Saturday, 28 May 2016

NILIYOJIFUNZA KATIKA MAZUNGUMZO YA SHEIKH QASSIM BIN ALI KHAN - KASSIM IBRAHIM

Kassim Ibrahim
Photo

Niliyojifunza leo...katika ukumbi wa hotel....ya Golden Tulip:

''Katika kongamano lililoandaliwa na ndugu zetu wa Kalamu Education Foundation (KEF) na mada ya umoja iliyowasilishwa na Shekh Qassim bin Ali Khan kutoka America...

Kongamano la leo (jana) ni muendelezo wa makongamano ya Welcome Ramadhan...ambapo leo (jana) kumefanyika makongamano...mawili pale My fair plaza...limefanyika kongamano la kina Mama...wakiwa na mke wa Sh Qassim Ali Khan..

Kongamano limefana kwa kuunganisha viongozi wa Taasisi mbalimbali...na Masheikh wakubwa…

Awali ya yote alianza kuzungumza Shekh Mohamed Issa akielezea fikra ya Umoja na umuhimu wake kwa Waislamu..

Shekh Mohamed alianza kwa kuonyesha umuhimu wa Waislamu kukutana na kupanga mambo yao kwa pamoja..kubadilishana fikra na huo ndio msingi wa Allah(s.w) kutupa sala tano kila siku...

Shekh Mohamed alichagiza kwa Aya na hadithi....zinazohimiza umoja na mshikamano akisisitiza...na kusema "Alaykum...bil Jamah" shikamaneni kwa pamoja huku akipiga mfano wa maneno ya Mtume(s.a.w) "akisema shikamaneni na umoja hakika Mbwa Mwitu ...siku zote huwa anakula kondoo aliyejitenga...

Shekh Mohamed Alizidi kushajihisha ya kwamba kitabu cha Allah ndio Nuru inayoangaza kila kitu...

Alisema kupitia kongamano hilo...ni wasaa mzuri kwa Waislamu..kujadili fikra ya ugaidi..na visababishi vyake...pili kujadili upande wa uchumi...ni vipi tutajikwamua kutoka katika lindi la umaskini...alimaliza kwa kuonyesha uwepo wa Taasisi nyingi ni jambo jema...ila litaleta tija kama kutakuwa na ushirikiano mzuri kwa taasisi moja na nyingine...

Mada iliyowasilishwa na Imam Qassim Ali khan..ilitikisa nyoyo za Waislamu na watu kutokwa na machozi..

Shekh Qassim...alisilimu mwaka 1971...kabla ya kusilimu alikuwa mchungaji.....amefanya kazi kubwa za kujitolea kuihudumia jamii...kujenga misikiti na kuwa mshauri kwa wafungwa magerezani huko Amerika....

Shekh Qassim...amefanikiwa kusilimisha watu 3000 huko U.S.A pamoja na kuwasilimisha ndugu zake....

Shekh Qassim ni Imam wa Masjid Huston huko Texas...ktk kuchagiza Mada yake aliwakumbusha wajumbe ya kwamba fanya kazi kwa bidiii ili uweze kuwaunganisha Waislamu....

Alisema kila Muislamu ana "potential"uwezo wa kufanya mambo ambayo sisi hatuyaoni....alisema jambo la umoja ni jambo la asili hata viungo vyote vinaonyesha hivyo...

Alionyesha Umma unapita ktk wakati mgumu sana hivi sasa kuna vita 100 zinaendelea duniani...

Shekh alipiga mfano akisema hata mawingu angani huonyesha Umoja....alitoa kisa kimoja kilichomtokea yeye binafsi aliposafiri kwenye ndege ghafla ndege ile ikapatwa na mtikisiko wa ajabu....akamuuliza jirani yake akajibu....ni "Air pocket" mfuko wa ndege unapopita kwenye mawingu ndio mtikisiko huo unatokea....Shekh akacheka huku anasema mtikisiko ule unatokana.....tone la maji "microscopic" linapodondoka kwenda chini haliathiri chochote kwenye ndege yenye uzito wa matani....ila matone hayo yakiungana ndio hutikisa ndege....

Shekh Qassim aliwafananisha Waislamu ni sawa na computer hard disk...ambayo inatakiwa kufanyiwa "defragmentation" ili kuondoa tofauti baina yetu.....na kuungana kwa pamoja...
🙏
Shekh alisema....hivi mnafikiri Allah atakuacheni hivi hivi bila kukujaribuni huku akinukuu ayah ktk surat Ankabut...

🙏hatuna hakika kama mnapenda Allah...Quran...Mtume bila ya kuwatahini...alisema kujaribiwa kiukweli ni pindi linapohitajika jambo utoe mchango wako...wa nafsi na mali kwa msafiri aliyeharibikiwa...au mtu mwenye njaa hapo ndio utakuwa umetahiniwa kwelikweli...

Shekh alihitimisha Muhadhara kwa nukta muhimu huku akitokwa na Machozi
..akisema Allah katika Suratil fil aliilinda Alkaba......sehemu ambayo ilikuwa na masanamu 360....watu wakiizunguka wakiwa uchi na kufanya zinaa lakini Allah aliilinda na kuhifadhi.....

Basi kila mmoja katika sisi anamapungufu yake na ana mazuri yake....tusichunguze mapungufu ya mtu binafsi....Alllah ana mpango wa kututakasa Allah ana mpango wa kutusamehe...


Jicho la mwanadamu sehemu ya ndani huitwa pupil..na mwanafunzi anapokuwa ngazi ya primary huitwa pupils...watoto wanaoitwa pupils huona kwa msaada wa mwalimu pindi nuru inapozidi....hivyo basi kadri elimu inavyozidi mtu huwa mpole na mlaini...Jamii yoyote ile haiwezi kupata manufaa....kama haitojali mtu mmoja atapata nini...?''

Itaendelea In Shaallah...

Kassim Ibrahim ni mwanafunzi katika moja ya taasisi ya elimu ya juu na ni mmoja wa viongozi wa vijana toka alipokuwa sekondari.

No comments: