BAKWATA
Sehemu ya Kwanza
Mgogoro wa East African
Muslim Welfare Society (EAMWS) wa Mwaka wa 1968
Kutokana
na katiba ya mwaka wa 1957 lengo kuu la EAMWS ilikuwa ni kuutangaza Uislam
katika Afrika ya Masharikií. EAMWS yenyewe ilikuwa ikijigamba kuwa uti wake wa
mgongo ilikuwa ni tabligh, yaani utangazaji wa dini. Jumuiya hii iliyoanzishwa mwaka 1933 ilikuwa
ya Waislam wa mataifa yote katika uanachama na katika uongozi wake. Katika uhai
wake wa miaka thelathini na tano EAMWS ilijiweka mbali sana na siasa. Jumuiya
hii ilishughulikia kuutetea na kuueneza Uislam katika Afrika ya Mashariki.
Lakini baada ya kutokea maasi ya Tanganyika Rifles mwaka 1964 yaliyopelekea
viongozi wengi wa Kiislam kuwekwa kizuizini, EAMWS ikawa imepoteza mwelekeo
wake na kudhoofika. Baadhi ya matawi yaliyokuwa katika majimbo yakafungwa kwa
woga na kukosa viongozi thabiti na kwa matawi mengine yalifungwa kwa sababu
viongozi wake walkuwa wakichimbwa chinichini na serikali. Waislam wengi
walihisi vitisho vya serikali kwa hiyo waliogopa kuchukua uongozi wa EAMWS.
Wengi waliogopa kuitumikia EAMWS kwa kuwa walihisi ofisi za jumuiya hiyo
zilikuwa zikichukuliwa na serikali kama vituo vya upinzani dhidi yake. Kwa
zaidi ya miaka mitatu toka ule mkutano wa mwaka 1963, EAMWS haikuweza kufanya
mkutano wowote.
EAMWS
ilipokuja kuitisha mkutano wake wa mwaka mjini Arusha mwaka 1966 kikajitokeza
kikundi kutoka upande wa Tanzania kikidai EAMWS ijigawe, kila nchi iwe na
mamlaka yake na ijitegemee yenyewe, yaani Tanzania, Kenya na Uganda zote ziwe
mbalimbali. Kikundi hiki kilichokuwa kikidai utengano vilevile kikadai kuwa
katiba ya EAMWS nayo iwe ya ëkizalendoí Hii ilikuwa na maana kuwa uongozi
itabidi iifanyie katiba marekebisho ili kuiwezesha Tanzania kuwa huru ndani ya
EAMWS. Wajumbe waliokuwa wanaona mbali kutoka Tanzania na wengine kutoka Kenya
na Uganda, na kwa hakiaka mkutano mzima kwa ujumla walipinga kitendo hicho,
wakidai kuwa kwa kufanya hivyo Waislam wa Tanzania watakuwa wametengwa na umma
wa Kiislam wa Afrika ya Mashariki. Jambo hili likitokea, si tu litakuwa
limewadhoofisha Waislam wa Tanzania peke yao, bali Waislam wa Afrika ya
Mashariki nzima. Wajumbe wa Kenya na Uganda walikuwa wanatambua kuwa kulikuwa na
shinikizo kubwa kutoka serikali ya Tanzania kwa Watanzania kujitoa kutoka
EAMWS. Halikadhalika ilikuwa inafahamika kuwa wajumbe wa Tanzania walikuwa
wakifanya kazi chini ya shinikizo kali kutoka serikali ya Nyerere.
Haikuwa
siri sana kuwa baadhi ya viongozi wa EAMWS walikuwa kisirisiri wakiandamwa na
serikali. Lakini mkutano ule haukuzungumzia matatizo haya kwa kuwa hayo
yalichukuwaliwa kama matatizo ya ndani ya nchi. Hata hivyo kwa ule moyo wa
Kiislam wa kuhurumiana, wajumbe wa Kenya na Uganda kwa faragha walionyesha
masikitiko yao kwa Tewa kuhusu ile hali iliyokuwa ikiwakabili Waislam wa
Tanzania. Wajumbe walipokuwa wakiondoka kurejea makwao, ilikuwa wazi kuwa
serikali ya Tanzania ilikuwa ikiingilia kati EAMWS kiasi cha kuifanya jumuiya
hiyo ishindwe kufanya kazi yake vyema na kupitisha maamuzi yake. Hali hii
ilijidhihirisha wazi pale kwa kipindi kizima cha mkutano, makachero wa serikali
walikuwa wamejitokeza kwa wingi mjini Arusha.
Haukupita
muda ikadhihirika kuwa serikali ilikuwa imepania kuivunja EAMWS kwa kuwatumia
Waislam wachache walioteuliwa kwa kazi hiyo. Lengo likiwa ni kuanzisha taasisi
mpya ambayo serikali itaweza kuiamuru. Ieleweke hapa kuwa kama tulivyokwisha
eleza hapo nyuma, serikali nzima ya Tanzani ilikuwa mikononi mwa Wakristo na
watendaji hawa walikuwa wapo chini ya Kanisa. Hii ilikuwa na maana kuwa
kilichotakiwa kuwepo ilikuwa taasisi ya Kiislam ambayo Kanisa itaweza kuiamuru.
Hii ilikuwa ni jambo lazima lifanyike ili kuwadhibiti Waislam kama nguvu
inayoweza kuleta mabadiliko ya siasa. Baada ya kuelewa hali hii ndipo sasa
tunaweza kuuangalia kile kilichoitwa mgogoro wa EAMWS ambao ulidumu kwa miezi
mitatu ya mwisho ya mwaka wa 1968.
Ilituweze
kuuelewa vyema kisa kizima cha ëmgogoroí ni muhimu kwanza kuelewa chanzo chake,
hadhi za wahusika wakuu na nafasi zao katika ëmgogoroí ule. Mwisho, ni muhimu
kuweka bayana na kuchambua nafasi ya Julius Nyerere, serikali yake, chama cha
TANU na vyombo vya dola katika ëmgogoroí ule. Hii itasaidia kuelewa kama kweli
ulikuwepo ëmgogoroí katika EAMWS, au ëmgogoroí ulibambikizwa na watu katika
TANU, serikali na ndani ya Waislam wenyewe ili kuwadhoofisha Waislam kwa nia ya
kuwa usije Uislam ukawa na nguvu katika Tanzania hivyo kuwawezesha Waislam
kushika madaraka ya nchi.
Mwaka
wa 1967 Mwalimu Julius Nyerere alitangaza Azimio la Arusha hatua ambayo iliitia
Tanzania katika siasa ya ujamaa. Sera hii mpya ya uchumi ilipokelewa vyema na
wananchi. Mtu ambae hata alikuwa hajulikani, tena mwalimu wa shule ya msingi
akijulikana kwa jina la Adam Nasibu ambae alikuwa katibu wa Bukoba wa EAMWS,
alichukua nafasi hii kwa kuongoza maandamano hadi ofisi ya TANU ya Mkoa
kumuunga mkono Mwalimu Nyerere na sera yake mpya ya uchumi ya Azimio la Arusha.
Adam Nasibu inasemekana kuwa alisema ujamaa ni sawa na mafundisho ya Qurían
Tukufu. Adam Nasibu hakuishia hapo alikwenda mbele zaidi na kutoa ëmiongozo kwa
viongozi wote wa Kiislam wa Bukoba akifafanua Azimio la Arushaí. Wasiokuwa Waislam walimuona Adam Nasibu kama
Muislam mwenye mwamko mzuri wa kimaendeleo, na kwa kuwa yeye alikuwa ni
kiongozi wa EAMWS, kuunga kwake mkono Azimio la Arusha kulionekana kama kitendo
rasmi cha jumuiya hiyo kuunga mkono sera hiyo. Lakini kabla ya yeye kufanya
haya, hakuna mtu aliyemjua mwalimu huyu wa shule kama mwanasiasa licha ya kuwa
msomi mwenye uwezo wa kuchambua mambo.
No comments:
Post a Comment