Inatengenezwa...
Fuatilia...
Kama ada Wakristo lazima wawazidi Waislam katika kila jambo...
Uwiano wa kijinsia uwepo nk. nk. ila hilo tu la Waislam kuwa sawa na Wakristo...
Maneno hayo hapo chini yanatoka katika kitabu changu, ''Maisha
na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Kisa
Kilichofichwa Kisifahamike Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa
Waingereza Katika Tanganyika.''
''Bahati mbaya mgao wa madaraka katika siasa Tanzania
umewatupa nje Waislam, ingawa inafahamika kuwa usalama na utulivu wa nchi
yeyote unategemea mizani hii kuwa sawa. Vyanzo tofauti vya takwimu vinatoa
takwimu tofauti zinazopingana kuhusu hesabu ya Waislam na Wakristo katika
Tanzania. Hii inatokana na ukweli kuwa somo hili ni nyeti. Katika nchi za
Kiafrika ambazo zina wafuasi wengi wa dini hizi mbili, kwa mfano Tanzania na
Nigeria,[1]
uchunguzi wa kuwa ni dini gani ina wafuasi wengi kupita mwenzake ni chanzo cha
mgongano na mzozo. Tatizo hili lipo Tanzania. D.B. Barret [1]
anasema kuwa Waislam Tanzania ni wachache wakilinganishwa na Wakristo. Takwimu
zake zinaeleza kuwa Waislam ni 26%, Wakristo 45% na Wapagani ni 28%. Takwimu za
Tanzania National Demographic Survey za mwaka wa 1973 zinaonyesha kuwa Waislam
ni wengi kidogo kupita Wakristo wakiwa 40%, Wakristo 38.9% na Wapagani 21.1%.
Lakini takwimu za Africa South of the Sahara,[1] zinaonyesha Waislam
ni wengi Tanzania kwa 60%. Takwimu hizi zimebaki hivyo bila ya mabadiliko toka
mwaka 1982.''
Hii ndiyo hali ya uwiano wa dini kuu mbili Tanzania, Uislam na Ukristo.
Waislam wamekuwa wakilalamika kwa miaka mingi sana kuwa kuna njama za kuukandamiza Uislam na Waislam Tanzania. Hili limekuwa suala nyeti ambalo serikali inaliogopa hata kulisemea. Sana sana wakizungumza kuhusu tatizo hili ni ka serikali kuonya ''wakorofi wachache'' wanaotaka kuvuruga amani na mshikamano. Sikiliza makongamano ya kuzungumzia amani. Tatizo la kuwa Ukristo umejijenga ndani ya serikali na kutumika kupendelea Wakristo haliguswi. Inakuwaje hivi ilhali hiyo mikutano inahudhuriwa na Waislam? Dhulma hii wao hawaioni? Vipi kila nyanja uwiano uzingatiwe ila hili la dini kuu mbili hizi? Lipo tatizo lingine. Ukiitaja serikali ni sawa na kulitaja Kanisa kwa sababu serikali nzima inahodhiwa na Wakristo. Hebu soma hapo chini uone vipi Kanisa lilivyojichimbia katika serikali na vyombo vyake vyote na hii ni pamoja na Bunge. Padri Sivalon katika kitabu chake, ''Kanisa Katoliki...'' anasema Kanisa Katoliki kupitia wafuasi wake wamehodhi takriban 75% ya viti vyote vya Bunge na hiyo 30% iliyobaki wanagawana Wakristo wa madhehebu nyingine na Waislam na mgao wa Waislam si zaidi ya 6%. Katika hali kama hii Bunge la Katiba limeshindilia msumari wa moto katika kidonda cha Waislam kwa kuchagua Wakristo wengi katika kila kundi katika Bunge la Katiba. Uwiano huo wa makundi yote kundi la dini halikupewa umuhimu. Hauku
makundi mbalimbali uwiano wa makundi yote 201
Uwiano wa kijinsia wanaume 101 wanawake 100
Wanawake NGO Wajumbe 13
Wakristo 12 Muislam 1
Vyama Vya Siasa Wajumbe 28
Wakristo 18 Waislam 10
Tasisi za Elimu Wajumbe 13
Wakristo 12 Waislam 1
Walemavu Wajumbe 13
Wakrsito 10 Waislam 3
Vyama Vya Wafanyakazi Wajumbe 15
Wakisto 9 Waislam 5
Wafugaji Wajumbe 17
Wakristo 16 Waislam 1
Wavuvi Wajumbe 17
Wakristo 15 Waislam 2
Wakulima Wajumbe 13
Wakristo 8 Waislam 5
Malengo Yanayofanana Wajumbe 14
Wakristo 9 Waislam 5
Tasisi za Dini Wajumbe 13
Wakristo 8 Waislam 5
Kwa nini uwiano wa dini haukuzingatiwa?
Jamani hata katika zile kazi zetu sisi za uvuvi na ukulima tunazidiwa na Wakristo?
Hata walemavu basi Wakristo waongoze wao wawe wengi?
Hili ni lazima lijadiliwe na Wabunge wa Katiba Waislam kabla ya kikao kuanza rasmi na lirekebishwe vinginevyo mtakuwa mmemsaidia dhalim aendelee kudhulumu.
Na wala Waislam wasijidanganye kuwa dini si muhimu katika siasa za Tanzania.
makundi mbalimbali uwiano wa makundi yote 201
Bunge la Katiba
Uwiano wa kijinsia wanaume 101 wanawake 100
Wanawake NGO Wajumbe 13
Wakristo 12 Muislam 1
Vyama Vya Siasa Wajumbe 28
Wakristo 18 Waislam 10
Tasisi za Elimu Wajumbe 13
Wakristo 12 Waislam 1
Walemavu Wajumbe 13
Wakrsito 10 Waislam 3
Vyama Vya Wafanyakazi Wajumbe 15
Wakisto 9 Waislam 5
Wafugaji Wajumbe 17
Wakristo 16 Waislam 1
Wavuvi Wajumbe 17
Wakristo 15 Waislam 2
Wakulima Wajumbe 13
Wakristo 8 Waislam 5
Malengo Yanayofanana Wajumbe 14
Wakristo 9 Waislam 5
Tasisi za Dini Wajumbe 13
Wakristo 8 Waislam 5
Kwa nini uwiano wa dini haukuzingatiwa?
Jamani hata katika zile kazi zetu sisi za uvuvi na ukulima tunazidiwa na Wakristo?
Hata walemavu basi Wakristo waongoze wao wawe wengi?
Hili ni lazima lijadiliwe na Wabunge wa Katiba Waislam kabla ya kikao kuanza rasmi na lirekebishwe vinginevyo mtakuwa mmemsaidia dhalim aendelee kudhulumu.
Na wala Waislam wasijidanganye kuwa dini si muhimu katika siasa za Tanzania.
2 comments:
Hao wanaopenda kuwakandamiza Waislamu Tanzania wanasahau kwamba jahazi ikizama watazama watu wote. Waislamu na Wakristo pia. Mvua ikinyesha inarovya kila mtu. Bora haki ifanywe mapema kabla jahazi ya Tanzania haijazama.
Uislamu ni mfumo kamili wa Maisha ni mfumo usio hitajia mchanyiko na mifumo mengine kukamilika kwake ni mfumo usiohitaji kukopa fikra, dhana, wala kanuni ili kutimia ni mfumo halisi usio hitaji nadharia. Tumeuacha mfumo huu tutasaga sagwa na kukandamizwa na madhalimu mpaka turudi tuukumbatie mfumo wetu kwa mikono miwili, kwa nafsi zetu, damu zetu na kila kitu cha maisha yetu.
Post a Comment