Re: Sheikh ilunga hassan kapungu 1957 -2014
Chizi Maarifa,kama asilimia ni akina bokoharan mtakuwaje shortlisted?unadhan wanaangalia uwiano au elimu dunia?we kalia madrasa halaf ubak miaka yote unalalamika na mfumo kristo.wenzenu wanasonga mbele .nenda mikoa yenye christians weng uone wanavyoshindana kujenga shule. mbeya,kinjaro,bukoba,arusha,ir inga n.k halaf nenda tbr,tanga,kigoma,mtwara,pwan wanavyoshindana kuoa na kuzaa..ushirikina na hal duni.nenda zanzibar....
Haikuwa nia yangu kukujibu kuhusu suala la Waislam kujenga shule.
Inawezekana kabisa hujui historia ya Waislam na juhudi zao katika elimu na ndiyo maana ukaja na hoja hiyo.
Inaelekea wewe ni mgeni hapa jamvini.
Mimi nimetoa ushahidi jinsi watendaji Wakristo wanavyohujumu juhudi za Waislam katika elimu.
Nitakuwekea baadhi ya mifano ambayo tayari nilishaizungumza hapa kwa kirefu:
- Nyerere kuipiga marufuku East African Muslim Welfare Society (EAMWS)1968 ili isijenge Chuo Kikuu
- Serikali kukataa Chuo Kikuu Cha Kiislam kilichotaka kujengwa na OIC kisijengwe Tanzania
- Serikali kupiga vita Darul Imaan isijenge shule Kibaha
- Serikali kuondoa uongozi wa vijana wa WARSHA waliokuwa wanataka kuziborehs shule zilizokuwa chini ya BAKWATA shule ambazo zilijengwa na EAMWS kabla ya kupigwa marufuku
- Hujuma kwa vijana wa Kiislam ndani ya Wizara ya Elimu iliyogunduliwa na WARSHA 1981 na kuthibitishwa na marehemu Prof. Malima 1987
- Hujuma kwa shule za Kiislam katika NECTA
Hii ni baadhi ya mifano na Waislam wameiomba serikali wakae chini wajadili lakini serikali inaogopa kufanya hivyo juu ya kupatiwa ushahidi wa haya niliyosema.
Hayo mengine unayosema ya kuoa kwani kuna ubaya katika kuoa na kupata kizazi?
Ama hilo la ushirikina Uislam unakataza shirki na ni katika dhambi kubwa sana.
Kuhusu hali duni hilo ni suala linalotaka uzi wake maalum tujadili.
No comments:
Post a Comment