Abbas Kleist Sykes
| Balozi Abbas Sykes akihojiwa na mwandishi katika kipindi cha televisheni nyumbani kwake Sea View |
| Aliyesimama Nyuma ya Masheikh ni Abbas Sykes na Waliokaa Kulia ni Sheikh Omar bin Sumeit na Kushoto ni Sheikh Ahmed bin Hussein Wakati hii miaka ya mwanzoni 1960 Abbas Sykes Alikuwa Regional Commissioner wa Jimbo la Jimbo la Mashariki |
![]() |
| Kushoto Kwenda Kulia: Kanyama Chiume, Kaluta Amri Abeid, Hastings Kamuzi Banda, Abbas Sykes (Nyuma katikatio ya Banda na Nyerere) na Julius Nyerere |
| Abbas Sykes Siku ya Khitma ya Kaka Yake Ally Sykes Akisalimiana na Watu Waliokuja Kwenye Dua |
| Abbas Sykes Akiwa Katika Maktaba Yake Nyumbani Kwake Sea View |
![]() |
| Kabaka Mutesa |
Ilikuwa Nairobi katika miaka ya katikati ya 1940 wakati Abbas Sykes anapelekwa na baba yake, Kleist Sykes kwenda kusoma King's College Budo, Uganda:
''Tulikuwa hotelini Nairobi mimi na baba tuko njiani kuelekea Kampala. Pale hotelini baba akakutana na jamaa wa Kinubi na katika maongezi baba akawaeleza kuwa alikuwa katika safari anaelekea Uganda kunipeleka mimi shule. Basi mmoja wao akamwambia baba kuwa shule nzuri sana ni King's College Budo itakuwa vyema kama anatanipeleka shule hiyo. Hapo King's |College Budo ndipo nilipokuja kusoma darasa moja na Freddie Mutesa ambae baadae akajakuwa Kabaka wa Buganda na Rais wa Uganda mwaka 1962.''
''Tulikuwa hotelini Nairobi mimi na baba tuko njiani kuelekea Kampala. Pale hotelini baba akakutana na jamaa wa Kinubi na katika maongezi baba akawaeleza kuwa alikuwa katika safari anaelekea Uganda kunipeleka mimi shule. Basi mmoja wao akamwambia baba kuwa shule nzuri sana ni King's College Budo itakuwa vyema kama anatanipeleka shule hiyo. Hapo King's |College Budo ndipo nilipokuja kusoma darasa moja na Freddie Mutesa ambae baadae akajakuwa Kabaka wa Buganda na Rais wa Uganda mwaka 1962.''
Abbas Sykes Katika Kamati ya Saadan Abdu Kandoro na Japhet Kirilo Kuchangisha Fedha ya Kupeleka Mjumbe UNO
September 1953
''Uongozi
wa TAA Makao Makuu ulianza kampeni ya nchi nzima kuueleza umma matokeo ya
safari ya Kirilo kwenye Umoja wa Mataifa kuhusu mgogoro wa ardhi ya Wameru na
vilevile kuchangisha fedha za kupeleka msafara mwingine katika Umoja wa Mataifa
kuueleza umoja huo kuwa Tanganyika ilikuwa chini ya udhamini na Watanganyika
walikuwa sasa na haki ya kudai uhuru wao. Kamati ya TAA ya watu watatu
iliyowajumuisha Kandoro, Kirilo na Abbas Sykes iliundwa kwa ajili hiyo. Ally
Sykes akiwa mweka hazina msaidizi wa TAA aliombwa ampelekee Kirilo hawala ya
posta Usa River kama nauli ya kumwezesha kusafiri hadi Dodoma kujiunga na ile
kamati ya watu watatu. Kulikuwa hakuna huduma ya fedha katika posta ya Usa
River na fedha zile zilikaa hapo kwa muda bila ya kuchukuliwa hadi hapo
zilipopelekwa posta ya Arusha mjini ambako Kirilo alizichukua.[1] Kuanzia tarehe 26 Septemba, 1953 kwa takriban
mwezi mmoja ile kamati ilitembelea na kuhutubia mikutano ya hadhara, ikikusanya
fedha Dodoma, Mwanza, Bukoba, Ukerewe, Tarime, Musoma na Shinyanga. Rais wa
chama cha TAA, kanda ya ziwa, Paul Bomani aliipokea ile kamati ya watu watatu
na kuhutubia mikutano pamoja nao katika jimbo lote. Bomani aliwaambia wanachama
wa TAA na wananchi wote mjini Mwanza kuhusu umuhimu wa kuchanga fedha kwa kwa
kusudio hilo.''
Abbas Sykes na Picha ya Waasisi wa TANU, New Street 1954
![]() |
| Waasisi wa TANU TAA Headquarters, New Street Dar es Salaam |
| Kushoto Dossa Aziz, Kulia Abdulwahid Sykes |
''Kuna
picha mashuhuri sana ya wanachama waasisi wa TANU. Katika picha hiyo wanachama
watatu hawaonekani, Ally Sykes, Tewa Said Tewa na Kasella Bantu. Hawa walikuwa
watumishi wa serikali na kwa kanuni za utumishi katika serikali ya Kiingereza,
watumishi wa serikali walikuwa hawaruhusiwi kujihusisha na siasa. Mwafrika
yoyote aliyevunja amri hiyo kuu adhabu yake ilikuwa kufukuzwa kazi mara moja.
Kwa hiyo picha hiyo ilipopigwa Ally, Tewa na Kasella Bantu walijondoa. Picha
hiyo ilipigwa na Gomes mpiga picha maarufu sana wa Ki-Goa katika siku zile.
Abdulwahid alikuwa amepatana na Gomes aje makao makuu ya TAA kupiga picha hiyo
ya historia. Kwa bahati mbaya Gomes alichelewa kufika ofisi ya TAA. Abdulwahid
alikosa subira kwa hiyo, alimwomba mdogo wake Abbas kwenda kumchukua Gomes
kutoka kwenye studio yake Acacia Avenue (siku hizi Samora Avenue) katikati ya
mji. Chombo pekee cha usafiri walichokuwa nacho TAA ilikuwa baiskeli moja
iliyochakaa. Wakati Abbas ananyonga baiskeli kuelekea mjini kumchukua Gomes,
Gomes alikuwa keshaondoka anakuja makao makuu ya TAA; kwa hiyo wakaipishana
njiani. Hivi ndivyo Abbas Sykes alivyokosa kuwepo ndani ya picha hiyo
mashuhuri.''
August 1954
Kiasi cha kama juma moja baada ya kuundwa kwa TANU Zuberi Mtemvu akamwambia Nyerere waende Morogoro wakakitangaze chama:
''Mtemvu alimuelezea Ally kwa ufupi juu ya mkutano wao na Nyerere Morogoro mjini na aliomba apewe mara moja kadi 200 za TANU. Ally aliwaandikia na kuwapa kadi za uanachama wa TANU, Mtemvu na Tambwe na akamwambia mdogo wake Abbas, awaalike wote wawili kwenye mkutano wa uzinduzi wa tawi la TANU la Dar es Salaam ambao ulikuwa ufanyike Jumamosi iliyofuata...Mkutano
wa uzinduzi wa TANU ulihudhuriwa na kikundi kidogo cha takriban watu 20
miongoni mwao Julius Nyerere, Abdulwahid na Ally Sykes, Dossa Aziz, John Rupia,
Mshume Kiyate, [1]
Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajabu Diwani,
Schneider Plantan, Marsha Bilali, Rashid Ally Meli, Frederick Njiliwa, Iddi
Faiz Mafongo, Iddi Tulio, Denis Phombeah na wengineo...''
Basi la Majigo, 1952/53
Nyerere alikuwa akija Dar es Salaam kutoka Pugu alikuwa anapanda basi moja la Muhindi. Kituo cha basi hili kilikuwa Mtaa wa Msimbazi na Aggrey. Ukiingia na mzigo ndani ya basi basi yule Muhindi utamsikia akipiga kelele, ''Majigo juu, majigo juu.'' Maana ya maneno haya ilikuwa, ''Mzigo juu.'' Yaani mizigo ipandishwe juu ya basi kwenye ''carrier.'' Hivi ndivyo basi lile lilivyopta umaarufu wake na kuishia kuitwa ''Majigo.' Hiki kilikuwa kipindi kabla ya Nyerere hajajiuzulu ualimu. Nyerere alikkuwa akishashuka pale kwa Majigo atashika njia kuelekea Kariakoo Market kwa Abdulwahid Sykes ambae wakati ule alikuwa Market Master. Ilikuwa katika kipindi hiki ndipo Abbas Sykes alipojuana na Nyerere na Nyerere alipojiuzulu ualimu alikuja akakaa nyumbani kwa Abdulwahid Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukukuu na hapo ndipo alipokujajuana zaidi na Abbas Sykes kwa kuwa wakati ule Abbas alikuwa anakyaa kwa kaka yake.
Abbas Sykes Aliponihadithia Ufukura Uliomkuta Dossa Aziz Mwisho wa Maisha Yake
Fatilia hapa...
Fatilia ukurasa huu.
Tunatengeneza...
Kwa kipindi cha zaidi ya miaka thelathini si CCM wala si rafiki yake mpenzi Julius Nyerere alikuwa anafahamu Dossa anaishi vipi na ana hali gani. Rafiki zake wachache waliokuwa wakimtembelea nyumbani kwake pale Mlandizi walihuzunishwa na hali yake. Dossa mtu aliyekuwa na mali katika miaka ya 1950 alikuwa akiishi katika hali ya ufukara. Hali hii ya ufukara ilitaka kumkosesha kuhudhuria Mkutano Mkuu wa CCM mwaka 1987 pale Kizota ambapo waasisi wote wa TANU walialikwa. Sababu kubwa ilikuwa ni ukosefu wa nguo na viatu vya kuvaa katika hadhara kama hiyo. Ilikuwa mmoja wa marafiki zake wa zamani Abbas Sykes ndiye aliyemnunulia nguo na viatu vya kumwezesha kwenda Dodoma. Rafiki zake walipomshauri aende kwa Nyerere ampatie msaada Dossa alijibu kuwa yeye hawezi kulifanya hilo kwa kuwa Nyerere anajua kuwa yeye alitumia fedha zake nyingi katika harakati za kudai uhuru na kama yeye Nyerere leo kamsahau yeye hana sababu ya kumfuata. Jibu la Dossa lilikuwa jibu la muungwana, mtu asiyekubali kujidhalilisha.
Abbas Sykes na Kumbukumbu ya Baba Yangu Said Salum Abdallah
Katika Dar es Salaam ya Miaka ya 1950
Katika Dar es Salaam ya Miaka ya 1950
Ukumbi wa Abbas Sykes umepambika vyema na ukiwa kwenye ukumbi wake unaiona Bahari ya Hindi kwa uzuri kabisa na upepo mzuri unakupiga.
Lakini kitu cha mvuto ni kitambaa cheusi cha Al Kaaba ambacho kakiweka katika fremu kubwa pale ukumbini. (Balozi Sykes anasema ameingia hadi ya Kaaba na aliyemfanyia itifaki hiyo alikuwa Balozi Abdallah Sued wakati alipokuwa balozi wa Tanzania Saudi Arabia). Hapo ukumbini kama ni msomaji wa magazeti utapambana na kila aina la chapisho kuanzia magazeti ya ndani hadi ya nje ya nchi.
Siku ile jicho langu liliangukia kwenye video inayoitwa, ''High Society,'' ni senema ya zamani sana katika miaka ya 1950. Kwa kitambo kirefu niliishika ile video na nikawa kama imenitoa pale. Bwana Abbas alililiona lile akanambia, ''Mohamed mimi na baba yako tulitoka Kipata kwenda Avalon Cinema kwa miguu kuangalia film hiyo.''
Kuna kisa katika hiyo video.
Katika film ile kuna wachezaji nyota wa senema na wanamuziki wa wakati ule kama Bing Crosby. Huyu alikuwa muimbaji mahiri sana. Mwingine ni mpiga muziki wa jazz Louis Armstrong, Frank Sinatra ambae na yeye alikuwa mwimbaji maarufu.
Hapa ndipo nataka nisimame kidogo nirudi nyuma mwaka 1964 siku ya Eid El Fitr. Nilikuwa na umri wa miaka 12 na siku ya Eid kwetu watoto ilikuwa siku maalum sana maana ndiyo siku tuliruhusiwa kurudi nyumbani usiku kama saa tatu hivi kutoka kutembea. Kulikuwa na jumba la senema maarufu Dar es Salaam likiitwa Empire Cinema. Empire Cinema walikuwa wameweka tangazo, ''Eid Attraction Elvis Presley in Blue Hawaii.'' Elvis Presley ndiyo alikuwa kipenzi chetu vijana. Alikuwa ''pop star'' hakuna wa kumshinda. Kwa enzi hizi za sasa hadhi yake ilikuwa sawa na Michael Jackson.
Siku ya Eid ilipofika mimi na rafiki zangu tukenda kuangalia hiyo film ''Blue Hawaii'' ya Elvis.
Sasa asubuhi wakati nakunywa chai na baba mimi stori yangu ikawa Elvis, Elvis Elvis...
Baba yangu akanambia, ''Sisi tulipokuwa watoto ''hero'' wetu alikuwa Bing Crosby.''
Ndipo hapo nikalishika hili jina na siku ile nilipoiona ile video nyumbani kwa Balozi Abbas Sykes ikanikumbusha kisa changu cha utoto cha Elvis na marehemu baba yangu.
Mkasa bado haujakwisha.
Kisa hiki cha video ya ''High Society'' nikamuhadithia rafiki yangu Harith Ghassany.
Sasa sikumbuki vyema kama wakati ule Harith alikuwa Muscat au Washington lakini siku alipokuja Dar es Salaam kunitembelea akaniletea audio CD mbili za muziki wa Bing Crosby akanambia, ''Guy nimekuletea hizi CD kumbukumbu ya mzee.''
| Said Salum Abdallah |
Re: Tanganyika(TANU) imetoka mbali waasisi wake wengi wao wametangulia mbele ya haki






Edit Post

No comments:
Post a Comment