![]() |
Maalim Mohamed Matar |
Historia ya African Association, TANU na historia nzima ya kudai uhuru wa
Tanganyika ina mashujaa wake halikadhalika ina wengine ambao ingawa
hawakuwa katikati ya jukwaa lakini walikuwa washiriki katika nafasi ile ya
utazamaji.
Siku chache zilizopita baada ya Yericko kuzungumza kuhusu nafasi ya rais
katika TAA hili lilinifanya nifikiri na ndipo yakanijia majina ya wazalendo
wengi ambao ingawa hawakuwa na nafasi ya uongozi kama uongozi hivi
leo unavyotambulikana lakini walifanya makubwa katika kuijenga TANU na
katika kupigani uhuru wa Tanganyika.
Mathalan Sheikh Hassan bin Amir au Hamza Mwapachu.
Ndipo katika bandiko langu kumjibu Yericko nikamueleza habari za Hamza
Mwapachu.
Mwapachu hakuwa na nafasi katika TAA pale Makao Makuu New Street wala
jina lake halipo katika wale waasisi 17 wa TANU lakini hayo yote kwa hakika
yasingepatikana bila ya mchango wake wa fikra kuanzia miaka ya mwishoni
1940.
Sasa watu kama Yericko wako wengi sana ambao hawaijui historia ya uhuru
na kwa hakika hatuwezi kuwalaumu watu kama hawa kwani wataijuaje historia
hii ikiwa haikuandikwa?
Tutawalaumu pale tu watakaposomeshwa historia ya kweli na wao wakafanya
ukaidi.
Turudi kwa kisa hiki cha Abdallah Kassim Hanga.
Waliokuwa karibu ya Mwalimu Nyerere wanasema kuwa baada ya kupata
taarifa za kuuliwa Hanga, Nyerere alihuzunika sana.
Inasemekana haikumptikia kabisa Nyerere kuwa Hanga atauliwa.
Bado iko nafasi kubwa sana kwa wanahistoria hasa wazalendo kutafiti na
kuandika historia ya Tanzania kama inavyostahili kuandikwa.
In Sha Allah ukipatikana wasaa na sababu nitamueleza Maalim Mohamed
Matar.
Nini kiliwafanya Hanga, Nabwa na yule mpashaji habari wangu waende kwake
kumuomba amombee Mungu Hanga?
Baada ya kukamatwa kwa Hanga haukupita muda mrefu Maalim Matar
alikamatwa na kuwekwa kizuizini Ukonga Prison lakini kukamatwa kwake
hakukuwa na uhusiano wowote na mkasa wa Hanga.
No comments:
Post a Comment