Saturday, 8 February 2014

Maulid ya Al Madrasatul Fauz Wassalaam

Allah Litie Mwanga Kaburi la Sheikh Letu Shaaban Harir kwa Kutufunzia Vijana Wanaopeleka Mbele Dini Yako

Maonyesho ya Watoto
Jumamosi  8 Mfungo Saba 1435






Asil ya Madrasatul Fauz Wassalaam ni wanafunzi wa marehemu Sheikh Shaaban Harir aliyekuwa muasisi wa Maawal Islamiyya moja ya taasisi kubwa za Tanga. Baadhi ya wanafunzi wake kuhitimu wakaja Dar es Salaam kusomesha kitabu cha Allah. Hivi sasa madras hii ni moja ya madras kubwa Magomeni Mapipa na ina wanafuzi takriban 200 wa kiume na wa kike. Kila mwaka vijana hawa hufanya Maulid ya kumuadhimisha Mtume SAW. Siku ya kwanza asubuhi wanafunzi hufanya maonyesho kuwaonyesha wazazi kile walichojifunza katika mwaka mzima. Hii inakuwa siku nzima. Usiku huwa samai na sikiu ya pili baada ya L'Asr hufanyika zafa na usiku ndipo husomwa Maulid. Maonyesho na Maulid huvitia sana na kupendezesha mandhar yote ya Magomeni Mapipa. Siku mbili mfululizo ni Qur'an ikisomwa, Qasida na wanafunzi wakieleza mada tofauti walizosomeshwa na waalimu wao.



Sheikh Mohamed Said Harir na baadhi ya wanafunzi wake










SAMAI
8 Mfungo Saba 1435






Kushoto kwenda kulia: Sheikh Alhad Omar, Sheikh Burhan Bakar na Sheikh Ahmed Kizigo

ZAFFA 
9 Mfungo Saba 1435

Displaying 20140209_181847.jpg













MAULID
9 Mfungo Saba 1435



Displaying 20140209_233408.jpg











No comments: