Showing posts with label gallery. Show all posts
Showing posts with label gallery. Show all posts

Thursday 1 March 2018


Mwandishi katika video hii anaanza kuzungumza katika dakika ya 40:40

Hii ni simulizi ya mkasa wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ilipodhaniwa kalishwa chakula kilichotiwa sumu kwa nia ya kutaka kukatisha maisha yake nyumbani kwa Abdulwahid Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu katika miaka ya kati 1950 baada ya Mwalimu kutoka UNO safari ya kwanza 1955
Bi. Mruguru bint Mussa
Mama yake Abdulwahid Sykes

Bi. Nyang'ombe Mugaya
Mama yake Baba wa Taifa
Kushoto Bi. Mwamvua bint Mashu (Mama Daisy), wa tatu
Bi. Titi Mohamed akifuatiwa na Bi. Zainab mke wa Tewa
Said Tewa

Kushoto Dossa Aziz, Julius Nyerere, Abdul Sykes na Lawi Sijaona

Saturday 9 July 2016





Mwinyi Baraka


Kushoto: Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Julius Nyerere, Sheikh Abdallah
Chaurembo, Rashid Kawawa na Tewa Said














Photo: Mwinyi Baraka na Julius Nyerere
Mwinyi Baraka na Nyerere

Photo: Muslim Academy Zanzibar
Watatu kulia ni Mwinyi Baraka Sheikh Said Omar Abdallah

Kutoka kulia kwenda kushoto: Waliokaa: wa kwanza ni Sayyid Ahmad Hamid Mansab Ibn Shaykh Abi Bakr bin Salim (alikuwa akisomesha Nahw, na Sarf); wa pili kutoka kulia ni Al-ällama alkabir Sheikh Sulaiman bin Muahammad Al-Alawi - huyu bwana ni mwalimu wa karibu maulamaa wote wa Zanzibar na nchi jirani za Afrika ya Mashariki- alilkuwa bahari isiyo na fukwe kwenye elimu mbali mbali. 

Yeye alisomesha Fiqh; Arudhi (elimu ya fani ya kutunga mashairi ya Kiarabu); Balagha na kadhalika. Ni shida, kama si muhali, kumpata mwana chuoni ye yote katika Afrika ya Mashariki, Kati na Kusini, asiwe mwanafunzi wa Maulana huyu: Allah yarhamhu.

Maisha yake yote yalikuwa katika kusomesha dini tu, tokea anaamka hadi anakwenda kulala.
Msikiti Gofu ulikuwa ndio mahali anaposomesha kuanzia baada ya sala ya Alfajiri, hadi baadaye kwenda Muslim Academy, na akirudi baada ya sala ya Adhuhuri hadi baada ya sala ya Isha. Allah yarhamhu wa yuskinuhu al-Janna.

Wa tatu kutoka kulia na Sayyid Umar bin Abdallah Ibn Shaykh Abi Bakr bin Salim (Mwinyi Baraka). Yeye alikuwa Mwalimu Mkuu wa Muslim Academy. Wa nne kutoka kulia ni Sayyid Abdurrahman bin Hamid Al-Sirry - Huyu Bwana alikuwa bahari katika elimu za Lugha, Mashairi na fani nyengine. Yeye alisomesha Arabic Literature (al-Adab al-Arabiyy).

Wa tano kutoka kulia ni Sayyid Ali Badawi Jamalullayl- huyu Bwana alikuwa alim mkubwa sana. Alisomesha Jiographia ya Nyota, Sayari na Ardhi. Vile vile alisomesha Elimu ya Maani na Balaghah



Thursday 31 March 2016

Utangulizi

Baada ya kumsikiliza Aman Thani akieleza shida na unyama waliokuwa wakifanyiwa jela swali la kwanza lililonijia ni kuwa inawezekanaje Waislam wakafanyiana unyama wa kiwango kile ilhali Allah amesema Muislam nduguye ni Muislam na Zanzibar ndiyo ilikuwa kitovu cha Uislam Afrika ya Mashariki na Kati?

Zanzibar inarejea hivi sasa kule ilikotoka. Wazanzibari hawajajifunza? 

Thursday 28 January 2016





Katikati ni Abeid Amani Karume na mstari wa nyuma wa tatu kulia
ni Mtoro Reahani picha hii Karume alipiga na viongozi wa Young Africans Dar es Salaam
mwaka wa 1948


Merry Black Birds Band
Kushoto waliokaa wa pili ni Ahmed Rashad Ali akifuatiwa na Ally Sykes wa mwisho kulia ni Abdallah Matesa
Waliosimama wa pili ni Abbas Sykes picha ilipigwa Zanzibar katika miaka ya mwanzoni 1950

''...Dome Budohi vilevile alipata kupiga muziki na Skylarks, bendi maarufu na iliyopendwa na vijana wa Dar es Salaam katika miaka ya 1950. Wanamuziki wengine walikuwa Abdulwahid, Ally na Abbas Sykes pamoja na Said Kastiko, Abdallah Athmani Matesa na vijana wengine kutoka Afrika Kusini kama Khomo na James Msikinya. Kabla hajafariki, Kleist Sykes ndiye aliyekuwa mdhamini wa bendi hii na ndiyo alionunua vyombo vya bendi. Ally Sykes aliporudi kutoka Nairobi baada ya vita na Kleist alipotambua mapenzi ya mwanae katika muziki, alimnunulia vyombo vya bendi ili kumfanya asiondoke tena kurudi Kenya. Bendi hii ilipendwa sana na ndiyo bendi pekee iliyokuwa ikipiga muziki wa Kizungu kama vile jazz, foxtrot, waltz na mitindo mingine kama hiyo. Bendi hii baadaye ilibadilisha jina na kuitwa Blackbirds. Maangazo ya radio yalipoanza Tanganyika mwaka wa 1952, midundo ya Blackbirds ilikuwa haikosekani kusikika radioni, Sauti ya Dar es Salaam...''

Kushoto: Prof. Mohamed Bakari na Mwandishi
Fatih University, Instanbul

Saturday 23 January 2016



Kushoto Bilali Rehani Waikela akiwa katika mahakamani Morogoro kusikiliza kesi ya Sheikh Ponda

Bilali Rehani Waikela akiwa na Wakili Juma Nassoro Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam alipokuja kama shahidi katika kesi ya Sheikh Ponda Issa Ponda

Friday 22 January 2016




Wagombea wa TANU katika Uchaguzi wa Kura Tatu 1958



Sheikh Ali Muhsin Barwani mwandishi wa ''Conflict and Harmony in Zanzibar.'
Dubai (1997)'

Kleist Sykes
Kushoto: Prof. Saida Othman Yahya Prof. Issa Shivji wakimhoji mwandishi kuhusu Mwalimu Julius Nyerere.
Hawa ni katika jopo linalofanya utafiti ili kuandika kitabu cha maisha ya Mwalimu Nyerere


itunes pic

Tafadhali bonyeza link hiyo hapo chini usikilize mahojiano ya Deus Gunze na Mohamed Said



Katika kitabu chake cha "The life and Times of Abdulwahid Sykes (1924-1968): The untold story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika" mwandishi Mohamed Said anaangalia mchango wa waislam katika harakati za kuleta uhuru wa Tanganyika. Je waislam ndio walioanzisha TAA na TANU? Je ni kweli Mwalimu Nyerere alinyakua TANU toka kwa waislam na kukifanya kuwa chombo cha kanisa? Nani alisaidia sana kuleta uhuru wa Tanganyika kati ya Mwalimu Nyerere na Abdul Sykes? Sikiliza zaidi.

Raia Mwema Januari 27 - 2 Februari 2016 uk. 12






Kamati Ndogo ya Siasa Ndani ya TAA, 1951

''Hakuna nyaraka zozote zinazoonyesha kama African Association ilikuwa imetayarisha mpango wa kushughulikia hali ya siasa.  Kuelewa mwelekeo wa siasa kama wakati ule inabidi mtu atazame mwenendo wa viongozi wa TAA na jinsi walivyokuwa wakiyashughulikia mambo tofauti yaliyokuwa yakiwadhili wananchi. Jambo la kwanza alilofanya Abdulwahid mara tu baada ya kuingia madarakani ni kuunda TAA Political Subcommittee (Kamati Ndogo ya Siasa ya TAA)  iliyomjumuisha yeye mwenyewe Abdulwahid, Sheikh Hassan bin Amir kama mufti wa Tanganyika; Dr. Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu, Said Chaurembo aliyekuwa liwali wa mahakama ya Kariakoo; John Rupia na Stephen Mhando. Kazi ya kamati hii ilikuwa ni kushughulika na masuala yote ya siasa katika Tanganyika. Kuundwa kwake ndiyo hasa ulikuwa mwanzo wa siasa za dhahiri katika Tanganyika na mwanzo wa harakati za kudai uhuru wa Mtanganyika.'' 


Kutoka kitabu cha ''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes...''


John Iliffe




Dr. Vedasto Kyaruzi





Kushoto Prof. Haroub Othman, Ahmed Rashad na Sheikh Ahmed Islam


''Mwaka a 1986, miaka miwili kabla, baada ya takriban miaka ishirini na tano ya ukimya, Ally Sykes alikubali kufanya majadiliano na mwandishi wa Kiingereza kutoka Africa Events, Paula Park. Park akachapisha majadiliano aliyofanya na Ally Sykes kuhusu ukoo wa Sykes  na mchango wao katika historia ya uhuru wa Tanganyika.Makala ile iliposomwa Ally Sykes akawa anapata simu kutoka kwa marafiki zake na kwa wafanyabiashara wenzake wakitaka uhakika kama yale yaliyoandikwa katika gazeti lile kweli yeye ameyasema. Haukupita muda mrefu, maofisa wa Idara ya Uhamiaji walimtembelea Park na kumuomba aondoke nchini.''
Kutoka kitabu cha ''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes...''


Baraza la Wazee wa TANU 1955






''Barua hii ya Mzee Kawawa kwa Ally Sykes ilikuwa ikimfahamisha Ally Sykes hali ya siasa Kanda ya Ziwa. Hii barua hadi leo ipo katika nyaraka za akina Sykes. Nilipokaa na Ally Sykes kutaka maelezo ya barua ile aliyoandikiwa na Kawawa, Ally Sykes alinipa kisa hiki:

Mwaka 1951 nilichaguliwa kuwa katibu mkuu wa Tanganyika African Government Servants Association (TAGSA). Chama hiki kiliundwa mwaka wa 1927 kwa lengo la kuendeleza maelewano mazuri baina ya serikali ya Malkia na sisi watumishi Waafrika. Rashid Kawawa alikuwa mwana kamati. Mimi nilichaguliwa pamoja na Thomas Marealle kama rais wa TAGSA. Katiba ya TAGSA iliamuru uchaguzi wa kila mwaka, na mimin nilirudishwa madarakani kama katibu mara nne hadi Oktoba, 1954 nilipojiuzulu baada ya kuhamishwa kwenda Korogwe kama adhabu kwa kuwa miongoni mwa wale wanachama 17 waliounda TANU. Watu kadhaa walishika urais. Stephen Mhando na Dr Wilbard Mwanjisi wote hao waliwahi kuchaguliwa kuwa marais wa TAGSA. Miongoni mwa wanachama watendaji wa TAGSA walikuwa Dr Michael Lugazia na Rashid Kawawa ambao alichaguliwa kuwa katibu baada ya mimi kujiuzulu. Kupitia TAGSA, Kawawa alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Tanganyika Federation of Labour (TFL).''

Kanyama Chiune (1927 - 2007)



Excerpts from Dictionary of African Biography, Oxford University Press, New York 2011
Paul von Lettow-Vorbeck, 1933
Paul von Lettow-Vorbeck

Guerilla East Africa WWI Colonel Von Lettow-Vorbeck Germany Bio Edwin Hoyt 1981



Balozi Abbas Kleist Sykes akihojiwa na Mwandishi

Kleist Abdulwahid Sykes (1950 -)
Kushoto: Dossa Aziz, Julius Nyerere, Abdulwahid Sykes na Lawi Sijaona 1957

Kleist (Abdallah) Sykes Mbuwane (1894 - 1949)

Friday 15 January 2016


MAPITIO YA KITABU SIMBA WA VITA KATIKA HISTORIA YA TANZANIA RASHIDI MFAUME KAWAWA

Na Mohamed Said

Kwa mara ya kwanza Tanzania ilishuhudia kuandikwa kwa historia ya mmoja wa viongozi wakuu wake kupitia kitabu “Simba wa Vita Katika Historia ya Tanzania Rashidi Mfaume Kawawa” kilichoandikwa na Dk. John M. J. Magotti. Sidhani kama katika historia ya Tanzania kuna kumbukumbu ya kuandikwa kwa kitabu kinachohusu maisha ya kingozi yoyote achilia mbali kufanyika kwa sherehe ya kukizindua kitabu hicho Ikulu ikiongozwa na rais mwenyewe.  Kwa hakika sherehe ilifana sana na tukakisubiri kwa hamu kitabu madukani ili tupate kunufaika na kumbukumbu za Mzee Kawawa.

Msomaji anaweza kukisoma kitabu chote chenye kurasa 127 kwa muda wa saa moja akawa kakimaliza chote na atakapokiweka chini akawa hakubakia na chochote cha maana katika fikra yake. Kwa nini iwe msomaji asibaki na kumbukumbu yoyote ya kiongozi mkubwa kama Mzee Kawawa mtu aliyeshuhudia kwa macho yake mwenyewe harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika na si hivyo tu yeye mwenyewe ni mmoja wa wale waliopigania uhuru wa Tanganyika na kushika nyadhifa kubwa za uongozi chini ya Mwalimu Julius Nyerere. Kwa kawaida vitabu vya maisha ya viongozi hasa wapigania uhuru huwa vina mambo mengi  sana ambayo kwa muda mrefu huwa siri, hayafahamiki hadi hapo kitabu kitakapoandikwa ama kwa mkono wake kiongozi mwenyewe au kuandikwa na muandishi. Mifano ipo mingi. Kitabu kama “Mahatma Gandhi” klichoandikwa na Robert Payne au “Long Walk to Freedom” alichoandika Nelson Mandela mwenyewe au “Seeds of Freedom” alichoandika Bildad Kaggia hakika unapomaliza kusoma vitabu hivi lazima urudi nyuma kufungua kurasa hapa na pale kuzisoma upya zile sehemu zinasosisimua.

Huwezi kupata haya katika kitabu cha Mzee Kawawa. Huwezi kuyapata haya kwa kuwa mwandishi hakuandika kitu. Hakuandika kitu si kama Mzee Kawawa hana historia ya kusisimua na kuwa hana mengi ambayo wengi hawayajui katika maisha yake, nadhani mwandishi hakuwezakuja na jipya labda kwa sababu hakufanya utafiti wa kutosha kuweza kuandika kitabu kinachomuhusu simba wa vita aneunguruma. Kuna msemo wa Kiswahili usemao “Aungurumapo simba mcheza ni nani?” Kwa hakika simba wa vita hakuunguruma kabisa katika kitabu hiki. Sijui lawama zielekezwe wapi.

Mimi simjui Mzee Rashidi Kawawa kwa kiwango cha kusema naweza kunyanyua kalamu na kufanya pitio la kitabu kilichoandikwa kuhusu yeye. Nathubutu kuandika kuhusu kitabu chake kutokana na kumjua kwangu mimi nikiwa kama mwandishi na mtafiti ambae katika kutafiti kwangu nimekutana na jina la Mzee Kawawa hapa na pale katika nyaraka zilizo katika hifadhi ya ukoo wa akina Sykes. Nitatumia uzoefu wangu huu kueleza yale niliyoyaona katika nyaraka hizi na ninayojua kuhusu Mzee Kawawa na kufanya tathmini kwa yale niliyoyasoma katika kitabu cha Magotti.

Miaka kama ishirini iliyopita nikiwa kijana mdogo nilipata hamu ya kuandika historia ya kudai uhuru wa Tanganyika. Sikuona mtu wa kumuendea isipokuwa Ally Sykes. Nilipomueleza kuwa nia yangu ni kuandika kitabu kuhusu marehemu kaka yake Abdulwahid Sykes (1924- 1968) Ally Sykes alinambia kuwa atanipa nyaraka zake zote nizipitie kisha ndiyo nakaenae chini kwa mahojiano ya ana kwa ana. Katika nyaraka alizonikabidhi ndani yake nilikuta barua ya mkono aliyoandika Rashid Kawawa mwaka 1952 kutoka Bukoba akimletea Ally Sykes aliekuwa Dar es Salaam. Barua hii ya Mzee Kawawa kwa Ally Sykes ilikuwa ikimfahamisha Ally Sykes hali ya siasa Kanda ya Ziwa. Hii barua hadi leo ipo katika nyaraka za akina Sykes. Nilipokaa na Ally Sykes kutaka maelezo ya barua ile aliyoandikiwa na Kawawa, Ally Sykes alinipa kisa hiki:

Mwaka 1951 nilichaguliwa kuwa katibu mkuu wa Tanganyika African Government Servants Association (TAGSA). Chama hiki kiliundwa mwaka wa 1927 kwa lengo la kuendeleza maelewano mazuri baina ya serikali ya Malkia na sisi watumishi Waafrika. Rashid Kawawa alikuwa mwana kamati. Mimi nilichaguliwa pamoja na Thomas Marealle kama rais wa TAGSA. Katiba ya TAGSA iliamuru uchaguzi wa kila mwaka, na mimin nilirudishwa madarakani kama katibu mara nne hadi Oktoba, 1954 nilipojiuzulu baada ya kuhamishwa kwenda Korogwe kamaadhabu kwa kuwa miongoni mwa wale wanachama 17 waliounda TANU. Watu kadhaa walishika urais. Stephen Mhando na Dr Wilbard Mwanjisi wote hao waliwahi kuchaguliwa kuwa marais wa TAGSA. Miongoni mwa wanachama watendaji wa TAGSA walikuwa Dr Michael Lugazia na Rashid Kawawa ambao alichaguliwa kuwa katibu baada ya mimi kujiuzulu. Kupitia TAGSA, Kawawa alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Tanganyika Federation of Labour (TFL).

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulipokuja kuzuru Tanganyika Agosti, 1951 kwa mara ya tatu, vyama vyote viwili, TAA na TAGSA, viliwakilisha malalamiko kwa ujumbe huo. TAGSA iliwakilisha malalamiko yake kuhusu ubaguzi katika utumishi serikalini kwa mujibu wa kupanga mishahara kufuatana na rangi ya ngozi. Mshahara wa Mwafrika ulikuwa wa chini zaidi kuliko ule aliokuwa akipokea Mzungu au Muasia kwa kazi hiyo hiyo. Kwa mfano Mwandishi wa hati mkato Mzungu alikuwa akipata mshahara mkubwa kuliko Mwafrika aliyekuwa na shahada au digrii kutoka chuo Kikuu cha Makerere. TAGSA vilevile tulilalamika kuhusu kuajiri makarani wa kutoka India na hali walikuwepo Waafrika kutoka Afrika ya Mashariki na Nyasaland ambao wangeweza kujaza nafasi hizo kwa urahisi.

Vyama vyetu hivi viwili TAA na TAGSA viliwakilisha malalamiko haya tukifahamu fika kwamba Uingereza ilikuwa ikiitawala Tanganyikachini ya vifungu nambari 76 na 77 vya Umoja wa Mataifa ambavyo viliwekwa ili kuendeleza maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ya nchi zilizokuwa chini ya udhamini. Kama mdhamini Uingereza ilitakiwa kuhimiza na kuheshimu haki za binadamu na uhuru wa kwa wote bila kubagua kwa misingi yajinsia, lugha au dini. Lakini Uingereza ilikuwa ikipuuza vifungu hivi bila aibu. TAGSA tuliwakilisha malalamiko haya ili Umoja wa Mataifa ujue matatizo halisi ya ukoloni nchini Tanganyika.

Mimi nikiwa katibu wa TAGSA nilifuatilia serikalini masuala yaliyoainishwa ndani ya malalamiko yetu. Suala lililokuwa likituhangaisha sanawakati ule ilikuwa uajiri wa Wahindi kutoka India, jambo ambalo niliieleza serikali halikuwa na faida, maadam kulikuwako na Waafrika ndani ya nchi ambao wangeweza kujaza nafasi zile. Jambo hili lilikuwa likisababisha manugíuniko makubwa miongoni mwa Waafrika. Hakuna majibu maridhawa yaliyopatikana kutoka kwa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa. Barua tulizoandika serikalini juu ya masuala hayo zilipuzwa na Chief Secretary, Bruce Hutt. Katika kufuatilia malalamiko haya, Niliandika barua moja kali sana na kwa mara ya kwanza bila kutafuna maneno niliuliza uhalali wa Waingereza kututawala Waafrika wa Tanganyika. Nillimwambia Katibu Mkuu kuwa kwa kuwa serikali imeshindwa kupata ufumbuzi kwa matatizo ya Waafrika, Uingereza lazima ijitoe Tanganyikana Umoja wa Mataifa utawale Tanganyika. Barua hiyo ilimkasirisha Katibu Mkuu na siku chache baadaye nilipokea barua kutoka serikalini iliyokuwa imejaa vitisho, dharau, stihizai na makemeo. Nikajibiwa kuwa hakuwa na suala la Umoja wa Mataifa kutekeleza utawala wa moja kwa moja Tanganyika.

Dkt Mwanjisi alikuwa amegusa suala nyeti sanakwa kuzungumzia matatizo ya ubaguzi wa rangi uliokuwa ukitukabili Waafrika wa . Kawawa, kama mjumbe wa kamati, akaniandikia barua akanitahadharisha nisichapishe ile hotuba ya Dkt Mwanjisi katika jarida la TAGSA bila idhini ya kamati ya utendaji. Kufuatia majibishano haya kati ya TAGSA na serikali, Dkt Mwanjisi kama alivyofanyiwa Dk Kyaruzi kabla yake, akahamishwa kutoka hospitali ya Sewa Haji mjini Dar es Salaamhadi Kingolwira Prison Hospitalkaribu na Morogoro. Kawawa na yeye akapewa uhamisho kwenda Bukoba na mimi nikapewa uhamisho kwenda Mtwara. Dk Mwanjisi na Kawawa walikubali uhamisho wao na wakaondoka Dar es Salaam. Mimi nilikataa uhamisho na nikabakia Dar es Salaam kupinga uhamisho wangu.

Alipokuwa Bukoba ndipo Kawawa akamwandikia Ally Sykes barua ile ya mwaka 1952 akimweleza hali ya siasa kamaalivyoikuta Kanda ya Ziwa. Huyu ndiye Kawawa niliyemjua mimi kupitia nyaraka na mahojiano na Ally Sykes. Kwa kweli inasikitisha kuwa Dk Magotti hakupata fursa ya kuziangalia nyaraka hizi muhimu sana katika siyo historia ya Kawawa bali katika historia ya kuundwa kwa TANU na kudai uhuru wa Tanganyika. Endapo angepata nafasi ya kuziona hizi nyaraka zingempelekea katika kuwajua wazalendo wengine waliotajwa mle ndani kama Dk. Kyaruzi, Dk. Wilbard Mwanjisi ambao Kawawa alikuwanao katika harakati za TAGSA. Katika majina hayo angeweza kudodosa mengi kutoka kwa Mzee Kawawa na hivyo kuandika yale ambayo hayafahamiki kwa wengi. Hii imgekifanya kitabu kiwe cha maana.

Mathalan Kawawa angeeleza mtafaruku kati ya Mwalimu Nyerere na Dk. Mwanjisi nini chanzo chake na nini ikajakuwa matokeo yake. Halikadhalika angempa fursa Mzee Kawawa kumuhadithia mchango wa Dk. Michael Lugazia katika kuasisi kwa TANU hasa kipindi kile cha 1953 wakati TAA ilipokuwa inatayarisha rasimu ya katiba ya TANU. Kwa ufupi ni kuwa Dk Lugazi alikuwa akijaribu kuamsha ari ya TAA Bukoba ari iliyokufa kutokana na kufungwa kwa kiongozi wa TAA Bukoba Ali Migeyo. Kisa cha Ali Migeyo ni moja ya visa vinavyosikitisha sana katika historia ya Tanganyika kwani aliwekwa kizuizini na Mwalimu Nyerere kama alivyofungwa na Waingereza. Haiwezekani kuwa Kawawa asiwe na habari na kile kilichopelekea mpigania uhuru hodari kama Ali Migeyo aishie jela tena wakati nchi ikiwa huru. Migeyo alifungwa na wakoloni kwa kuwahamasisha Watanganyika kudai uhuru labda Mzee Kawawa angeulizwa angeeleza ni nini kilitokea wakaamua kumfunga Migeyo kama walivyomfunga Waingereza.

Kitabu kimegusia kazi alofanya Kawawa kama mtumishi wa serikali ya kikoloni katika kambi za raia wa Kenyawalioshukukiwa kuwa ni Mau Mau.  Katika hawa wafungwa walikuwawepo wananchama wa TANU ingawa hawa walikuwa Wakenya. Maarufu katika hawa alikuwa Dome Okochi Budohi (ambae kadi yake ya TANU ilikuwa na 6) na Patrick Aoko. Budohi alicheza senema pamoja na Kawawa iliyoitwa “Wageni Wema.” Kawawa na Budohi walikuwa wakifahamiana vizuri sana kwa sababu wote walikuwa wasanii. Budohi alikuwa mmojawapo katika bendi ya vijana wa mjini iliyojulikana kama Skylarks. Bendi hii baadaye ilibadilisha jina na kuitwa Blackbirds. Matangazo ya radio yalipoanza Tanganyika, Blackbirds midundo ya Blackbirds ilikuwa haikosekani kusikika radioni katika Sauti ya Dar es Salaam. Kawawa kama walivyo vijama wote wa Dar es Salaam wa wakati ule alikuwa mmmoja wa wapenzi wa bendi hii na alikuwa hakosekani Ukumbi wa Arnatouglo bendi hii ikitumbuiza katika ile miaka ya 1950. Ilikuwa katika ule upigaji muziki wa Budohi ndipo alipoungana na Kawawa katika kutengenezwa kwa senama hiyo ya “Wageni Wema” ambayo mwandishi kaitaja lakini aliishia hapo tu.

Budohi na Aoko ni kati ya wafungwa wa Mau Mau waliokuwa Handeni ambako Kawawa alikuwa na jukumu la kuwaangalia. Budohi ndiyo alikuwa mtu wa kati baina ya TAA na KAU na kuanzia hali ya hatari ilipotangazwa Kenya mwaka 1952 Budohi na Aoko wakawa katika jicho kali la makachero. Makachero hawa Waafrika wanafahamika na wengine walikuja kufanya kazi hiyohiyo katika Tanganyikahuru.  Hiki ndicho kipindi ambacho Kaimu Rais wa TAA na Katibu wa TAA Abdulwahid Sykes alipokutana na Kenyatta Nairobi. Wakati Wakenya hawa wanafungwa Tanganyika, viongozi wa KAU akina Bildad Kaggia, Jomo Kenyatta, Kun’gu Karumba, Achieng Oneko, Paul Ngei na Fred Kubai walikuwa wamekamatwa Kenya. Kawawa ni mmoja kati ya viongozi hawa na ingependeza sana kama kupitia kwake tungeelezwa jinsi KAU na TAA ilivyokuwa ikishirikiana kwani haiwezekani kuwa Budohi na Kawawa uswahiba wao ukaishia kwenye kucheza senema tu.

Wanaharakati wote walishtushwa na kutiwa mbaroni kwa Budohi na Aoko. Haiwezekani kuwa iwe Mzee Kawawa kasahau matukio haya muhimu. Budohi na Aoko walikuwa wamefungwa minyororo walipokuwa katika selo pale Kituo cha Kati cha Polisi kwa sasa jumba hiloliko kituo cha mabasi kinachojulikana kama“station.”  Waliwekwa pale kwa miezi sita muda wote wakiwa na minyororo miguuni. Waliwekwa pale kwa miezi sita wakihojiwa kabla hawajapelekwa Handeni walipomkuta Kawawa. Hivi ndivyo vitu ambavyo kwa hakika vingeongeza ladha ya kitabu cha Mzee Kawawa endapo mwandishi angechukua muda kutafiti na kuzungumza na watu waliokuwa katika harakati wakati ule ambao bado wa hai kama Ally Sykes na mdogo wake Balozi Abbas Sykes na wengine wengi ambao walikuwepo wakati ule kama Mzee Chipaka.

Katika migomo ya wakati wa kudai uhuru hakuna mgomo uliofanikiwa na kuvuta hisia za wananchi kamamgomo wa reli wa mwaka 1960 uliodumu kwa siku 62. Ukiachia kutajwa tu kama sehemu ya historia undani wake na jinsi mipango yake ilivyokwenda na nafasi ya viongozi wa Tanganyika Railway African Union (TRAU) walivyopata misaada kutoka nchi za Mashariki hivi havijawekwa wazi. Si treni, meli wala mabasi ya railway yaliyotembea kwa mieizi mitatu. Mipango ya mgomo huu ilifanyika Tabora ambako ndiko palikuwa na karakana kuu ya reli na hapo ndipo palipokuwa makao makuu ya viongozi wa TRAU, Salum Abdallah mwenyekiti na Kassanga Tumbo katibu. Kawawa ana mengi katika kadhia hii kwa kuwa yeye wakati ule ndiye alikuwa Katibu Mkuu wa TFL. Inasemekana mgomo huu miezi michache kabla Tanganyika haijapata uhuru ndiyo ilikuwa kama zinduo kwa Mwalimu Nyerere kutambua kuwa hakuwa peke yake na sauti kwa wananchi. Walikuwapo viongozi wengine pembeni yake ambao nao wakipiga wananchi wanacheza. Ilimdhihirikia kuwa huko mbeleni wanakokwenda ipo siku atapambana na viongozi hawa. Hivyo ndivyo ilivyotokea.

Inasemekana Mwalimu Nyerere akimtumia Kawawa alianza mipango kabambe ya kujitayarisha hilolisitokee. Hii ilikuwa nukta muhimu sanakwani haukupita muda baada ya uhuru kupatikana mwaka wa 1961 viongozi hawa wa vyama vya wafanyakazi wakajikuta wamewekwa kizuizini. Wasomaji wangependa kujua Kawawa alijihisi vipi wakati viongozi wenzake wa vyama vya wafanyakazi aliofanya nao kazi wakati wa kudai uhuru wakishirikiana na TANU kama Victor Mkello, Paul Pamba, Abdallah Mwamba, Hassan Khupe, Salum Abdallah na wengine wengi walipokamatwa mwaka wa 1964 na kuwekwa kizuizini kwa amri ya Mwalimu Nyerere. Maelezo ya Mzee Kawawa katika mambo haya yangetia mwanga katika yale mengi yasiyofahamika katika historia ya Tanzania.

Waislam wangependa sanakujua hisia za Kawawa kama muumini alihisi vipi wakati makachero walipomvamia mzalendo aliyepigania uhuru wa Tanganyika Mufti wa TanganyikaSheikh Hassan bin Amir usiku wa manane na kumrudisha Zanzibar na kuwekewa masharti kuwa hana ruhusa kurejea Tanzania Bara. Nilitegemea kusoma sakata zima la kukamatwa kwa Sheikh Hassan bin Amir na kuvunjwa kwa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) jumuia ya Waislam iliyokuwa ikipanga kujenga Chuo Kikuu Dar es Salaam.

Nilitegemea halikadhalika kusoma mchango wa Mzee Kawawa katika kuunda Bakwata. Mengi yamesemwa kuhusu hujuma hii kwa Waislam moja wapo ni kuwa EAMWS ilivunjwa kwa shinikizo la Kanisa Katoliki likimtumia Mwalimu Nyerere. Hili si jambo la siri tena tafiti mbalimbali zimefanywa na vitabu kuandikwa na waandishi kutoka nje ya Tanzania kuhusu tatizo hili la kujitokeza udini mapema baada ya uhuru kupatikana. Kwa kuwa Kawawa alikuwa pamoja na Mwalimu Nyerere na alishiriki katika kuunda Bakwata wananchi hasa Waislam wangenufaika kusoma hisia zake wakati maamuzi hayo yanapitishwa na serikali. Kwa hakika kuna maamuzi mengi sanaambayo Kawawa alishiriki yaliwaumiza sanaWaislam katika juhudi zao za kujitafutia elimu. Waislam wangependa sana kujua ni kipi kilikuwa kinamsukuma kufanya vile.

Kwa yeyote atakaepata bahati ya kusoma kitabu cha maisha ya Mzee Kawawa ni wazi hatakuta jipya ambalo hakuwa akilijua kabla. Kwa ajili hii basi mlango bado uko wazi kwa watafiti wengine kuandika kitabu kuhusu Rashidi Mfaume Kawawa kwani maisha ya Mzee Kawawa bado hayajaandikwa. Hata hivyo tumpongeze mwandishi kwa kazi hii kwani ni baada ya yeye kutuandikia kitabu ndipo nasi tumepata nguvu ya kunyanyua kalamu zetu na kusema.

3rd January 2010