Showing posts with label nyakati. Show all posts
Showing posts with label nyakati. Show all posts
Thursday, 28 August 2025
Saturday, 24 February 2018
IKO WAPI TANGA ILE? HASSAN R HASSAN
Tanga ya
zamani zile, ya jagina Shaabani
Aliyesifika
kule, na kote Uswahilini
Mbona kama
izamile, haipo kwenye ramani
Iko wapi
Tanga ile?
Tanga yake
Jinamizi, Sheikih Ali Zakuwani
Ilo ikikaza
uzi, kwa mambo yenye thamani
Imegota zake
mbizi, nani wa kuiauni?
Iko wapi
Tanga ile?
Tanga ya
Mwalimu Pera, Pera bin Ridhiwani
Zama zake
iling'ara, na kushika usukani
Doro leo
yadorora, haitajwi midomoni
Iko wapi
Tanga ile?
Tanga ya
Sheikh Mdanzi, wa Hanasa muhisani
Iloenea
mapenzi, na baraka tani tani
Ya sasa ni
kama bunzi, makaziye jalalani
Iko wapi
Tanga ile?
Tanga ya
Mwinyihatibu, Mohamedi nambawani
Aloandika
vitabu, vizuri vyenye maani
Mbali
imejitanibu, haipo hatuioni
Iko wapi
Tanga ile?
Tanga ya
Sheikh Ghulamu, Mwabondo mtu makini
Aloifunza
kaumu, ushairi pamwe dini
Umekwisha
umuhimu, Tanga sasa Tanga duni
Iko wapi
Tanga ile?
Tanga ya
Sheikh Hemedi, Buhry wa Mnyanjani
Ilolea
auladi, kwa kumcha Rahmani
Imeenda
hairudi, imakeni hii shani
Iko wapi
Tanga ile?
Tanga ya
Sheikh Salimu, Kibao niambieni
Iko wapi
waadhamu, nikaishufu kwa mboni
Nikajifunze
nudhumu, nikiwamo Tanga ndani
Iko wapi
Tanga ile?
Tanga ya
Sheikh Saidi, Nuru aso mshindani
Ilopendwa ja
waridi, au vile asumini
Hae! Imezama
sudi, bahati si mara thani
Iko wapi
Tanga ile?
Tanga yake
Sheikh Ali, Hemedi mwanachuoni
Iliyotajika
mbali, Ulaya na Arabuni
Leo imelala
chali, waruka watu na nyuni
Iko wapi
Tanga ile?
Tanga yake
Mohamedi, Ali Buhry mwendani
Aliyekuwa
stadi, na fasaha wa uneni
Ilo sasa si
ya jadi, ya jadi i wapi kwani?
Iko wapi
Tanga ile?
Tanga ya
Sheikh Kigamba, gwiji la Chongoleani
Iliyotoa
miamba, waloongoza safuni
Kwa umbuji
walitamba, kilugha hata kifani
Iko wapi
Tanga ile?
Tanga ya
Sheikh Kihere, Kihere wa Vibambani
Ilotamba si
kwa sare, ingiapo shindanoni
Hadi wakaona
gere, kina fulani fulani
Iko wapi
Tanga ile?
Tanga yake
Abdalla, wa Baruwa Baruwani
Iliyokosa
kulala, kwa kukirimu wageni
Watu
wakanywa na kula, kindugu na kijirani
Iko wapi
Tanga ile?
Tanga ya
Mwalimu Mbega, yeye kwake ujombani
Wa kuiga
wakaiga, kwa mazuri kusheheni
Tangu yahame
mafiga, hakuna chungu jikoni
Iko wapi
Tanga ile?
Tanga ya bin
Matunga, Abdi alo rubani
Ilojaliwa
malenga, mwambao huu wa Pwani
I wapi nende
ienga, nikumbukie zamani
Iko wapi Tanga
ile?
I wapi ile i
wapi, Tanga ile nijuzeni
Imebadilika
vipi, toka juu kuwa chini
Na warithiwe
wa kupi, walipo nionesheni
Iko wapi
Tanga ile?
Hassan R Hassan
Hassan R Hassan
Saturday, 11 March 2017
RAMADHANI RASHID MADABIDA NA SOPHIA SIMBA JE WAMEFANYA ALIYOFANYA MSALITI ALEXANDAR TOBIAS?
Ofisi Ndogo ya Chama Cha Mapinduzi Patrice Lumumba Avenue |
Nina
hakika si wengi hata humo ndani ya CCM wamepata kusikia jina la Alexander
Tobias. Hawajapata kuisikia jina hili kama vile walivyokuwa hawajapata kusikia
majina ya wazalendo wengi walipigania uhuru wa Tanganyika. Tufatane katika kisa
hiki utakisikia kisa cha Alexander Tobias vile alikisaliti chama cha TANU hata
kabla hakijazaliwa.
Ilikuwa
mwaka wa 1987 niko ofisi ya Mzee Germano Pacha katika jengo la Biashara ya
Wazee Tabora nikiwa nimesindikizwa na wenyeji wangu wawili, Ali Salum Mkangwa
na Ilunga Hassan Kapungu. Ofisi hizi za wazee wa TANU zilikuwa takriban kila mkoa
khasa sehemu za mijini. Kazi yao kubwa ilikuwa kushughulika katika maduka yao
na bidhaa adimu kama vile mafuta ya kupikia, mchele, sukari na wakati mwingine
vitu kama sabuni nk. Hizi zilikuwa ni zile nyakati za hali ngumu sana ya uchumi
Tanzania kila kitu kiliadimika. Huyu Germano Pacha ni mmoja katika watu 17
waliounda pamoja na Mwalimu Nyerere chama cha TANU 1954. Nilikuwa niko katika
utafiti wa historia ya TANU na Sheikh Abubakar Mwilima aliniambia kuwa ni muhimu
nikamuhoji Mzee Germano Pacha kwani alikuwa anajua mengi katika historia ya
uhuru wa Tanganyika. Hakuwa Sheikh Mwilima peke yake aliyenipa ushauri huu.
Hassan Upeka aliyekuwa katika Idara ya Usalama ya TANU toka mwaka wa 1956 na
yeye pia alinishauri na kutia mkazo kuwa ni lazima niende Tabora nikazungumze
na Mzee Pacha. Alikuwa Mzee Germano Pacha ndiyo aliyonifahamisha kwa mara ya
kwanza kufukuzwa kwa kiongozi katika TAA wakati wa harakati za kudai uhuru wa
Tanganyika.
Mzee
Pacha anasema katika mkutano wa mwaka wa
1954 wa TAA mkutano ulioasisi TANU walimfukuza chama Alexander Tobias aliyekuwa
Katibu Mtendaji wa TAA Makao Makuu New Street kwa kosa la usaliti. Alexander
Tobias alichukua majalada ya TANU ya siri akawapa Waingereza kupitia idara yao
ya ujasusi Special Branch. Inasemekana Waingereza walimuhonga fedha nyingi kwa
kazi ile. Huyu Alexander Tobias alianza kazi pale New Street June 1953 wakati Mwalimu
Nyerere anachukua uongozi wa TAA. Alexander Tobias alikuwa mfanyakazi wa kwanza
kuajiriwa na TAA kama katibu wa kudumu pale Makao Makuu ya TAA. Uamuzi huu wa
kuwa na sekretariati pale Makao Makuu ulifanyika Nansio baada ya mashauriano kati
ya Abdul Sykes na Hamza Mwapachu wakati wanashauriana na wanafanya mipango ya
kumtia Nyerere katika uongozi wa TANU kupitia uchaguzi wa TAA wa April 1953.
Alexander
Tobias akaanza kazi June 1953 Nyerere akiwa Rais wa TAA na Abdul Sykes Makamo
wa Rais na hapo inaaminika ndipo alipodakwa na Special Branch na akawa sasa
anawapa siri za TAA na mwisho akawakabidhi majalada yenyewe. Ukipitia nyaraka
za Sykes za mwaka wa 1953 hiki ndicho kipindi ambacho TAA walikuwa wako
katika muendelezo wa mawasiliano na vyama vingine vya siasa nje ya mipaka ya
Tanganyika. Nimesoma barua kadhaa katika nyaraka za Sykes ambazo Alexander
Tobias alikuwa anaandika kwa niaba ya TAA kuiandikia serikali ya Kiingereza.
Katika barua hizo ziliyonivutia sana ni zile ya kumuombea ruhusa Ally Sykes kama kiongozi wa TAA kusafiri kwenda Lusaka, Northern Rhodesia kuhudhuria mkutano wa Pan African
Congress uliokuwa umeitishwa na Kenneth Kaunda akiwa kiongozi wa African
National Congress. Mkutano huu ulikuwa ujumuishe vyama vya siasa vilivyokuwa
Kusini ya Sahara kuzungumzia ukombozi wa nchi zao.
Ni wazi
Alexander Tobias kwa nafasi yake katika kipindi kile cha mpito kuelekea kuunda
TANU mwaka unaofuatia, alijua siri nyingi za chama na kwa kiasi kikubwa kwa usaliti wake aliwadhoofisha sana wazalendo wa TAA. Yale ambayo alifanya hakika ulikuwa ni
usaliti mkubwa ambao usingeweza kustahamilika ila yeye kufukuzwa chama na hicho
ndicho kilichofanyika siku ya kwanza tu katika mkutano wa TAA wa 1954. TANU
isingeweza kuwa na wanachama wasaliti wa mfano wa Alexander Thobias.
Nimekileta
kisa hiki baada ya kusoma katika mitandao ya kijamii kuwa kimepita kimbunga ndani ya mkutano wa CCM
Dodoma kinakumba wanachama waliokwenda kinyume na matakwa ya chama. Chanzo
kikiwa Uchaguzi Mkuu wa 2015. Baadhi wamefukuzwa chama, wengine wamepewa
karipio kali na wengine wamesamehewa. Ni
muhimu sana kwa chama kuijua historia yake. Bahati mbaya CCM haina historia
ukiacha ile ya kuundwa kwake mwaka wa 1977. CCM haina moja walijualo katika
historia ya TANU na ukombozi wa Tanganyika. Ndipo pale mwanzo nikasema
tufuatane ili tumjue msaliti Alexander Tobias. Ikwa huijui jana yako huwezi
ukaijua leo yako. Ndiyo leo hii bado tunapapasa kama vipofu katika mengi ambayo laiti tungeijua historia yetu bila shaka tungeijua na mila ya siasa zetu katika vyama vya siasa.
Alexander
Tobias aifukuzwa chama kwa usaliti dhahiri. Swali la kujiuliza ni hili. Hawa
waliofukuzwa CCM wamefukuzwa kwa usaliti? Kisa chao kinajulikana na kinatokana
na uteuzi wa nafasi ya mgombea urais katika CCM. Tofauti zao zilitokea hapa. Yawezekana
kweli msimamo wa kumuunga mkono huyu na kumpinga yule katika chama cha siasa ikawa kosa kiasi
kupelekea watu kufukuzana chama? Ikitokea mathalan Katibu Mtendaji wa CCM
akaiba majalada pale Makao Makuu Dodoma akayauza kwa wapinzani kama alivyofanya
Alexander Tobias 1953, kosa hili ni wazi ni la mwanachama kufukuzwa chama kwani
ni usaliti. Hili la wanachama kugongana katika uchaguzi wa nani apeperushe
bendera kugombea urais wa nchi kupitia CCM hukumu yake inahitaji utulivu wa
fikra.
Nampa pole ndugu yangu Ramadhani Madabida kwa yaliyomfika.
Nampa pole ndugu yangu Ramadhani Madabida kwa yaliyomfika.
Nakumbuka
kama jana vile siku nilipomuona Madabida katika TV akizungumza pale Lumumba akajaribu
kumnadi alyedhaniwa ni mgombea wake wa urais mbele ya vyombo vya habari. Mashaallah Madabida
ni mzungumzaji hodari anaejua kuchagua maneno yake kwa uzito unaostahili.
Madabida alizungumza vizuri sana hadi akafika kuinukuu Qur’an.
Zamani sana nilimuazima Madabida kitabu kinaitwa, ‘’Khrushchev Remembers.’’ Katika kitabu hiki utamu unakuja pale Stalin alipokufa na pakawa na ombwe zito na ombwe hilo likazua mvutano kati Nikita Khrushchev na Lavrenty Beria. Kati ya kambi mbili hizi ipi ichukue uongozi? Mwisho wa kinyang’anyiro kile mshindi alipatikana na damu nyingi ilibaki sakafuni.
Nawafananisha Madabida, Sophia Simba na wenzao waliofukuzwa pamoja na wale viongozi wa Chama Cha Kikomunisti cha Urusi waliopoteza maisha yao kwa kukimbilia kupanda jahazi lililokuwa liashapangiwa kuzamishwa.
Naamini Madabida anakikumbuka kitabu hiki na yale yaliyomfika Beria na wenzake.
Zamani sana nilimuazima Madabida kitabu kinaitwa, ‘’Khrushchev Remembers.’’ Katika kitabu hiki utamu unakuja pale Stalin alipokufa na pakawa na ombwe zito na ombwe hilo likazua mvutano kati Nikita Khrushchev na Lavrenty Beria. Kati ya kambi mbili hizi ipi ichukue uongozi? Mwisho wa kinyang’anyiro kile mshindi alipatikana na damu nyingi ilibaki sakafuni.
Nawafananisha Madabida, Sophia Simba na wenzao waliofukuzwa pamoja na wale viongozi wa Chama Cha Kikomunisti cha Urusi waliopoteza maisha yao kwa kukimbilia kupanda jahazi lililokuwa liashapangiwa kuzamishwa.
Naamini Madabida anakikumbuka kitabu hiki na yale yaliyomfika Beria na wenzake.
Friday, 10 March 2017
KIBATARI
Utangulizi
Nilipokuwa nasoma hizo beti za Kibatari nimepata faraja kuona kuwa Wazanzibari wamejifunza kujicheka na hii ni ishara nzuri. Huku kunashusha shinikizo la damu na huleta kicheko moyoni na kicheko huleta nuru katika uso. Nuru nayo huangaza pote.
Kibatari |
Ewe wangu kibatari
Utulize moyo wako
Wewe bado u mzuri
Liondowe sononeko
Umeme ulinighuri
Kukusahau mwenzako
Lakini sasa tayari
Takutafuta uliko
Na mie takugomeya
Nitoe kiburi chako
Wa Zeco ushazoweya
Huo ndo kiasi chako
Sasa kaka subiriya
TANESCO kiboko yako
Kibatari kibatari
Sikama sijakikubali
Kimelea wasomi mahiri
Hata huwezi amini
Swali langu jamani
Naomba mnijibuni
Wenye kosa ati ni walipaji kwani?
Suali hili ni kubwa
Liende mbele sambamba
Siku, wiki Na mwezimbamba
Mifuko yetu mwairamba
Tuelezwe kwa makini Kosa hili ni la
naniiii?
Mbona mwababaisha sana huku mkifunga
goli porini
Kibatari nakupenda Ila utaua
jamaniiiii
Ndugu yenu kibatari
Sitaki chenu kiburi
Mlinitupa duhuri
Kwa hiyo yenu ghururi
Na nyingi zenu shururi
Niliweza zisubiri
Nikawa kama kaburi
Wala hamnidhukuri
Mlikuwa mwafikiri
Kuwa mimi ni faqiri
Wapi wenu uhodari
Na ule ujemedari
Nawapeni tahadhari
Kosa msilikariri
Munitundike vizuri
Kwenye uzi wa hariri
Tuesday, 27 September 2016
MHESHIMIWA KATANI AHMED KATANI (CUF) MBUNGE KIJANA WA TANDAHIMBA (UKURASA WA NYONGEZA)
Inawezekana kabisa kuwa hata kwa mbali au hata kwa ndoto mbaya ya kutisha ya jinamizi Mh. Ahmed Katani alipatapo kufikiri kuwa itatokea siku yeye atasoma tamko la uamuzi wa kumfukuza Prof. Ibrahim Haruna Lipumba kutoka CUF. Kama wasemavyo wanasiasa wenyewe, siku ni muda mrefu sana katika siasa. Mwandishi alikutana na Mh. Katani siku chache zilizopita alipofika nyumbani kwake akiongozana na Mh. Riziki Shahari Mbunge wa Mafia Viti Maalum wakitokea Bungeni Dodoma. Mazungumzo aliyofanya na Mwandishi kwa muda mfupi kama ungewasikiliza utadhani wawili hawa walikuwa wanajuana kwa muda mrefu. Msomaji anaweza kusoma utangulizi hapo chini wa ukurasa ambao Mwandishi aliandika kama ufunguzi wa matumaini kuwa iko siku Mh. Katani atakuja na historia ya maisha yake katika siasa za upinzani. Mh. Katani Ahmed Katani tayari keshaingia katika jedwali la historia kwa kusoma tamko la kumfukuza Prof. Lipumba kutoka CUF.
Hivi yawezekana kwa Prof. Lipumba kumtazama usoni kijana wake Mh. Katani na akasema maneno aliyosema Julius Caesar, ''Et tu Brute?''
Msikikilize Mh. Katani hapo chini:
Utangulizi
Mheshimiwa Katani Mbunge wa Tandahimba ni kijana kwa maana halisi ya neno lenyewe. Katika muda mfupi wa kuzungumza nae kwa mara ya kwanza akisubiri kikombe cha kahawa alipopita nyumbani kwa Mwandishi, Mwandishi amegundua kuwa Mh. Katani amekalia kitabu ambacho ikiwa atakiandika kinatosha kuwa rejea ya kueleza adha za siasa za upinzani khasa wakati wa uchaguzi mkuu. Ukurasa huu umefunguliwa rasmi kumsubiri Mh. Katani afunguke kwa faida ya wapenda demokrasia...
Mheshimiwa Katani Mbunge wa Tandahimba |
Monday, 26 September 2016
MAPOKEZI YA MAHUJAJI UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE 1437
Mahujaji nje ya Uwanja wa Julius Nyerere |
Sheikh Abdallah Jabir
Ingia hapo chini kusikiliza mahojiano:
https://soundcloud.com/mohamed-said-1018/abdallah-jabir-haj-trust Katikati Prof. Mussa Assad kulia Ramadhani Sengati na Kushoto Masasi Kulia ni Sheikh Salim Mtambo |
Mtemi Ramadhani

Prof. Mohamed Bakari |
Kulia Prof. Mohamed Bakari na Said Mohamed |
Sunday, 18 September 2016
BALOZI DR. RAMADHANI KITWANA DAU APAA KWENDA KUALA LUMPUR KUIWAKILISHA TANZANIA
Dr. Ramadhani Kitwana Dau akiwa Uwanja wa Julius Kambarage Nyerere Dar es Salaam akielekea Kuala Lumpur Malaysia jioni ya leo kwenda kushika nafasiyake ya Ubalozi Nyuma akimsindikiza ni Mh. Mbaraka Dau Mbunge wa Mafia na aliyevaa kofia ni Bwana Lumba pia kutoka Mafia |
Friday, 16 September 2016
TENZI: FADHILA ZA MOLA - ARQAM
Hakika isiyo shaka
Yakini metajika
Ukumbini imefika
Ya Bwana Msifika
Humpa anomtaka
Fadhila zake Rabbuka
Hujawa bila mipaka
Zikatimu na kufika
Viumbe tuakitika
Amina Rabbi labeka
Alhamdu twatamka
Kukiri kufadhilika
Ewe kiumbe kumbuka
Mja ulositirika
Uendako hujafika
Mola wako hajkwita
Tenda ulowajibika
Jiepushe na pirika
Usije kughafilika
Dunia ikakupita
Sije pitwa na niaka
Ukaja vuka mipaka
Kaingiwa na mashaka
Ukabaki unajuta
Twakuomba wetu Mola
Ewe Subhana Taala
Ni wewe Jalla wa ‘Ala
Kwa sifazo tunakwita
Utukinge na balaa
Zilizo kwenye mitaa
Maovu yalozagaa
Maneno huwa muhibu...
Yalonenwa na sahibu...
Uwe karibu...
Tungo zipate khatibu...
''Msomi Bwana Saidi..
Pokea mkono wa Idi..
Leo kwako mefaidi..
Kunifukiza kwa udi..
Pokea mkono wa Idi..
Leo kwako mefaidi..
Kunifukiza kwa udi..
Zangu hini
shukrani..
Hakika sikuamini..
Kujiona hadharani..
Humo mwako sebleni...''
Hakika sikuamini..
Kujiona hadharani..
Humo mwako sebleni...''
Sunday, 11 September 2016
TENZI ZA KUTULIZA NYOYO DUA KWA MAHUJAJI NA KHKITANI
Ewe Mola Mtukufu
Twakuomba ya Raufu
Waja wako dhaifu
Dua zetu zipokea
Twakuomba ya Raufu
Waja wako dhaifu
Dua zetu zipokea
Ndugu zetu Isilamu
Walotimiza la muhimu
Nguzo ilio adhimu
Dua tunawaombea
Walotimiza la muhimu
Nguzo ilio adhimu
Dua tunawaombea
Kufika kwao Makka
Hilo halina shaka
Uwezo wake Rabbuka
Pasi na kutegemewa
Hilo halina shaka
Uwezo wake Rabbuka
Pasi na kutegemewa
Wageni wa sharafu
Katika miji mitukufu
Kwa Hijja na kutufu
Makka na Madina pia
Katika miji mitukufu
Kwa Hijja na kutufu
Makka na Madina pia
Zijaalie zao Hijja
Ziwe na nzuri tija
Pasiwe na hoja
Au kasoro kuingia
Wajaalie ya wepesi
Pasiwe hata tetesi
Kama nyeupe karatasi
Ibada zao zitoke doa
Uwape pia nguvu
Na akili Tulivu
Waepushie maovu Manasiki kukamilia
Kwa salama na kheri
Waja wako wazuri
Uwarejeshe safari
Hijja zao kutimia
Sala na salamu
Zimfikie Hashimu
Mtume Akiramu
Muhammad Nabiyya
Mola wetu Rabbana
Yailahi Subhana
Dua Twaomba sana
Mikono juu twainua
Yailahi Subhana
Dua Twaomba sana
Mikono juu twainua
Khkitani
*Allahuma Rabil Alamina
Twaitika Maalim Duana
Tena twakushuru sana
Kwa Dua kwa wetu Subhana
Azipoke ya Manani Maulana
Amina Yarabil Amina
Ahmed Al Brazil
Tena twakushuru sana
Kwa Dua kwa wetu Subhana
Azipoke ya Manani Maulana
Amina Yarabil Amina
Ahmed Al Brazil
Tuesday, 6 September 2016
KUTOKA MAKKA 1437
Fuatilia ukurasa huu In Shaallah tutaweka picha kila tuzipatapo za mahujaji kutoka Tanzania...
Kulia: Imam wa Msikiti wa Mtoro Sheikh Zuberi Yahya, Ustadh Mussa, Hafidh Mohamed Ali Hassan (Kibabu), Sheikh Othman Maalim na Ustadh Hassan (Picha kwa hisani ya Sheikh Zuberi Yahya) |
Sala ya Ijumaa Makka |
Saturday, 13 August 2016
JIONI MOJA NA MAALIM SEIF SHARIF HAMAD
Maalim Seif akizungumza na Mwandishi (haonekani kwenye picha) nyumbani kwake Dar es Salaam |
Mwandishi akimkabidhi Maalim Seif kitabu cha Kumbukumbu za Ali Muhsin Barwani ''Conflict and Harmony in Zanzibar.'' |
Kumtembelea Maalim Seif
nyumbani kwake ni mfano Waingereza wangesema ‘’a walk in the park,’’
Kiswahili chake labda mtu ungesema unatoka chumbani kw.ako unakuja sebuleni
yaani ni wepesi usiomithilika. Maalim nimefahamiananae kwa mara ya kwanza 1992
nilionananae Starlight Hotel Titi Street, Dar es Salaam. Hizi zilikuwa siku za mwanzo za
siasa za vyama vingi. Miaka mingi imepita na hapa katikati tukionana kwa mbali
sana na kwa muda mfupi mfupi ile ya kupeana salaam, Waswahili wanausemi, ‘’salaam
ya Mungu,’’ ikiwa na maana mnasalimiana kisha mnapitana kila mtu na hamsini
zake. Lakini namini Maalim akinisoma na wakati mwingine akinisikia katika
vyombo vya habari, pia wakati mwingine akipata salaam zangu kupitia jamaa na marafiki. Lakini
mimi Maalim nimenfuatilia kwa karibu na nimempiga picha nyingi sana kwa
kiasi ya miaka ishirini na zaidi.
Leo nimepata bahati ya kumfikia nyumbani
kwake Sharif Shamba nje na mbali na matarumbeta na shamrashamra za mikutano na mengineyo.
Ilikuwa starehe tukinywa kahawa na kucheka mfano tuko barzani tunapumzika. Lakini tabu kukutana na mtu kama Maalim Seif ukaacha kumdodosa lau kwa mbali kwa namna ya maskhara. Najua kitabu cha Ali Muhsin kakisoma kilipochapwa tu mwaka wa 1997 lakini niliona nimepelekee kuchokoza upya fikra zake. Mimi binafsi katik kitabu cha Ali Muhsin moja ya sehemu iliyokamata fikra zangu ni pale anapohadithia yale aliyokutananayo katika jela mbalimbali za Tanganyika wakati alipofungwa baada ya mapinduzi. Nikamrushia Maalim swali, ''Maalim tupate basi kitabu makhsusi ulipokuwa kifungoni.'' Kacheka kidogo. Nilikuwa nimemkumbusha mbali. Jibu lake lilikuwa, ''In Shaallah.'' Sikumuacha karibu nikaongeza na ''Memoirs...'' yaani kumbukumbu za maisha yake. Mara ya mwisho kuwa jirani sana na Maalim ilikuwa mwaka wa 2012 Bwawani Hotel nikiwa na TV Imaan tulikokwenda kumsikiliza Maalim akizungumza kuhusu hali ya Zanzibar na mategemeo ya wananchi.
Maalim alikuwa sasa yuko serikalini. Nakumbuka shida niliyowapa walinzi pale nilipoingia katika chuma cha faragha alipokuwa Maalim Seif, Mzee Hassan Nasoro Moyo na viongozi wengine. Mimi nilikuwa nje na wala sikuwa na nia ya kuingia ndani ya chumba kile kwani mtangazaji na mtu wa kamera tayari walikuwa ndani ya chuma kile wakishughulika. hawa vijana wote wana vitambulisho shingoni vinaning'inia na watu wa usalama weshawaruhusu. Mimi sina chochote lakini Ismail Jussa ndiye kanishika mkono tunazunguma basi hadi mle chumbani nikawa sasa uso kwa uso na Maalim. Ikawa sasa tunazungumza hili na lile, ''easy.'' Sasa nimefungua ''tablet,'' yangu nampiga picha Maalim na wakati mwingine kumwelekeza ''pose,'' niitakayo. Kumbe jamaa wa Usalama kidogo weshafanya wasiwasi wa kutaka kunijua mie nani. Mara niko kwa Mzee Moyo tunazunguza na kucheka. Lakini jamaa wa Usalama bado hawajanijua mie nani. Mara nimerukia Eddy Riyami basi ikawa kwao wao ni tafrani kidogo. Nilipotoka nje tu wakanifikia kwa maswali...
Jicho halisahau kile ambacho jicho la kamera liliona. Naomba kamera yangu ikuchukue katika barabara ya kumbukumbu turudi nyuma zaidi ya miaka ishirini iliyopita pale nilipoanza kufuatilia nyayo za Maalim na wale aliokuwa pamoja na yeye...
Maalim alikuwa sasa yuko serikalini. Nakumbuka shida niliyowapa walinzi pale nilipoingia katika chuma cha faragha alipokuwa Maalim Seif, Mzee Hassan Nasoro Moyo na viongozi wengine. Mimi nilikuwa nje na wala sikuwa na nia ya kuingia ndani ya chumba kile kwani mtangazaji na mtu wa kamera tayari walikuwa ndani ya chuma kile wakishughulika. hawa vijana wote wana vitambulisho shingoni vinaning'inia na watu wa usalama weshawaruhusu. Mimi sina chochote lakini Ismail Jussa ndiye kanishika mkono tunazunguma basi hadi mle chumbani nikawa sasa uso kwa uso na Maalim. Ikawa sasa tunazungumza hili na lile, ''easy.'' Sasa nimefungua ''tablet,'' yangu nampiga picha Maalim na wakati mwingine kumwelekeza ''pose,'' niitakayo. Kumbe jamaa wa Usalama kidogo weshafanya wasiwasi wa kutaka kunijua mie nani. Mara niko kwa Mzee Moyo tunazunguza na kucheka. Lakini jamaa wa Usalama bado hawajanijua mie nani. Mara nimerukia Eddy Riyami basi ikawa kwao wao ni tafrani kidogo. Nilipotoka nje tu wakanifikia kwa maswali...
Jicho halisahau kile ambacho jicho la kamera liliona. Naomba kamera yangu ikuchukue katika barabara ya kumbukumbu turudi nyuma zaidi ya miaka ishirini iliyopita pale nilipoanza kufuatilia nyayo za Maalim na wale aliokuwa pamoja na yeye...
Fatilia ukurasa huu...In Shaallah tunautengeneza....
Mwandishi akiwa Viwanja Vya Jangwani akifuatilia mkutano wa CUF na kupiga picha mwaka wa 2000 |
![]() |
Kalenda ya Maalim Seif kuingia Ikulu Zanzibar 1995 ilikuwa imewekwa kwenye maskani maarufu CUF ''Jaws,'' Stone Town |
Mwaka wa 2012 baada ya miaka 17 kupita na hali ya siasa za Zanzibar kubadilika, Maalim na CUF wakipata nguvu kila kukicha nilifanya mahojiano ya televisheni na Baraka Shamte, kada mkubwa wa CCM na mwana ASP. Wakati huu Maalim alikuwa Makamu wa Rais wa Zanzibar. Nimepata kumjadili Baraka Shamte mara kadhaa katika mitandao ya kijamii. baraka Shamte ni mtu mwenye histroia kubwa katika historia ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka wa 1964. Baraka Shamte ametunukiwa nishani ya miaka 50 ya mapinduzi.
![]() |
Mwandishi Akifanya Mahojiano na Baraka Shamte Kada Maarufu wa CCM Nyumbani
Kwake Mkunazini Zanzibar Kuhusu Historia ya Mapinduzi. Baraka Shamte ni Mtoto wa Mohamed Shamte Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Zanzibar Aliyepinduliwa Katika Mapinduzi ya 1964 |
Uchaguzi wa Mkuu Zanzibar 1995 Mwandishi akiwa nje ya kituo cha kupiga kura Darajani siku ili mvua kubwa ilipiga |
Shaaban Mloo na Kabourou kampeni za uchaguzi wa 2000 |
Kushoto: Prof. Ibrahim Lipumba, Shekue, Mama Ummie na Ummie biti yake.
Nilipokutana na Maalim kwa mara ya kwanza aliniuliza uwezekano wa CUF kupata wanachama Bara. Fikira ya Maalim ilikuwa ni kuwapata wazee wetu wa Dar es Salaam kuunga mkono chama. Mimi nikamwambia kuwa wazee wetu tuwaache kwa sasa tulenge vijana. Nakumbuka nilirudi tena kwa Maalim na baadhi ya vijana wachache viongozi na tukabadilishana mawazo.
Vijana hawa walikuwa wametokea chama cha National Reconstruction Alliance ambako mwenyekiti alikuwa Prof. Malima na alipokufa ikawa vijana wamepwelewa. Sasa Alipopatikana Prof. Lipumba moto ukawaka upya na matumaini mapya yakaibuka. Mwandishi ndiye ailiyemtambulisha Prof. Lipumba katika mkutano mkuu wa CUF. Tulikuwa tunaingia katika uchaguzi mkuu wa 1995. Mwandishi ndiye ailiyemtambulisha Prof. Lipumba katika mkutano mkuu wa CUF. Tulikuwa tunaingia katika uchaguzi mkuu wa 1995. Kwa kuwa mwandishi hakuwa mjumbe katika mkutano ule alisubiri nje ya ukumbi pale Star Light hadi usiku wa manane ndipo alipoingizwa mkutanoni kwa kazi hiyo tu kisha akatoka nje kupisha mkutano uendelee. Siku zile kwa shida ya fedha CUF wakifanya mikutano yao usiku na asubuhi wajumbe wanapanda mabasi kurejea makwao. Naamini Maalim hakujuta kwa kuletewa vijana badala ya wazee wetu kwani kila alipopita mikoani na vijijini alipokelewa na vijana hawa. Baadae zilitufikia taarifa kuwa wapinzani wetu walishangazwa ni lini tulijenga mtandao ule wa nchi nzima na bila shaka swali hili pia lilikuwa kichwani kwa Maalim. Iko siku In Shaallah tutaelezana ni vipi hawa vijana walipatikana na tulikuwa na hadi anuani zao pamoja na nyumba na mtaa...ni hadithi ya kusisimua sana... ![]()
Vijana wanachama wa NEMA mstari wa mwisho wapili kutoka kushoto waliosimama
ni Shaaban Mzuzuri, mwandishi, Salehe Yongo (marehemu) na Adam Juma.
Tulikuwa sisi ndiyo waasisi wa ''mtandao.''
Mtandao wa Kikwete, Lowassa, Rostam wa 2005 uliomtia madarakani Jakawa Kikwete ulikuja miaka kumi baada yetu ila tofauti ilikuwa moja tu. Sisi ni watu masikini ya Mungu hatukuwa na fedha kilichokuwa kikitusukuma ni mapenzi ya nchi yetu na ari ya kupigania usawa na haki kwa kila mwananchi bila ya ubaguzi.
|
Mwandishi akiwa IDM Mzumbe akikitangaza kitabu cha Abdul Sykes 1999
Uchaguzi. wa mwaka wa 1995 ulitufunza mengi na kilipotoka kitabu changu, ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924- 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika,'' kitabu kilifungua mlango mwingine wa kuwafikia vijana wa Kiislam wasomi. Kitabu kilifungua historia mpya haijapatapo kuandikwa popote na kubwa zaidi ya yote mchango wa Waislam katika uhuru wa Tanganyika..Vijana walipatwa na butwaa kusoma kuwa TANU haikuasisiwa kama walivyokuwa wakifundishwa katika historia na Nyerere bali na marehemu Abdulwahid Sykes. Historia waliokuwa vijana wakisomeshwa toka shule ya msingi hadi chuo kikuu ikaporomoka kwa kasi ya ajabu. Harakati hizi mpya za chama kingine nje ya CCM ikapata wafuasi wapya.

Sasa likazuka tabaka lau kama ni dogo la wasomi vijana wa Kiislam ambao kwa yale waliyoyasoma katika kitabu kile wakahisi wao na wazee wao ni jamii iliyodhulumiwa kwani haiwezekani Waislam wapiganie uhuru kwa kiasi kile kisha mwishowe uhuru wenyewe usiwanufaishe kitu. Hapa ndipo nilipogundua kosa nililafanya la kuandika kitabu kwa Kiingereza badala ya Kiswahili na hivyo kukosa wasomaji wengi.
Kwa upande wa vijana wa Kizanzibari nao walishangazwa kusikia kuwa Sheikh Hassan bin Amir Mzanzibari alipigania uhuru wa Tanganyika bega kwa bega na Julius Nyerere na akina Abdul Sykes. Mwandishi akaalikwa Chuo Kikuu Cha Zanzibar akatoe mada kuhusu Sheikh Hassan bin Amir. CUF haikuwa na tabu kwa vijana wasomi Zanzibar. Lile lilikuwa jimbo lao salama. Shida ilikuwa katika vyuo vikuu Bara. Katika uchaguzi wa 1995 tulimsindikiza Prof. Lipumba aliyekuwa mgombea urais wa Bara kwa tiketi ya CUF. Hivi vyuo vikuu Bara ni ngome ya Ukristo kwani Waislam hawajaweza kufikia hata asilimia kumi. Wanafunzi waliokuja kumsikiliza Prof. Lipumba walikuja zaidi katika kumkejeli kuliko kumsikiliza kama mgombea urais na mchumi bingwa. Lakini uchaguzi wa mwaka wa 2000 umma uliojitokeza katika mikutano ya Prof. Lipumba ulitisha CCM. Hasa mapokezi ambayo hayajapata kuonekana siku alipotoka Mwanza kuja Dar es Salaam wakati wa uchaguzi.
Sheikh Hassan bim Amir akipeana mkono na Julius Nyerere katika sherehe ya kuweka jiwe la msingi la Chuo Kikuu Cha Waislam 1968 |
Kwa upande wa vijana wa Kizanzibari nao walishangazwa kusikia kuwa Sheikh Hassan bin Amir Mzanzibari alipigania uhuru wa Tanganyika bega kwa bega na Julius Nyerere na akina Abdul Sykes. Mwandishi akaalikwa Chuo Kikuu Cha Zanzibar akatoe mada kuhusu Sheikh Hassan bin Amir. CUF haikuwa na tabu kwa vijana wasomi Zanzibar. Lile lilikuwa jimbo lao salama. Shida ilikuwa katika vyuo vikuu Bara. Katika uchaguzi wa 1995 tulimsindikiza Prof. Lipumba aliyekuwa mgombea urais wa Bara kwa tiketi ya CUF. Hivi vyuo vikuu Bara ni ngome ya Ukristo kwani Waislam hawajaweza kufikia hata asilimia kumi. Wanafunzi waliokuja kumsikiliza Prof. Lipumba walikuja zaidi katika kumkejeli kuliko kumsikiliza kama mgombea urais na mchumi bingwa. Lakini uchaguzi wa mwaka wa 2000 umma uliojitokeza katika mikutano ya Prof. Lipumba ulitisha CCM. Hasa mapokezi ambayo hayajapata kuonekana siku alipotoka Mwanza kuja Dar es Salaam wakati wa uchaguzi.
