Saturday, 20 June 2015

DARSA YA RAMADHAN TAFSIR YA QUR'AN MASJID JUMUIYATIL ISLAMIYA UBUNGO


Sheikh Majid Akidarsisha Masjid Jumuiyatil Islamiyya Ubungo



https://ssl.gstatic.com/ui/v1/icons/mail/images/cleardot.gif
Leo Chungu Tatu Ramadhan 1436 Dhuhr imenikuta Ubungo/Mandela. Takbir za sala nazisikia zikirindima kutoka vipaza sauti lakini msikiti wenyewe siuoni. Nikauliza na nikaelekezwa. Msikiti mkubwa unajengwa lakini pembeni Waislam wameweka msala wasali wakisubiri kukamilika kwa ujenzi. Hapo ndipo nilipomkuta Sheikh Majid anasomesha kitabu cha Allah. Nilipokuwa nikiangalia ile mandhar ya msala ikanijia picha ya misikiti iliyokuwapo Dar es Salaam miaka ya 1950. Nilikaa kusikiliza darsa nikapata picha ya Masjid Badawy Sheikh Hassan bin Amir anasomesha tafsir ya Qur'an... Nilipokuwa naondoka nilangalia ujenzi na Mashaallah inaelekea In Sha Allah utatoka msikiti wa haja. Katika Msala niliona ubao pembeni ya Kibla ukionyesha michango ambayo Waislam wanachanga kila baada ya sala kwa ajili ya ujenzi wa msikiti. 

Allah awafanyie wepesi. 
Amin.

No comments: