Muhammad Ali 1942 – 2016

Muhammad Ali alipata kusema
baada yangu mimi kutakuwa hakuna tena ngumi. Hivi ndivyo ilivyo. Si watu wengi
baada ya Ali kuondoka ulingoni waliendelea kufuatilia tena ngumi. Ali alichukua
ubingwa kwa kumpiga Sony Liston mwaka wa 1964 wakati ule aikijulikana kama
Cassius Clay. Miaka ya 1960 imepewa jina la ‘’The Roaring 60s’’ kwa sababu
ilikuwa miaka ya mengi sana. Huu ulikuwa wakati ambao sisi ambao sasa ni watu
wazima au ukipenda ni wazee tulikuwa vijana katika miaka ya ‘’teens’’ – ‘’teenegers.’’
Ilikuwa ndiyo miaka ya Muhammad Ali na Sony Liston, ilikuwa miaka ya Sam Cooke,
Beatles na Rolling Stones, ilikuwa miaka ya Eric Bardon na Animals…ilikuwa
miaka ya Martin Luther King. Elvis Presley na Cliff Richard. Ilikuwa miaka ya
Woodstock. Miaka ya Jimi Hendrinx na Janis Joplin. Hapa kwetu East Africa tulikuwa na nyota yetu - Sal Davis na ''Makini'' nyimbo yake iliyovuma aliyoitoa mwaka wa 1963. Dar es Salaam tulikuwa na Chipukizi Club na Hussein Shebe. Henin Seif na Raymond Chihota wakitumbuza na band ya vijana wa Kigoa ikiitwa The Blue Diamonds.
Ilikuwa miaka ya wazimu kwa
hakika ilikuwa miaka ya wazimu khasa. Vita vya Vietnam vilikuwa vinaendelea
kila ukifungua radio habari ni za Saigon na Hanoi. Huu ndiyo wakati yalipotokea
mauaji ya kutisha ya Mai Lai huko Vietnam. Juu ya vurugu hizi zote aliyekuwa
aking’ara na ‘’icon,’’ ya wengi alikuwa Muhammad Ali Bingwa wa Dunia wa
Masumbwi wa Uzito wa Juu. Hodari wa kuzungumza wakati mwingine kwa mashairi: ‘’Harry
Cooper has been talking too much, he will go down in five.’’ ‘’Fly like a
butterfly and sting like a bee. Rumble young man rumble.’’
Ali akiburudisha
ndani na nje ya ulingo. Ni tabu kwa mtu kujaribu kumweleza Muhammad Ali kwani
kaandikwa sana tena na waandishiwa kutajika. Nataka kumalizia kwa kusema kuwa moja ya vitabu vyangu katika
orodha ya vitabu ninavyovipenda na hurudia kuvisoma tena na tena na tena kila nipatapo
nafasi ni kitabu alichoandika mwenyewe Ali kuhusu maisha yake: ‘’The Greatest
My Own Story.’’
Miaka miwili iliyopita niliandika maneno haya katika JF:
Miaka miwili iliyopita niliandika maneno haya katika JF:


No comments:
Post a Comment