
| Picha ya Bismini |
| Bi. Maunda Plantan mjukuu wa Affande Plantan akimsomesha Mwandishi historia ya wazee wake katika Tanganyika. Bi. Maunda alikuwa mwalimu na mtangazaji wa kwanza wa kike Tanganyika Radio Dar es Salaam ilipoanzishwa nwaka wa 1952 |
Macos,
Ahsante
sana kwa kunitaja katika hii mada ya Picha ya Bismini na kuniomba nichangie.
Wakati wa Vita ya Pili ya Dunia (1914 - 1918) Tanganyika ilikuwa chini ya utawala wa Wajerumani. Sanamu hii ya Bismini ni kwa ajili ya kuwakumbuka askari waliopigana upande wa Muingereza dhidi ya Mjerumani.
Wakati wa Vita ya Pili ya Dunia (1914 - 1918) Tanganyika ilikuwa chini ya utawala wa Wajerumani. Sanamu hii ya Bismini ni kwa ajili ya kuwakumbuka askari waliopigana upande wa Muingereza dhidi ya Mjerumani.
Hii ni
kumbukumbu ya babu zetu askari na wapagazi Waafrika ndani ya jeshi la Muingereza. Kama ulivyosema ni kuwa awali ilikuwapo picha
ya Herman Von Wissman. Huyu Wissman ndiye
aliyeongoza vita dhidi ya wananchi wa Tanganyika kwa kuleta askari mamluki Wanubi kutoka
Sudan na Wazulu kutoka Mozambique.
Katika
hawa Wanubi maarufu katika askari hawa katika mji wa Dar es Salaam ni Mzee Hamisi baba yake Ibrahim Hamisi mmoja wa waasisi wa African Association pale ilipoanzishwa
mwaka wa 1929. Mtoto wa Ibrahim Hamisi, Abdallah
Ibrahim ni mmoja
wa watu niliozungumza nao katika kujifunza historia ya mji wa Dar es Salaam.
Askari wengine
walitoka Congo na mmoja wapo ni babu yangu mkuu Samitungo Mwekapopo aliyekuwa katika
Boma la Wajerumani Shirati, Musoma. Katika Wazulu walioingia Tanganyika pamoja na Wissman ambao taarifa
zao ziliweza kuhifadhiwa ni Sykes Mbuwane baba yake Kleist Sykes, baba yao Abduwahid, Ally na Abbas Sykes.
Hawa
askari wote mamluki walikuwa katika kikosi kilichojulikana baadae kama
''Germany Constabulary,'' na
mkuu wa jeshi hili alikuwa Affande Plantan baba yao Mwalimu Thomas Saudtz Plantan, Schneider
Abdilllah Plantan, na Ramadhani Mashado Plantan.
Wakati
wa Vita Vya Pili Mwalimu Thomas Plantan ndiye alikuwa rais wa African Association. Inasemekana huyu Affande Plantan alikuwa ndiye chifu wa Wazulu Mozambique na
ndiye aliyewekeana mkataba na Wissman kuja na jeshi la Wazulu kuiteka
Tanganyika. Mamluki hawa wa Kizulu walikuja na meli ya kivita ya Wajerumani hadi Pangani. Hapo ndipo yalipoanza mapambano yao na Abushiri na baada ya kukamatwa Abushiri ndipo jeshi likaelekea Kalenga kwa Chifu Mkwawa.
Katika
mswada wa kitabu alichoandika Kleist Sykes (1894 - 1949) kuhusu maisha yake, Kleist anaeleza kuwa mkataba ulikuwa Wazulu na
Wajerumani kuitawala Tanganyika kwa ushirika. Wazulu na ujuzi wao katika
medani ya vita uliwawezesha Wajerumani kuwashinda Abushiri bin Salim na Chifu Mkwawa. Wajerumani ndiyo
katika kuonesha shukurani yao kwa Wazulu walimfanya Affande Plantan kuwa mkuu wa
majeshi yao na wakaliita jeshi hilo ''Germany Constabulary.'' Haya kaeleza Kleist katika mswada wake.
Vilevile
waliwajengea shule watoto wa wanajeshi wao ambayo ilikuwa ilipo sasa Ocean Road Hospital ambako Kleist alisoma
hapo hadi darasa la sita na alipomaliza akaingizwa katika jeshi pamoja
na Schneider.
Wakati
wote wa utawala wa Wajerumani Waafrika hawa wakiishi ndani ya kambi ilikuwatenganisha
na wazalendo wa Tanganyika kwa falsafa ile ile ya wakoloni. Wagawe uwatawale.
Kwa hali
hii ya kutoa elimu kwa watoto wa askari katika jeshi la Wajerumani, hawa wakoloni
walifanikiwa kuwanyanyua juu Wazulu na Wanubi kiasi kuwa waliposhindwa Vita Kuu
ya Pili na Waingereza kuja sasa kuitawala Tanganyika, walioweza kupata kazi za maana
katika utawala mpya walikuwa hawa Wazulu na Wanubi ingawa katika vita ile
walipigana dhidi ya Muingereza katika jeshi la Wajerumani.
Watoto
wa hawa Wazulu walioingia Tanganyika na Wissman ambao walipigana dhidi ya Waingereza ambao kumbukumbu zao
zimehifadhiwa na akina Sykes na Plantan.
Katika
Vita ya Kwanza ya Dunia watoto wa hawa Wazulu walipigana chini ya uongozi
wa Von Lettow Vorbeck aliyekuwa wakati ule ndiye mkuu wa
majeshi ya Ujerumani Tanganyika.
Kleist ndiye alikuwa Aide de Camp wa Vorbeck.
Vorbeck alipoona kazidiwa nguvu na majeshi ya Waingereza
akishambuliwa na General
Smuts kutoka Afrika ya Kusini alivuka mpaka
akakimbilia Mozambique na baadhi ya askari wake wa Kizulu.
Kleist alikamatwa mateka na akawekwa kambi ya askari
mateka Dodoma.
Kitu cha
kuangalia ni kuwa hawa watoto wa Wazulu na Wanubi ambao walipigana dhidi ya
Waingereza ndiyo waliokuja kufanya mabadiliko makubwa katika siasa za
Tanganyika katika kudai
uhuru kutoka kwa Waingereza, uhuru ambao ni wa nchi ambayo ilikuwa yao kwa
kuhamia na wengine kwa kuzaliwa.
Mathalan Mwalimu Thomas Plantan na nduguze wote hawakuzaliwa Tanganyika
walikuja baada ya baba yao kuwa
keshajiweka vizuri nchini.
Kumbukumbu
zinaonyesha kuwa Mashado Plantan alikuja Tanganyika mwaka wa 1905.
Hawa
vijana wote wa Kizulu walikuwa katika African Association, Kleist akiwa muasisi
khasa na Schneider akiwa mwanaharakati wa kupigiwa mfano kwani
aliwataabisha sana Waingereza khasa wakati wa
Vita ya Pili ya Dunia (1938 - 1945) kiasi cha Waingereza kuamua
kumkamata na kumuweka kizuizini Mwanza alikofungwa hadi mwisho wa vita.
Mashado yeye alianzisha gazeti,
''Zuhra,'' na ndiyo ilikuwa sauti ya Mtanganyika wakati wa ukoloni.
Kleist ingawa alikuwa karibu sana na Waingereza
yeye alijiingiza katika siasa za kuwapinga Waingereza kichinichini na alipounda
African Association na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam
wa Tanganyika) chama alichokiasisi mwaka wa
1933 na rafiki yake wa Kimanyema, Mzee
bin Sudi.
Hawa
vijana wa Kizulu katika Tanganyika ile ya 1930 wao wakijiona bado ni askari
katika jeshi la Kijerumani na zaidi kwa kuwa wote walikuwa wakikisema Kijerumani kama
maji. Hili jambo bila shaka likiwakera
sana Waingereza.
Sidhani
kama hawa Wazulu na Wanubi walikuwa wakikerwa na ile sanamu ya kamanda wa baba
zao Hermann von Wissman.
Lakini
Vita ya Pili ya Dunia ilipoingia Abdulwahid Sykes na mdogo wake Ally walivaa sare za
majeshi ya King's African Rifles (KAR) kupigana na Wajerumani ambao
walikuwa washirika wa babu na baba yao.
Abdul na Ally walikwenda kupigana Burma dhidi ya Wajapani na
wote wawili walipewa medali ya ''Burma Star,'' na Waingereza baada ya
kwisha vita mwaka wa 1945.
Hizi ndizo athari za ukoloni. Kumbukumbu hizi tuzichukulie kama kumbukumbu katika
historia ya Tanganyika. Soko la Kariakoo ambako ndipo Waingereza walipokuwa
wakiwaandika kazi za upagazi babu zetu wakati wa vita bado lipo hali kadhalika Bismini na bunduki yake sanamu ile bado tunayo. Mimi
binafsi vyote hivi havinitaabishi hata chembe navitazama kama zilivyo -
historia yetu ambayo hatwezi kuikimbia hata kama tutataka.
Kuhusu
Diamond...
Kwa
kawaida mwanamuziki akifanya makubwa huwa anawekwa kwenye ''Hall of Fame,'' au
sanamu
yake inawekwa pale alipokuwa akifanyia muziki wake. Liverpool ipo sanamu ya The Beatles na Mephis ipo sanamu ya Elvis Presley.
![]() |
| Sanamu ya The Beatles Liverpool |
| Sanamu ya Elvis Presley |
![Click this image to show the full-size version. [IMG]](http://i1.liverpoolecho.co.uk/incoming/article10548696.ece/ALTERNATES/s615/JS78039909.jpg)
No comments:
Post a Comment