Tuesday, 24 May 2016

WORLD ISLAMIC HELP ILIPOTEMBELEA OFISI ZA KEF

SHEIKH SULTAN NIAZ UL HASSAN QADRI AND IMAM IJAZ AHMAD SHAMI KUTOKA UINGEREZA WATEMBELEA OFISI ZA KEF

As salaam Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh.

Leo ilikuwa siku nyingine njema kwa Taasisi yetu ya Kalamu Education Foundation kwa kutembelewa na Ugeni mkubwa wa Mkuu wa Taasisi ya Islamic Help Duniani Sheikh Sultan Niaz Ul Hassan Qadr akiongozana na Imam Ijaz Ahmad Shami mwanazuoni maarufu kijana kule Uingereza.

Alhamdulillah tumeona mwanga mkubwa wa kujenga ushirikiano kama taasisi zitoazo huduma kwa jamii yetu ya Kiislam na wefurahi sana juu ya mafunzo ya walimu wa madrassa na mpango wa ujenzi wa vituo 50 vya ‘’Integrated Academy,’’ hasa vijijini ambapo Imam Ijaz ameona wenzetu wanapiga hatua kubwa sana huku waliopo huko wengi ni Waislam. Alisisitiza umuhimu wa kuuhami Uislam usije ondoka nasi tuna mali na elimu.

Twamuomba Allah adumishe Udugu huu katika kusaidia umma wetu hasa vijijini.
Amiin ya Rabb.

Photo


Photo

Photo

Makala na picha kwa hisani ya KEF

No comments: