Nilikuwa naitafuta picha ya hayati Chief Michael Lukumbuzya kwa miaka mingi bila mafanikio. Sababu ya kuitafuta picha ya Chief Lukumbuzya ni kisa alichonihadithia Bi. Mwamvua biti Masha mke wa marehemu Abdulwahid Sykes maarufu akijuikana kwa jina la mwanae wa kwanza Daisy hivyo tukimuita Mama Daisy. Nilikuwa kila nikipata fursa ya kuwa na mama
yangu Bi. Mwamvua, yaani Mama Daisy nikipenda kumdodosa mambo
yalivyokuwa wakati wa ukoloni walipokuwa wanapambana na Muingereza, kwanza
kichinichini katika miaka ya mwanzo ya 1950 wakati wa TAA kisha
wakipambana na mkoloni dhahiri baada ya kuunda TANU mwaka wa 1954. Bi. Mwamvua alikuwa wakati
mwingine bila kutegemea akiniangushia
habari muhimu kupita kiasi. Mfano siku aliponiambia kuwa nafasi ya president wa
TANU nafasi ile ilikuwa ya Chief Kidaha Makwaia lakini alikataa ndipo bahati ikamuangukia Julius Nyerere.
Iko siku akanieleza taharuki iliyotokea nyumbani kwa Abdul Sykes baada ya Nyerere kula chakuka kilichomfanya tumbo limkate na ikadhaniwa kuwa amelishwa sumu. Mkasa huu ulitokea wakati mama yake Nyerere, Bi. Mugaya yuko na Mama Maria Nyerere vilevile wamekaa uani na akina mama wengine na Abdul Sykes, Nyerere na viongozi wengine wako nyumba kubwa wanapanga mipango ya kupeleka harakati mbele. Mama yake Nyerere alianza kulia akiamini kabisa kuwa mwanae katiliwa sumu katika chakula. Mama Daisyalikuwa na habari nyingi sana za nyakati zile. Historia ya TANU kama zilivyo nyaraka na picha zake nyingi zimo mikononi mwa watu.
Mfano mwingine ni wa mkutano wa kwanza wa Wanawake wa TANU uliokuwa ukifanyika Arnautoglo Hall na yeye alikuwa yuko nyumbani anafanya shughuli zake. Anasema, ‘’Aliporudi nyumbani Bwana Abdul kanikuta nimekaa, akaniuliza wewe hukwenda mkutanoni? Wenzako wote wako Arnautoglo…’’ Bi. Mwamvua anasema hapo hapo akachukua baibui lake na kuelekea mkutanoni. Wasemaji wakuu walikuwa Bi. Titi Mohamed na Bi. Tatu biti Mzee. Huu ndiyo mkutano wa kwanza wa wanawake wa TANU.
![]() |
| Chief David Kidaha Makwaia |

| Kuhoto Mama Daisy, Bi. Titi Mohamed na Bi. Zainab Tewa |
Katika mazungumzo kama haya ndipo siku moja akanihadithia habari za Chief Luumbuzya. Anasema walitoka Dar es Salaam yeye mumewe kwenda Nansio, Ukerewe kumtembelea Hamza Mwapachu. Anasema walipanda
meli Mwanza pamoja na Chief Lukumbuzya kuelekea Nansio. Lukumbuzya alikuwa anatokea Makerere Uganda alipokuwa anasoma anarudi nyumbani likizo. Abdul Sykes na Michael
Lukumbuzya hawakuwa wanajuana. Hamza Mwapachu alikuwa amekusanya wananchi na
kikundi cha ngoma kuja kumpokea bandarini Nansio President wa TAA Abdulwahid Sykes. Lukumbuzya
alishangazwa kukuta sherehe bandarini akifanyiwa mtu ambae yeye hakuwa anamjua na akiuliza anaambiwa mgeni ni mgeni kutoka Dar es Salaam. Lukumbuzya alipigwa na butwaa kuona mapokezi ya watu wake wa Ukerewe wakiwa katika nderemo wakati yeye chief hakuna hata mtu alikuwa
anajua kuwa yumo katika meli ile ile. Baadae Hamza Mwapachu alimfahamisha yule mgeni waliokuja kumpokea pale alikuwa nani katika siasa za Tanganyika.
![]() |
| Hamza Kibwana Mwapachu |
Simulizi kama hizi zilinifikirisha sana katika
kutaka kuwajua wazalando wa wakati ule. Hamza Mwapachu alikuwa anafanya haya ya
kukusanya wananchi kumpokea kiongozi wa Waafrika chini ya pua za Waingereza
bila kujali nini kitampata licha ya kuwa yeye kupewa uhamisho kupelekwa
kisiwani Ukerewe peke yake ilikuwa ni adhabu, kwa hakika ni kifungo khasa cha
kumtia kuzuizini asiweze kuenedeleza mipango yake ya kuunda chama cha siasa.
Uhuru ulipopatikana Chief Michael Lukumbuzya alipelekwa nje ambako alikuwa balozi na mwisho akawa balozi Canada ambako huko ndiko umauti ulikomfika.
Uhuru ulipopatikana Chief Michael Lukumbuzya alipelekwa nje ambako alikuwa balozi na mwisho akawa balozi Canada ambako huko ndiko umauti ulikomfika.
| Abdulwahid Sykes |

No comments:
Post a Comment