
Prof. Malima
| Mwalimu Athmani Khalfani Mrindoko Mwalimu ya Shule ya Msingi na Mwalimu wa Kusomesha Qur'an Kielelezo kimojawapo cha Udini na Dhulma Anakabiliwa na Kesi ya Kubambika ya Kujeruhi Soma Habari Zake |
![]() |
| Sheikh Rajab Chambuso Mwalimu wa Madras Anakabiliwa na Kesi ya Kushawishi Mauaji Soma Habari Zake |
| Sheikh Ponda Issa Ponda Akiwa Ameelekea Kibla Msikiti wa Kichangani Akiomba Dua Kabla ya Kuongoza Maandamno Dhidi ya NECTA iliyokuwa Ikihujumu Shule za Kiislam Katika Mitihani Sheikh Ponda Amepigwa Risasi Alipokuwa Morogoro kwa Mwaliko wa Waislam na Yuko Mahabusi Akisubiri Kesi |
![]() |
| Rashid Zahaki Aliyefukuzwa Jeshi la Polisi kwa Kupinga Mauaji ya Waislam Mwembechai 1998 |
| Suleiman Mamba Aliyepigana Katika Vita ya Majimaji 1905 - 1907 Dhidi ya Wajerumani Kupinga Dhulma |
| Sheikh Kassim Juma Alipotoka Rumande 1993 |
Nimekuwa nikichangia katika ukumbi huo kwa muda mrefu na Alhamdulilah nimekuwa maarufu khasa kwa kuwa nimeingia bila ya kuficha jina langu khalis.
Wengi wa wachangiaji wanazungumza nyuma ya pazia wakitumia majina ya bandia.
Nimejitahidi kwa kiasi alichoniwezesha Allah kueleza ukweli katika yote ambayo Waislam walikuwa wakishambuliwa.
Mathalan kuwa Waislam hawana mipango katika elimu, Waislam ni wavivu nk.
Haikupita muda michango yangu (na kuna vijana wengine wakaniunga mkono) ikawa maarufu na ikaleta changamoto mpya ndani ya ukumbi wa JF.
Wakati mwingine hutukanwa, kubughudhiwa, kutishwa, kukejeliwa na kadhalika. Lakini mimi na wenzangu hatukuacha.
Wenyewe husema tunatoa darsa kuwaelimisha ndugu zetu ambao hawakuwa hata wanaijua historia ya Tanganyika.
Kwa hakika tuliwashtua wengi wakati tukitaja majina ya waliopigania uhuru wa Tanganyika ambao walikuwa wao hawajawasikia toka kuzaliwa...Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir, Jumbe Tambaza, Tatu biti Mzee, Mama biti Maalim, Bi. Halima Selengia nk nk. Tena tukiandika na wasifu wao kamili.
JF Jukwaa la Siasa likashamiri na sisi wachangiaji tukang'ara pia na Uislam sasa ukawa unaagaliwa kwa sura nyingine.
Nakumbuka katika moja ya mjadala nilisema hotuba ya Nyerere UNO 1955 iliandikwa na akina Abdulwahid Sykes 1950 hii nusra iwaue ndugu zetu.
Sijapatapo kuona JF kuumia na kulipuka kama katika hili.
Sasa maswali yalivyorushwa kwa hasira ndipo majibu yakawa yanakuja moja baada ya jingine kwa utaratibu na kwa lugha ya kuoendeza.
Walikuwa hawajui kuwa hata hiyo TANU hakuanzisha Nyerere...
Walikuwa hawajasikia kuwa kulikuwa na TAA Political Subcommittee ikiwa chini ya Sheikh Hassan bin Amir...
Tuishie hapa nadhani msomaji umepata picha ya JF ni akina nani na nini sera zao.
Sina haja ya kukueleza kuhusu watu gani wengi Waislam au Wakristo...jibu tuliwapa katika historia ya Tanganyika.
Iweje ''minority'' wakomboe nchi?
Hivi majuzi JF wameweka bandiko ambalo nia yake khasa ilikuwa kumdhalilisha marehemu Prof. Malima.
Mimi na wenzangu tukaenda jamvini kumtetea marehemu kwani hayupo na kwa hiyo hana wa kumsemea.
Asiye na Mtu ana Allah.
Majibu yalipoanza kushuka haraka ule uzi ukafungwa.
Wamefunga kwa sababu ukweli ulikuwa unawachoma.
Ukweli na ushahidi wa ukweli ule uliwatisha pasi kiasi.
Walizungumza kuhusu udini wa Prof. Malima...
Sisi tukaweka ushahidi wa nani mdini.
Leo asubuhi nimewawekea hapo JF ushahidi wa udini katika serikali na hatari ya Mfumokristo.
Hata kabla sijamaliza bandiko langu limefutwa.Ndipo nakaona niwajulishe wasomaji wangu kuwa si kweli kuwa JF ''talk openly...''
Kizazi hiki tutakirithisha nini?
Dhulma ya Jeshi la Polisi?
Dhulma ya NECTA?


3 comments:
Mzee Mohamed Said tunakupongeza kwa kazi yako tukufu. Na tunakuomba usichoke.
Amma kwa hakika UKWELI UNAUMA MNO!
Na hili linaonekana wazi. Na hii ni moja ktk misukosuko walokutana nayo WASEMA KWELI.
Tunakuombe Mungu akuongeze nguvu na afya ili uendelee kuelimisha Ummah.
Amin
Amin
Post a Comment