!.
Sababu ni kivuli cha Mapinduzi!, kuna watu hata ukiwaona tuu kwa macho makavu, wanaonekana with "fire on their eyes" na chuki, maumivu, na hasira kubwa ndani ya mioyo yao, kisi cha kuwepo possibility ya visasi!, sasa mtu kama huyu nani atampa nchi?!.
Huku kunihadithia nani na nani walikufa na waliuawawa na nani, sio tuu tumeishahadithiwa sana, bali hata kuonyeshwa video za kupikwa za mapinduzi hayo!, na bado tunayaita ni Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ndivyo wanavyoyaita wenye mapinduzi yao!.
Poleni kwa machungu ya maumivu ya mapinduzi yale!.
Pasco
Mohamed SaidVerified User ✅
Pasco,
Unanitaabisha sana kwa kuwa ili kukujibu ukaridhika inabidi
niseme maneno ambayo huenda watu wakachukulia kuwa ni
ya dharau.
Pasco huna elimu ya kutosha katika mambo haya ndiyo maana
unataka usikilizishwe mahojiano ya Victor Mkello.
Hebu kwa kuanzia mjue Victor Mkello kwanza nini mchango wake
katika kupambana na wakoloni.
Ukimjua hayo mengine hayatakuwa shida kwako.
Dr. Harith Ghassany si msomi wa kupapasia.
Kasoma American University Cairo, University of Michigan na kumalizia
Harvard.
Katika utafiti wa kitabu kapitia maktaba zote kubwa katika African History
Marekani na kwenyewe Uingereza.
Kasoma vingi katika maktaba hizo.
Hapa nyumbani kazungumza na wengi wengine walikuwa watumishi wa
Special Branch ya wakoloni.
Mimi alinichukua kama Mtafiti Msaidizi.
Siku ya kwanza tulipokutana na Victor Mkello baada ya mazungumzo
alinambia, ''Victor Mkello ni kama Waingereza walivyomsema alivyo katika
taarifa zao za kijasusi.''
Pasco badala ya kusoma historia ya Zanzibar na kuielewa unataka usikilizishwe
''audio'' ya Victor Mkello.
Pasco bado hujafikia makamo ya kujadili mambo haya.
Mohamed SaidVerified User ✅
Pasco,
Kuna mtu baada ya kuona kibri chako katika hii post yako yako kwa
uchungu anasema huyu ni mtu wa kuapizwa.
Ana maana na wewe auliwe katika wako ujue uchungu wa mwana
kuuliwa kwa mapanga na risasi.
Nimemtuliza.
Nimemwambia haifai.
Huyu ni mtu asiyejua kitu na tumchukulie hivyo.
Nimemwambia kuwa nimekuasa uache kejeli lakini umerudia maneno
yale yale kwa kibri kile kile.
Nimemweleza hafai kuapizwa ila kuombewa dua.
Kanitajia baba yake alivyouliwa kisha akaja mtu akaipiga teke maiti
ya baba yake yeye akiona.
Alikuwa na umri wa miaka mitano.
Pasco hili si jambo la ushabiki na kujiona wewe hodari wa lugha kwa
kuandika, ''mapinduzi matakatifu,'' na mengine.
Utukufu ni wa Allah pekee.
Umezungumza kuhusu mapinduzi daima.
Ikiwa ni hivyo iweje sasa Wazanzibari wanaiangusha CCM mfululizo kila
uchaguzi?
Mkuu Maalim , kama tumefika huku, nashauri sasa tuendelee na kosoma nyuzi nyingine, ila hili la Mapinduzi Matukufu sio langu, tangu nimeanza kuyasikia, nimeyasikia yakiitwa hivi, na hizi ni baadhi ya nyuzi za wana JF waliyoyaita ni Mapinduzi Matukufu!, namna pekee ya kuuondoa utukufu wa Mapinduzi yale Matukufu, ni kuwasisitiza hao hao waliyoyaita Mapinduzi Matukufu kuacha kuyaita hivyo, na kibwagizo cha "Mapinduzi Daima" kifutwe!. CUF wamekaa ndani ya SUK kwa miaka 5, sikumbuki kama walifanya lolote kupinga jina hili la Mapinduzi Matukufu na "Mapinduzi Daima", hivyo hili la mtu kutaka kujiapiza kwa ajili yangu, itakuwa ni kunionea bure!, asante kuniombea waninusuru sasa tuendelee na mada nyingine!. Kwa kuanzia neno Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar limeandikwa katika nyuzi 1,540 humu ndani ya jf, hivyo nakuomba sasa tuachane na uzi huu, tembelea hizi nyuzi utoe hii elimu kuwa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar hayana utukufu wowote bali yalikuwa ni mauaji ya halaiki!.
Karibu
Pasco
Ni kwanini Mapinduzi ya Zanzibar wanayaita mapinduzi Matukufu
Mapinduzi Daima ndicho kinachoenziwa Zanzibar
Mapinduzi Yanayoitwa "Matukufu" ya Zanzibar yalivyotokea ...
Ukweli wa historia ya mapinduzi ya Zanzibar
Dkt. Shein azindua Sherehe za Mapinduzi kwa Usafi wa Mazingira ..
AZAM TV: MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUTOKA KUMBUKUMBU ZILIZO
CCM yasikitishwa, yaomba radhi kwa Bango lenye ujumbe wa Uchochezi.
Mapinduzi ya Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers
Picha: Katika kilele cha mapinduzi uwanja wa amani mjini Zanzibar .
Jina Chama cha Mapinduzi (CCM) limetokana na nini/wapi ..
Tamko la UVCCM Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers
Dk Salmin: Msikubali Mapinduzi kufutwa Zanzibar |
Tutakukumbuka hayati mzee Karume | JamiiForums | The Home of Great
Nini maana ya 'Kidumu Chama cha Mapinduzi' na 'Mapinduzi daima ..
Unaijua historia ya ASP na rangi ya sura yake?
JK: Mapinduzi Z'bar yamefungua fursa ya elimu kwa Wazanzibari ..
Kujiamini,kuchanganyikiwa halafu Hofu kuu!!!Ndoo la mapinduzi ..
Yaliyojificha kwenye muungano wetu
Kesho, Jumatatu ni siku ya mapumziko Tanzania Bara na Zanzibar .
UVCCM Zanzibar: Abeid Karume afukuzwe CCM
Mapinduzi ya Zanzibar: Ukweli ni Upi?
Nyerere, Okello, Jumbe, Shivj na Kifo cha Karume: Nani alimuua .
Waarabu wabaya sana, CUF na Wazenji wanataka kurudisha waarabu ..
Ahmed Rashad Ali Bingwa wa Propaganda za Ukombozi wa Afrika ...
Vijana elfu tano waendelea na matembezi kuenzi miaka 51 ya
Zanzibar Haijawahi Kutawaliwa Baada ya Mapinduzi Matukufu ya 1964
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi! |
Amiri Jeshi mkuu, iambie CCM isiilazimishe CUF ifuate njia ya ASP
Vyombo vya Habari Tanzania acheni Woga, Andikeni CCM Zanzibar .
Balozi Seif Ali Idi: Sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar ...
Makamu wa Kwanza wa Rais azua balaa CCM |
The Zanzibar political paradox: Mapinduzi sasa yamekosa mashiko .
Kuanguka haraka kwa CCM na Hatari inayolikumba Taifa hivi sasa ...
Vituko vya Watanganyika dhidi ya Zanzibar
Live channel ten .Balozi Karume ndani ya je tutafika ..
Siku ya Karume..
Sultan Qaboos karibu Tanzania |
picha nyingi maneno machache
Mchague Maalim Seif sharif Hamad atupeleke Umoja wa Mataifa ...
Haya ndio Mapinduzi ya Zanzibar, yamerikodiwa live na waitaliano ..
Mohamed SaidVerified User ✅
Pasco,
Ikiwa mtu anatukana na wewe ukalirudia tusi lile na wewe umetukana.
Hicho ndicho ulichokuwa ukikifanya wewe tena kwa jeuri, kebehi na kibri.
Nimefurahi kuwa umeelewa uzito wa jambo hili.
Pasco,
Sina tatizo na murua wako unaweza kufanya unachopenda.
Ninachofanya mimi ni kukufahamisha ubaya wa hulka yako.
Wako kama wewe wanaokataa kuwepo kwa Auschwitz na
Dachau.
Katika mapinduzi ''matukufu,'' watoto walibakwa pamoja
na mama zao chumba kimoja wakitazamana na katika hao
mabinti walikuwapo ambao walitolewa bikra wazazi wao
wakiona.
Huenda labda waliokuwa na afueni ya unyama ule ni wale
baada ya haya yote waliuliwa.
Ndipo aliposema uapizwe ili na wewe Allah akuonjeshe ladha
ya wako kufanyiwa waliofanyiwa wapendwa wao.
- Ndugu msomaji,
- Mjadala unaendelea hapa chini:
- http://www.jamiiforums.com/threads/mapinduzi-matukufu-ya-zanzibar-kumbe-waarabu-hawakufukuzwa-walikimbia-wenyewe-mzee-sukari.582421/page-15#post-16205941
No comments:
Post a Comment