Sheikh Ibrahim,
Salim Msoma hajaelezea
mambo yalivyokuwa kisawasawa.
Kundi la vijana waliopata mafunzo Misri
haikuwa makusudio ya Misri wala ya viongozi wa Hizbu kumuondoa mfalme.
Makusudio yalikuwa ni kujitayarisha kupambana
na Mkoloni kwa mabavu ikiwa njia za salama hazileti faida.
Katika waliopata mafunzo ya kijeshi Misri na amewataja Msoma, majina yao ni haya:
Salim Ali Ahmed Riyami
Nasor Isa Barwani
Ahmed Suleiman Riyami
Nasor Mohamed Miskiri
Hawa wote hawajapata
kuwa na fikra za kumpindua mfalme hata siku moja.
Bali walikuwa dhidi ya
makomred mpaka mwisho.
Kwa hakika Ahmed Suleiman kauliwa siku ya
mavamizi na aliyemuuwa ni Amor Dugheshi.
Ameuliwa
pamoja na Muhsin na Suleiman Badar.
Waliobakia wakitafutwa
na makomred siku ya mapinduzi lakini kwa bahati yao hawakupatikana
mpaka wakafika Raha Leo na Mola akawanusuru roho zao.
Ama nia ya Babu kuwapeleka vijana Cuba siijui.
Sitaki kuelezea chochote kuhusu hili kwani kwa upande wangu itakuwa ni dhana tu.
Washukran,
No comments:
Post a Comment