Wednesday, 18 May 2016

KUTOKA JF: KUMBUKUMBU ZA ALI MUHSIN BARWANI: ''CONFLICTS AND HARMONY IN ZANZIBAR''


Utangulizi
Nimekuwa nikiulizwa maswali mengi kuhusu historia ya Tanzania khasa kuhusu historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika na Zanzibar. Kwa ajili hii nimeona niongeze kitabu hiki katika orodha ya vitabu muhimu kwa wanafunzi wa historia ya Tanzania kuvisoma.Naamini yeyote atakaesoma kitabu cha Ali Muhsin Barwani na  kitabu cha Abdul Sykes atajifunza mengi ambayo hayakuwa hadhir kwake kabla.



[​IMG]

Wanamajlis,

Naona kumekuwa na hamu mpya ya kusoma historia ya nchi yetu.

Pamoja na kitabu cha Abdul Sykes kipo kitabu kingine kimeandikwa
na Ali Muhsin Barwani aliyekuwa kiongozi wa Zanzibar Nationalist
Party (Hizbu) ''Conflicts and Harmony in Zanzibar.''

Ali Muhsin alikuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wakati mapinduzi
yalipotokea mwaka wa 1964 na alifungwa jela za Bara kwa miaka 10.

Katika kitabu hiki Ali Muhsin anaeleza siasa za Zanzibar wakati wa 
kupigania uhuru wa Zanzibar yeye akiwa kiongozi wa Hizbu.

Ali Muhsin anaeleza mchango wa Nyerere katika kuunda Afro-Shirazi
Party (ASP) na jinsi kuundwa kwa chama hiki kilivyobadili muelekeo
wa siasa visiwani kutoka ''utaifa'' kuelekea ''ukabila.''

Ali Muhsin atakushika pale anapoeleza maisha yake ya jela kwa miaka
kumi akianzia Ukonga, Isanga hadi Butimba na Bukoba hadi kuachiwa 
mwaka wa 1974 na jinsi alivyotoroka nchini kupitia mpaka wa Horohoro 
kwa msaada wa mfungwa mwenzake waliojuana jela.

Ukikianza hukiweki chini.

Kitabu hiki kinapatikana maduka ya vitabu Ibn Hazm Media Centre Msikiti
wa Mtoro na Manyema na Duka la Vitabu la Rubawa Ilala Amana, Soma 
Bookshop, Mikocheni, Elite Bookshop Mbezi Samaki kwa bei ya shs: 10,000.00.

Pia kinapatikana Tanzania Publishing House (TPH) Samora Avenue kwa
bei ya shs: 13,000.00

No comments: