Uonevu na udini upo Tanzania
Na Alhaj Aboud Jumbe
HOJA zimekuwa
zikijengwa kuwa nchi yetu imefanikiwa kujenga utaifa ambapo hakuna ubaguzi wa
kidini au kikabila. Aidha, Mtanzania yeyote ukimuuliza atakuambia kuwa serikali
yetu haina dini. Kwa mtazamo huo viongozi hawaongozi kwa utashi wa dini zao
kuwahujumu wananchi wasio katika dini moja.
Wanasiasa wanapotoa
shutuma dhidi ya watu, wanaodai wana udini, taswira inayojengwa ni k uwa
Muislamu ndiye mdini, bali Mkristo hawezi kuwa mdini.
Ndio maana japo
serikali yaweza kuwa imejaa Wakristo ikilinganishwa na Waislamu, haionekani
kuwa ni tatizo.
Aidha, ndio maana
uongozi wa juu wa CCM una Wakristo wengi, lakini hausikii CCM ikiambiwa ni
chama cha Wakristo au kina udini. Lakini inapotokea chama kingine, kuwa na
viongozi Waislamu basi hubatizwa kuwa chama cha kidini.
Si wananchi wote
wanayoyatazama mambo kwa mtizamo huu. Wako wanaotoa hoja kuwa ubaguzi wa kidini
umekuwa ukifanyika, lakini kwa ustadi mkubwa.
Alhaj Aboud Jumbe,
Rais mstaafu wa Zanzibar ,
ametoa hoja kuonyesha kuwa Waislamu hawatendewi haki na kwamba Kanisa Katoliki
limepewa fursa ya pekee nchini.
Sehemu katika
kitabu chake inasema:
MTIRIRIKO wa
matukio ya kisiasa unaashiria agenda ya siri ambayo inaelekezwa kutumikia
Kanisa Katoliki ambalo siku zote linakuwa na uhusiano wa karibu na serikali
(hii) yenye kujenga mtizamo wa Kikristo ya Jamhuri ya Muungano na huku Waislamu
wakihasirika.
USHAHIDI uliopo
unaonesha kuwa Waislamu wa Tanzania Bara wamekuwa na uonevu ulioendelea na
kukoseshwa haki zao za msingi pamoja na kuwa katiba ya mwaka 1977 ilikuwa na
vipengele vya kuhakikisha haki za binadamu na usawa kwa raia wote.
Ushahidi wa ziada
unaonesha Kanisa nchini Tanzania
ndilo linatowa maelekezo ya kisiasa na mfumo wa kisiasa umekuwa ukitumiwa kutoa
upendeleo kwa Wakristo ambao tayari wamo katika kudhibiti nafasi mbalimbali
katika asasi za umma.
Kama tukichukulia
maendeleo ya hali ya kisiasa nchini hivi sasa kuhusiana na Muungano nina hakika
ya kuwa na shaka kuwa utaratibu mzima wa kuwabana Waislamu wa Tanzania Bara
unaendeshwa kwa mbinu za mchwa sambamba na ule wa kuikaba Zanzibar ili
kuilazimisha kuingia katika mpango wa muda mrefu wa kuiingiza katika serikali
moja ili kuhakikisha Waislamu kutoka pande zote mbili za Bahari ya Hindi hapa
Tanzania wanasujudu kwa Bwana mmoja.
Sura hii
inataftishi suala la dini na siasa katika Jamhuri ya Muungano. Mada hii huenda
ikawaudhi baadhi ya watu. Lakini siku zote ukweli hauwafurahishi wale ambao
hawapendi ujulikane kwa sababu zinazoeleweka ambazo ni za kuchukiza za
kibinafsi na zenye makusudio maovu.
Tangu nusu ya pili
ya mwaka 1993 mashambulizi mbalimbali yasiyo na msingi yamekuwa yakielekezwa na
kuongezewa nguvu dhidi ya Waislamu maalum, lakini pia kwa Uislamu kwa jumla.
Mashambulizi ya
awali yaliyofanywa na mtu binafsi, vikundi vya watu, vyombo vya dola na mwisho
vyombo vya habari yalielekezwa kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kujiunga na Jumuiya ya Mkutano
wa Kiislamu (OIC).
Hii ilikuwa ni
rasharasha tu ya mabomu kabla ya matusi hasa hayajafuatia baadae. Katika muda
huo huo lilipitikana jaribio lililoshindwa ambapo uvumi usio na msingi
ulienezwa kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano ilitaka kujiunga na Jumuiya
nyingine ya Kiislamu inayoitwa Islam in Africa Organization (IAO), hili likitowa
mwanga, mashambulizi haya yalipangwa kulenga shabaha gani. Na ilikuwa wazi kuwa
waliojikita katika majadiliano hayo hawakuelekeza mabishano yao nje ya Uislamu na Waislamu.
Kwa mfano, kuwepo
kwa ubalozi wa Vatican nchini Tanzania
hakukupata kuhojiwa pamoja na kuwa serikali hii inadai kuwa si ya kidini.
Kanisa, CCM na serikali vyote vimekaa kimya huku vikijua kutendeka kwa hilo lakini vikizibwa
mdomo.
Kana kwamba hiyo
haikutosha kuonesha kuwa kuna mlalio dhidi ya upande mmoja, kulifuatia jaribio
la kumng'oa Rais Mwinyi kupitia taratibu za Bunge, kudai kufukuzwa Rais wa
Zanzibar Dk. Salmin Amour na baadhi ya Mawaziri wake na kelele za kuwataka
mawaziri Waislamu katika Jamhuri ya Muugano wajiuzulu kwa kutaka kusilimisha Tanzania ,
inaonesha malengo ya mashambulizi hayo.
Mkakati ukaandaliwa
ambao ulitakiwa kuonesha kuwepo "kwa hila za Kiislamu" ili kujenga
hoja ya kuwasaka Waislamu ambao walionekana kuwa kero isiyostahimilika. Fursa
ilipopatikana basi ikatumiwa haraka. Uchokozi mbalimbali dhidi ya Waislamu ambao
mwengine haukuripotiwa ukaanza kuzua hisia tofauti za wakandamizaji na
wakandamizwaji kufuatia na ukamataji mkubwa na kesi katika mahakama ambazo
baadhi yake zimekuwa zikiendelea kwa muda mrefu.
Matukio haya
yamedhihirika kwa Waislamu wengi kuwa kumekuwa na hatua za makusudi kuchanganya
siasa na dini katika mambo ya serikali.
Kinyume na kampeni
inayosambazwa, Waislamu sio chanzo ila wao ni waathiriwa wa mbinu za makusudi
za kujenga mfumo wa uhasama ambao unazinyonya dini zote mbili na siasa ili kuwabana
Waislamu na pia kupata uwezo wa kuwakandamiza.
Dhana ya
kutenganisha dini na siasa katika wakati huu ilianzishwa na baadhi ya nchi za
Magharibi ili kuanzisha taifa lisilo na dini ili kuepuka uingiliaji wa Kanisa
ambao wakati huo ulikuwa ni mkubwa.
Awali kitendo kama
hicho kilionekana kama ni cha upinzani juu ya mamlaka ya Papa ambae alikuwa
ameigawa dunia, upande wa magharibi ukiwa kwa Uhispania iliyokuwa na nguvu na
upande wa mashariki kwa Ureno ambayo pia ilikuwa na nguvu na kuyaacha mataifa
makubwa ya Ulaya yakiwa yanakosa pahala pa kushika katika zama hizo.
Utaifa mpya katika
bara la Ulaya ulipingana na Papa na kundi lake kwa
kuanza kuvamia maeneo yaliyokuwa chini ya Uhispania na Ureno. Sio tu walianza
kujitangazia mamlaka zao huru, lakini pia walianza kujikatia maeneo mapya nje
na ndani ya Ulaya.
Baada ya kufanikiwa
kuunda mataifa yao walianzisha pia Makanisa yao ambayo yalikuwa na
lengo moja la kukuza dini. Kidogo kidogo mataifa haya "yasiyokuwa na
dini" yalianza kupeleka baadhi ya madaraka kwa wafalme, malkia na wabunge.
Wakati ambapo kuna
mgawanyo unaoeleweka na ulio wazi baina ya mamlaka ya kiroho na kiserikali kwa
upande wa dola na Kanisa, taasisi mbili hizo hazijaweza kusita kuingilia mambo
ya kidini, kiuchumi na kisiasa katika nchi zinazoendelea na kusababisha hali ya
kutoelewana, kutoaminiana, kukosekana kwa utulivu na pia kusababisha fujo
wakati wa utekelezaji wa mipango yao ya kihaini.
Hili hutokea zaidi
pale kunapokuwa na idadi kubwa ya Waislamu na Wakristo wanapoishi pamoja.
Tunaushahidi wa kutosha na usiopingika juu ya jambo hili kwa Tanzania .
Upitizi wa makini
wa kitabu "Kanisa Katoliki na siasa Tanzania Bara 1953-1985" unatoa
habari za ndani zisizo za kawaida juu ya kampeni dhidi ya Uislamu.
Kwa maneno mengine
kitabu hicho kwa kiasi fulani ni kukiri kwa yeye mwenyewe mwandishi juu ya
shughuli za Kanisa la Katoliki za kisiasa Tanzania ,
Kanisa ambalo haliwezi kutenganishwa na Vatican na ambalo ubalozi wake ni mmoja
katika balozi kongwe nchini Tanzania .
Kwa sababu
zisizoeleweka kitabu hiki kimeandikwa na kuchapishwa na waumini wa Kanisa hilo . Yaliyomo ndani ya
kitabu hicho hayajakanushwa wala kubishiwa na serikali ya Muungano ya Tanganyika au CCM, huu ukiwa ni ushahidi kamili
juu ya ukweli wa kukiri juu ya neno hilo .
Kwa sababu na malengo
yoyote ya kutolewa kitabu hicho , na lazima ziwepo sababu za msingi za kufanya
hivyo, kitabu hiki ni ufunuo mzuri juu ya mbinu za chini kwa chini za Kanisa
katika medani ya kisiasa Tanzania .
Kitabu kinaeleza ni
Kanisa Katoliki lililojenga njia ambazo ziliwawezesha kuwa na mahusiano ambayo
kitabu hicho inaeleza yalikuwa ya karibu kabisa na TANU wakati wa miaka ya
kupigania uhuru. Kinaonesha ni vipi Kanisa lilitayarisha waumini wake shupavu
ambao walikuwa wameshika karibu nafasi zote muhimu katika serikali mpya ya
Kiafrika ya Tanganyika .
Kinaeleza ni vipi
serikali ya Jamhuri ya Muungano ilirithi mfumo huo, na kuupanua kuingia katika
mamlaka ya Muungano na pia katika mambo yahusuyo Tanganyika . Na hapa tunaweza kupata
mwanga juu ya maana na ulazimishaji wa kuwepo serikali mbili badala ya tatu kwa
njia zilizogubikwa kama ilivyobainishwa na mkataba wa Muungano (mapatano ya
Muungano) na katiba zote zilizopitishwa Tanzania .
Hapa ndipo unapoona
kuna neno katika kudai kusimamishwa mfumo wa serikali moja. Nguvu hizo
zikapenya zaidi kupelekea Muungano wa ASP na TANU ambapo CCM iliendeleza kazi
za TANU kuhusiana na ushirikiano wa karibu na Kanisa Katoliki.
Kwa wale viongozi,
wawe wa Kanisa, CCM au serikali ya Muungano ambao walikuwa wakijipigia kelele
kutenganisha kwa siasa na dini, lakini wao wenyewe wakiwa ndio waendelezaji
wakubwa wa hilo ,
wana kazi ngumu ya kuelezea kwa umma kwa ujumla lakini zaidi kwa Waislamu.
Sivalon anaelezea juu ya mpango na njama zinazoendelea zikishirikisha Kanisa
Katoliki, Chama (TANU-CCM) na serikali ya Muungano.
Tangu njama hizo
ziwekwe wazi 1992 hapakuwa na kauli moja ya kupinga au kutolea maelezo juu ya hilo . Huku ni kukiri kwa
dhahiri juu ya mipango na njama za Kanisa zinazofanywa hali zikiwa zinaeleweka
na mkono wa chama na serikali yake.
Yafuatayo ni baadhi
ya madondoo kutoka kitabu hicho:
"Mwishowe
tutakuja kuonesha jinsi Rais mstaafu Nyerere alivyokuja kuwa kiungo cha pekee
kati ya chama/kanisa na Kanisa Katoliki. Uhusiano huo unaelezwa kwanza kama
msingi wa kuelewa jinsi gani na kwa kiasi gani viongozi wa Kanisa
walivyoingilia kati maendeleo ya siasa hapa Tanzania (uk. 5).
Huo uhusiano
ukawaweka viongozi wa Kanisa katika nafasi nzuri ya kuelekeza maelekezo ya
siasa Tanzania .
(uk. 9).
| Sheikh Ali Basaleh |
| Kitabu Cha Sheikh Aly Basaleh, Kwa Nini Waislam Wanalalamika |
![]() |
| Sheikh Ali Basaleh |

No comments:
Post a Comment