
Ni baada ya kutaka
kuwaombea wafuasi wa CCM wasifanyiwe mgomo. Aambiwa kama angekwenda Gongo na
wenziwe wote wangeachiwa ukumbi mtupu. Abanwa kuhusu mashekhe wa UAMSHO.
Masheikh wasema anakoroga kinyesi halafu anategemea kuskia harufu mzuri. Aambiwa
pasi na Shein kuirejesha haki aliodhulum nchi haiwezi kua na amani.
Kweli CCM hawamjui Mungu
mpaka pale waone wameinamiwa. Mufti mkuu wa Zanzibar Shkh. Saleh juzi alifanya
kikao na masheikh wa Pemba ambapo kikao hicho kililenga kuwataka masheikh hao
wasaidie katika kuiweka jamii pamoja na kuwataka wasitishe zoezi la mgomo
linaloendelea kisiwani huko tangia kurejewa kwa uchaguzi wa March 20.
Wakati Sheikh Saleh na
ujumbe wake aliokwenda nao wakiwataka masheikh hao kufanya hivyo na kuwaremba
kwa kila sifa masheikh hao, Masheikh hao wamekuja juu na kusema kua
hapawezekani kua na amani na upendo pasi na haki na uadilifu kutendeka.
Mmoja wa masheikh ambao
walipata nafasi ya kuchangia alisema na kuhoji kua tunawezaje kuyafikia
mafanikio wakati hatujapita katika njia ya mafanikio? Huku akisistiza kua
uislam hauangaliwi vipande vipande na kusema kua hatuwezi kuangalia mwisho wa
tatizo tu bali pia tunatakiwa kuangaia na chanzo cha tatizo huku akimwambia
sheikh Saleh kua asitegemee kukoroga kinyesi halafu akaskia harufu mzuri.
Nae shekh mwengine
alisema kua Shein kadhulum na mikono yake inanuka damu na yeye mwenyewe anajua
na kumtaka sheikh Saleh amwambie Shein arejeshe haki ya aliowadhulum ndipo
amani na upendo utarudi visiwani humo.
Shekh Saleh pia
alinasihiwa na kuambiwa kua aya na hadithi alizowatolea masheikh hao aende
akawatolee na viongozi wa serikali kama vile Shein, Balozi Seif na Maalim Seif
huenda labda na wao kama binadam wakafaham na wakaamua kutenda haki. Huku
sheikh mmoja akihoji kwa nini mambo haya waambiwe wao wasiende kuambiwa hao
waliosababisha matatizo haya? na kusema kua wao siku zote wanajulikana kipindi
cha shida tu na matatizo lakini kukiwa hakuna vitu hivyo na nchi imetulia
hawaitwi hata kupewa asante ingawa juhudi za kuituliza nchi kiasi kikubwa huzifanya
wao.
Wako masheke pia
walimuuliza sheikh Saleh wananchi watafanyaje ikiwa mtu ambaye hana bunduki na
uwezo wowote anateswa na kupigwa na kudhalilishwa na Jeshi la Polisi na Mazombi
bila ya kosa? Je ni haram kwao wao kuchukia? Pia aliulizwa tunawezaje kua na
mapenzi ya kushirikiana na watu ambao waliwaweka mashekhe wetu ndani na
kujisifia katika majukwaa ya kisiasa huku mashekhe hao na familia zao
zikiendelea kupata tabu? Hapo hapo mmoja wa mashekhe hao akamwambia sheikh
Saleh kua kutokana na alivo anaamin kua kama angeamua kusimama usiku na
kuwaombea dua tu masheikh wale basi masheikh wale wangepata nusra ya
Mwenyezi Mungu lakini inaonekana hata hilo limemshinda.
Aliendelea sheikh huyo
kwa kusema kua watu waliomba dua nyingi ili kuinusuru Zanzibar na mambo mbali
mbali lakini kuna viongozi wakawa wanapita na kusema kua vi Alamtara vyenu
havitowasaidia chochote sasa je mtu kama huyu ambaye anadharau na kuidhalilisha
hadi Quran (maneno ya Mungu) nae tushirikiane nae?
Hakika sheikh Saleh
ambaye ni mufti mkuu wa Zanzibar juzi alipata wakati mgumu sana na hii
imetokana na kukubali kutumiwa na CCM pamoja na ukweli kwamba ukweli na chanzo
cha matatizo haya yote anajua wazi kua yamesababishwa na CCM kwa dhambi
walioifanya ya kuwadhulum Wazanzibari.
CCM kwa sasa hakuna mtu
anaeweza kuisadia au kuinusuru katika namna yoyote ile maana imekataa kufata
maamrisho ya Allah ya kutenda haki na kuacha dhulma.
Shein anaposema kua
kauli za ubaguzi na kuzigawa jamii zimekatazwa katika dini zote huku akajitia
sahau kua dhulma imekatazwa zaidi ni sawa na hayo aliyoyasema sheikh kua
anakoroga kinyesi halafu anategemea kuskia harufu mzuri au anataka kuyafikia
mafanikio lakini hafati njia za mafanikio.
Sisi tunasema tena
tutawagomea na hatutoacha kuwagomea mpaka watubu na moja ya sharti ya toba ni
kama alivyosema mmoja wa masheikh hao kua ni kuirejesha haki kwa uliowadhulum.
Na hii ndio toba pekee
ya CCM itakayotufanya tuache kuwagomea, pasi na kufanya hivyo tutawagomea mpaka
wachanganyikiwe.
# Hakuna kurudi nyuma mpaka kieleweke#
Abdalla Dadi.
No comments:
Post a Comment