- Mimi ni mkazi wa Kilindi kundi la Wahuni waliojiita waislam liliweka kambi kijiji cha Lwande (kambi hiyo iliitwa Kandahari) kambi nyingine iliwekwa kijiji cha Kimamba kata ya Negero ilijulikana kama Madina. Jamaa hao waliungana na baadhi ya wenyeji na kuweka kambi hizo. Wakiwa maeneo hayo walianza kuwabagua Wanajamii kwa kujitenga na maeneo ya kuchota maji, kususia nyama zilizochinjwa na Waislam wengine, kupiga watu wanao pita ktk eneo hilo kwa pikipiki zilizofungwa spika, kupiga watu wasiotaka kwenda msikitini hata watu hao ni Wakristo, kutotambua Serikali za maeneo hayo kwa madai kuwa ni makafiri. Kukata mikono wezi, kwa ujumla walikuwa na mfumo wao wa utawala, mtu ambae si wa imani yao alikuwa haruhusiwi kuingia ndani ya kambi hizo. Wananchi wamelalamika mara nyingi kuhusu vikundi hivyo serikalini tangu mwaka 2008 lkn Serikali ilikuwa inajibu kuwa tunafuatilia.
Baadae ikafikia wakati hata watoa taarifa serikalini wakitambuliwa na watu hao walikuwa wanakamatwa na kupelekwa kambini kuteswa na inasemekana vijana wawili waliuawa huko ndani. Hali hiyo iliwafanya wanavijiji kuwa waooga kutoa taarifa na wakabaki wakinungunika kila kukicha.
Kibaya zaidi makundi hayo yalijijenga na kuwa maeneo ya mafunzo kwa vijana kwa ajili ya kupelekwa Somalia kujiunga na Alshabab, Vijana walikuwa wanachukuliwa vijiji vya Kwastemba, Bokwa, Mafisa, Gombero, Kikunde na maeneo kadhaa ya mikoa mingine. Mafunzo yalikuwa yanaratibiwa na kuongozwa na mtu aliejulikana Kama Master.
Kuna habari nyingi na za hatari kuhusu jamaa hawa na kama wangeachwa kwa miaka 3 mbele Boko haram nyingine ingeibuka Tanzania. Nampongeza sana Mkuu wa Mkoa kwa hatua ya kupambana na jamaa hawa na sisi wananchi wa maeneo haya hatutakubali watu hao warudi tena ktk maeneo yetu, kila anae rudi tunamshughulikia kwa sababu tumeoona mahakama zinataka kutuzingua.
Pia tunaishukuru Serikali ya wilaya kwani baadhi ya viongozi wa makundi hayo wanaendelea kukamatwa mmoja amekamatwa milima ya Korogwe na mwingine Arusha juzi. Mtendaji wetu wa kata aliitwa kwenda kuwatambua na ametuambia baada ya kuhojiwa na polisi aliekamatwa Arusha amekiri kuwa yeye ndie aliekuwa anachukua Vijana waliopata mafunzo na kuwapeleka Kenya kujiunga na Alshabab wa Kenya.
Watanzania wenzangu mnaoitakia mema nchi yetu tuwalaani jamaa hawa kwani ni hatari kwa nchi yetu. Nawapongeza sana viongozi wetu Dc Kilindi na Kamati yake ya ulinzi pamoja na Rc Tanga wote ni waislam wasingekubali kuwaondoa waislam wenzao lkn ni baada ya kujiridhisha kuwa hawa jamaa si waislam bali wanatumia mgongo wa dini kufanya maovu.
Kama hayo ndiyo makosa yao mbona hawakukamatwa kwa kuvunja
sheria za nchi na kushitakiwa mahakamani?
Unataka kuniaminisha kuwa serikali hii inafanya maamuzi yake kwa
dhana na hisia siyo ''hard facts?''
Yaani hawa ndugu zangu Waislam wa Kilindi wangeachiwa wawe
Waislam zaidi baada ya miaka mitatu wangehatarisha usalama wa
Handeni?
Huu ndiyo ushahidi mnaowapelekea Wamarekani kuwa mnawasaidia
kupambana na Al Shabab?
Huu ndiyo ushahidi mnaoogopa kujanao mahakamani?
Mnadhani Waislam hatuna akili?
Sheria gani inasema mtuakimkata mtu mkono nk. nk. avamiwe na
kuuliwa, msikiti na nyumba yake vichomwe moto?
Hiyo lugha ya ''kambi'' ''wahuni,'' si yako ikiwa wewe kweli ni Muislam
Naijua inapotoka.
Haiwezekani mtu anaeswali sala tano na kahifadhi Qur'an akawa muhuni.
Wahuni tunawajua na wengi ni kinyume cha hao unaoishinao hapo
wasiokunywa pombe, wasiozini, wanaoitika adhana ikipigwa nk. nk.
Wenye sifa hizi hawawezi kuwa wahuni.
Allah kawasifia katika Qur'an ikiwa wewe ni Muislam hilo utalijua.
Ingia soma Ibadu Rahman...ikiwa kweli wewe ni Muislam.
Hiyo lugha ya wewe kutaka kujinasibisha na Uislam imenidhihirishia
undani wako kwani Muislam hawi kama ulivyojidhihirisha.
Muislam Allah kasema ''Ruhamahu baina hum.'' Hicho sikioni kwako.
Nachokiona ni chuki na uongo unaotumiwa na maadui wa Uislam.
Inaelekwea wewe mgeni katika mambo haya.
Hujui namna ''mfumo,'' unavyofanyakazi.
Hivi wewe ulitegemea ''Operesheni Kilindi,'' iongozwe na Wakristo?
Kila mchezo una sheria zake.
Jitulize ujifunze utaelewa ndugu yangu lakini ikiwa kwa hakika wewe
ni Muislam.
Ukitaka kujua bongo za hao Waislam ulowataja na mfano wa hao
zinavyofanyakazi msome Malcolm X (Malik Shabaz) anavyoeleza
fikra za watumwa katika mashamba ya Wazungu kule ''Deep South,''
walivyokuwa wanatazamana.
Yule mtumwa anaefanyakazi za ndani kwenye nyumba ya ''Master,''
alikuwa anajibidiisha sana kujitofautisha na mtumwa mwenzake
anaetumika shambani.
Mtumwa wa ndani kila siku alikuwa anatafuta nafasi ya kujionyesha
kuwa yeye ni tofauti na nduguye anaelima shamba ili ''Master'' ampende.
Lakini ukweli unabaki pale pale wote kwenye macho ya Master ni
watumwa.
Akiamua anawauza wakati wowote.
Mimi si mtumwa wa yoyote yule mimi ni mtumwa wa Allah Subhana Wataala.
Sijipendekezi kwa yoyote ila kwa Allah
Simuogopi yoyote ila Allah.
Ndiyo maana unaona sijajificha nyuma ya jina bandia.
Nasema ukweli na niko tayari kuukubali ukweli pale utakapodhihiri
na laiti ndugu zangu wa Kilindi wangelikuwa ni magaidi wamekutwa na
silaha mimi ningeliwashutumu bila hofu kwa kuwa wanakwenda kinyume
na Uislam na mafunzo ya Allah na Mtume wake SAW.
Sote tunataka salama ya nchi yetu na tuwaachie vijukuu nchi nzuri
yenye utangamano baina ya Waislam na Wakrsto.
''Marijani,''
Nadhani ushajua unazungumza na nani.Last edited by Mohamed Said; Today at 11:17.
Re: Sakata la Kilindi na mauaji ya kijiji cha Madina, Handeni: Kupotea (kuuliwa) kwa Rajab Omari Mta
Marijani hayo usemayo ni uongo. Kama hayo ndiyo makosa yao mbona hawakukamatwa kwa kuvunja sheria za nchi na kushitakiwa mahakamani? Sheria gani inasema mtu akimkata mtu mkono nk. nk. avamiwe na kuuliwa, msikiti na nyumba yake vichomwe moto? Hiyo lugha ya kambi si yako naijua inapotoka. Hiyo lugha ya wewe kutaka kujinasibisha na Uislam imenidhihirishia undani wako kwani Muislam hawi kama ulivyojidhihirisha. Muislam Allah kasema ruhamahu baina hum. Hicho sikioni kwako. Nachokiona ni chuki na uongo unaotumiwa na maadui wa Uislam.
Hatutaki mambo ya Somalia au Nigeria hapa...hata wewe pia wakukamate,sijui umefanyiwa nini ktk utoto au ujana wako kinachokufanya ujisikie unaonewa kila siku.
Nilikuuliza maswali hapo juu hujayajibu...mabomu kanisani Arusha, kuchomwa moto makanisa Z'bar na mbagala ingekuwa misikiti ingekuwaje?
Badilisha mtazamo wako,hata kama kuna makosa yaliwahi kutokea nyuma...samehe na usahau tujenge taifa letu.
TANGU NIZALIWE SIJAWAHI KUPEWA FURSA YEYOTE KWA SABABU YA UKRISTO WANGU AU KUONA MTU AKINYIMWA FURSA YEYOTE KWA SABABU YA UISLAMU WAKE, NA NIMEZALIWA TANDIKA NA KUISHI NA JAMII KUBWA YA WAISLAMU KATIKA MAISHA YANGU...NA NDUGU ZANGU WA DAMU WENGI NI WAISLAMU.
Tuesday, 20 May 2014
KUTOKA JAMII FORUMS: Re: Sakata la Kilindi na mauaji ya kijiji cha Madina, Handeni: Kupotea (kuuliwa) kwa Rajab Omari Mtana
Re: Sakata la Kilindi na mauaji ya kijiji cha Madina, Handeni: Kupotea (kuuliwa) kwa Rajab Omari Mta
About Mohamed Said Historia, Siasa na Maendeleo Tanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment