Sunday, 12 June 2016

KUTOKA JF: HISTORIA YA ZANZIBAR NA TANGANYIKA



Pasco,
Unataka kupiga ala bila kujifunza chromatics.
Unataka kuizungumza historia ya Zanzibar bila kusoma historia yenyewe.

Lakini kubwa ni kuwa hata ''intellect,'' yako ni tatizo kidogo maana hata
mtu akikusoma hili linamtokea dhahiri kabisa.

Ataliona jinsi michango yako inavyokosa mantiki na matokeo yake ni haya
ya kuchanganya mambo.

Unachokijua wewe ni, ''mapinduzi matukufu,'' huna kingine.

Nikikuwekea mabandiko ya kukufikirisha unapotea kwa muda kisha unaibuka
na jambo lingine kabisa lile unalikimbia.

Ni kweli waliofungwa jela za Bara walinusurika kuuawa.
Lakini iweje umshukuru mtu aliyekukata mkono kwa kukurudishia kidole gumba?

Jana nilikuwa Zanzibar kutoa mada kuhusu Sheikh Hassan bin Amir.
Walionialika ni Mwinyi Baraka Foundation.

[​IMG]

Kongamano la Mwinyi Baraka Foundation 12 June 2016 Ukumbi wa Baytul Amiyn

Sheikh Hassan bin Amir ni Mzanzibari na alishiriki katika kuunda TANU na ni
mmoja wa wajumbe wa TAA Political Sub Committee 1950 wajumbe wengine
wakiwa, Dr. Kyaruzi, Abdul Sykes, Stephen Mhando, Hamza Mwapachu,
Said Chaurembo 
na John Rupia.

Sheikh Hassan bin Amir ndiyo aliyiongoza TANU kuwa ''a nationalist secularist
party,'' baada ya kufanya mkutano wa siri Mtaa wa Pemba Dar es Salaam na
baadhi ya viongozi wa TANU mwaka wa 1955 wakiwamo Rajab Diwani, Sheikh
Abdallah Chaurembo, Sheikh Nurdin Hussein
 na wengineo.

Sheikh Hassan bin Amir alikuwa Mufti wa Tanganyika hadi alipofukuzwa na
Nyerere mwaka wa 1968 na kurudishwa Zanzibar na kupigwa marufuku 

kukanyagaTanganyika baada ya ''mgogoro,'' wa East African Muslim Welfare
Society (EAMWS) uliopelekea kuundwa BAKWATA.

Lakini baada ya Sheikh Hassan kufariki mwaka wa 1979 Nyerere alihudhuria
hitma yake Msikiti wa Mtoro alialikwa na Sheikh Abdallah Chaurembo na
Sheikh Kassim Juma.

Mimi nilikuwapo hapo msiktini siku hiyo.

Ikiwa huyajui haya kwa undani maisha utahangaika na historia ya Tanganyika
kwani huu ndiyo msingi unaosimamisha si historia ya Nyerere bali historia nzima
ya uhuru wa Tanganyika na baada yake.

Pasco,
Hebu jitulize na isome historia kwanza kabla hujataka kupambana na mimi.
Watoto wa mjini wana Kiswahili chao.

Wanasema, ''Mimi si saizi yako.''
Maana ukinivaa utapwaya.

No comments: