Kisa cha Aga Khan na Viongozi wa BAKWATA
| Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi na Viongozi wa Juu wa Aga Khan |
| Sheikh Ali Hassan Mwinyi akiwa na viongozi wa Aga Khan na Viongozi wa BAKWATA Issa Shaaban Simba Mufti wa BAKWATA na Alhad Mussa Sheikh a BAKWATA wa Mkoa wa Dar es Salaam |
![]() |
| Kulia: Ali Mwinyi Tambwe Katibu wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika, Oscar Kambona, Ali Jumbe Kiro mmoja wa waasisi wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na huyu mwanamke pekee ni Mwalimu Sakina bint Arab. Picha imepikwa Government House miaka ya mwanzoni ya uhuru |
| Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi Akiwa na Uongozi wa Juu wa Aga Khan Hata watu wazima hupigiana hadithi...
Leo nimeona picha nyingi za Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi katika Michuzi Blog zikimuonyesha rais mstaafu akiwa na viongozi wa Aga Khan katika maonyesho ya jumuia hiyo.
Aga Khan si mgeni Tanzania na waliomuingiza nchini ni Waislam katika miaka ya 1930 kwa ajili ya kutoa misaada kwa Waislam. Katika miaka ya 1930 baba yake huyu Aga Khan wa sasa Shah Karim Al Hussein, Sir Sultan Mohamed Shah alitembelea Tanganyika na katika mradi mmoja wapo aliofika kuuangalia ulikuwa ujenzi wa shule ya Al Jamiatul Islamiyya School, Mtaa wa Agrrey na New Street uliokuwa ukijengwa na Waislam chini ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika jumuia ya Waislam iliyoanzishwa mwaka 1933 viongozi wake wakiwa Kleist Sykes, Ali Jumbe Kiro, Mzee bin Sudi na wazee wengine wa mjini. Katika hafla ile mwanafunzi aliyesoma risala mbele ya Aga Khan alikuwa mtoto wa Kleist, Abdulwahid. (Miaka mingi baadae Abdulwahid Sykes sasa kijana na mwanasiasa akajachaguliwa kuwa mjumbe katika Bodi ya Elimu ya Aga Khan).
Jengo la Al Jamiatul Islamiyya Muslim School
Sasa tuingie kwenye hadithi yenyewe. Miaka mingi ikapita na mwishowe Nyerere akatoka madarakani na serikali ikashikwa na Ali Hassan Mwinyi. Kwa takriban miaka 20 Aga Khan hakupata kutia mguu Tanzania. Katika utawala wa Mwinyi Aga Khan akaja Tanzania. Katika mazungumzo na Rais Mwinyi, Mwinyi akaomba msaada wa Aga Khan katika nyanja tatu - Elimu, Kilimo na Afya. Aga Khan akamueleza Rais Mwinyi kuwa Aga Khan walikuwapo Tanzania miaka ya nyuma wakisaidia katika elimu. Hili suala la elimu likamgusa sana Aga Khan kiasi cha yeye alipomaliza mazungumzo na Mwinyi akamwamrisha Katibu wa Elimu wa Aga Khan Tanzania, Riyaz Gulamani awakaribishe viongozi wa Waislam wa iliyokuwa EAMWS pamoja na viongozi wa BAKWATA katika chakula cha jioni ili wajadili maendeleo ya Waislam. Katika viongozi wa EAMWS walioalikwa katika hafla ile alikuwa Tewa Said Tewa. BAKWATA walioalikwa walikuwa Sheikh Mkuu wa BAKWATA Hemed bin Jumaa, Adam Nasibu aliyekuwa katibu wa BAKWATA, Mustafa Songambele mzee wa CCM na mwanakamati katika BAKWATA na Waislam wengineo. Baada ya chakula Aga Khan akawaeleza nia yake ya kuwaita na akawataka watoe wanachotaka wafanyiwe na Aga Khan katika elimu.
Mustafa Songambele
Hapa ndipo ''drama,'' ilipoanza. Akasimama kiongozi mmoja wa BAKWATA na mzee wa CCM akamwambia Aga Khan, ''Serikali ya Tanzania inawatosheleza Waislam katika elimu na hawahitaji msaada kutoka kokote.'' Naomba nisimame hapa. Mkasa huu kwa mara ya kwanza alinihadithia Riyaz Gulamani. Sikuamini kama inaweza kuwa kweli. Kisa hiki nikaja kuhadithiwa tena na Tewa Said Tewa kama vile alivyonihadithia Riyaz Gulamani. Hapo ndipo nikaamini kuwa kisa kile hakika kilitokea na Mzee Tewa akanipa na jina la huyo aliyesema maneno yale.
Tuendelee.
Aga Khan kwa upole kabisa akajibu kuwa jana yake alikuwa na Rais na yeye kaomba msaada wa elimu. Hapo sasa ndipo likazuka zogo baina ya viongozi wa BAKWATA na Waislam wengine mbele ya mgeni Aga Khan. Kufipisha mkasa. Kabla hajaondoka kufuatia yale aliyosikia na aliyoshuhudia, Aga Khan akamwambia Riyaz, ''Inaelekea hawa ndugu zetu bado hawajawa tayari lakini ushauri wangu ni kuwa uache mlango wetu wazi. Siku yoyote wakakapokuwa tayari basi tutatoa msaada.'' Mwisho wa hadithi yangu. |
''Juma lile lile Aga Khan ambae ndiye aliyekuwa akishambuliwa na kundi la Adam Nasibu, baada ya kutambua kuwa EAMWS isingeweza kamwe kuokolewa, akiwa Paris, Ufaransa alijiuzulu nafasi yake kama patron wa EAMWS.''
''Kuangushwa kwa EAMWS kulisababishwa na watu watatu ambao wao ndiyo walikuwa mstari wa mbele kabisa - Adam Nasibu, Sheikh Kassim Juma na Sheikh Abdallah Chaurembo aliyepata kuwa mwanafunzi hodari wa Sheikh Hassan bin Amir; na njama hii ikaungwa mkono na Rashid Kawawa na Abeid Amani Karume. Mkono wa Julius Nyerere na Kanisa Katoliki katika njama hii haukuonekana kabisa kama ilivyo kawaida katika njama zote za kupiga vita Uislam na Waislam Tanzania.''
1980s
Ungelitegemea viongozi wa BAKWATA wawe wamejifunza baada ya miaka hiyo yote ya udhalili wa Waislam lakini haikuwa hivyo.
Kwa apendae kupata habari zaidi aingie hapa http://www.mohammedsaid.com/2013/12/regional-conference-of-islam-in-eastern.html asome kisa cha Sheikh Kassim bin Juma na Julius Nyerere katika miaka ya mwanzo ya uhuru ashuhudie urafiki uliomalizikia katika uadui na uhasama wa hali ya juu kabisa.Vilevile msomaji atajionea jinsi Ali Hassan Mwinyi alivyojikuta ametumbukia katika mvutano na Kanisa ambao hakuutegemea kabisa.
Kwa apendae kupata habari zaidi aingie hapa http://www.mohammedsaid.com/2013/12/regional-conference-of-islam-in-eastern.html asome kisa cha Sheikh Kassim bin Juma na Julius Nyerere katika miaka ya mwanzo ya uhuru ashuhudie urafiki uliomalizikia katika uadui na uhasama wa hali ya juu kabisa.Vilevile msomaji atajionea jinsi Ali Hassan Mwinyi alivyojikuta ametumbukia katika mvutano na Kanisa ambao hakuutegemea kabisa.


No comments:
Post a Comment