Thursday 18 September 2014

HIJJA 1435/2014

Marehemu Sheikh Nurdin Hussein
Abdallah Jabir Muasisi wa Tanzania Haj Trust Akizungumza na Dr. Ziddy (hayuko kwenye picha) kuhusu historia ya
safari za Hijja Tanzania. Picha ya Chini inamuonyesha Kushoto Kewnda Kulia: Nassor Masoud, Dr. Ziddy, Mohamed Said, Maalim Miraj, na Abdallah Mohamed  Wakiwa Tanga Wakifanya Mahojiano na Maalim Miraji wa Shamsiyya Kuhusu Historia ya Hijja. Utafiti Huu Umedhaminiwa na Serikali ya
Saudi Arabia (King Abdulaziz Foundation)  na nia ni Kuandika Encyclopedia ya Hijja Duniani.




Shariff Mohamed Yahya akiwa katika Msikiti wa Barabara ya 10 Tanga akimweleza Dr. Ziddy 
historia ya babu yake mkuu (babu wa baba yake) Sheikh Mwinyimatano 
Hanzuani El Kindy aliyekwenda kuhiji Makka mwaka 1916 akitokea Tanga.
Wakati ule Saudi Arabia iilikuwa chini ya Ottoman Empire. 
 
 
Kushoto Sheikh Mohamed Bin Sheikh Suleiman Mbwana wa Zahrau, Tanga akiwa na Dr. Ziddy na Wasaidizi Watafiti 
Abdallah Mohamed (Kushoto) na Nassor Masoud (Kulia) 
Picha ya Chini Dr. Ziddy Akiwa Katika Msikti Mkongwe wa  Kilwa Wakati wa Utafiti wa Historia ya
Hijja Tanzania.


Historia ya safari ya Hijja katika Tanzania kuanzia miaka ya 1970 baada ya kuundwa kwa BAKWATA imekukuwa historia iliyogubikwa na matatizo makubwa. Sababu ya matatizo haya ni kushindwa kwa BAKWATA kumudu kuweka mipango mizuri ya kuwezesha Waislam kuifanya ibada hii. Kubwa katika matatizo ilikuwa ni kwanza ukiritimba na pili kushindwa kwa BAKWATA kuwa na watu wenye uwezo wa kuendesha mambo. Ilipofika utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi Waislam walilifikisha tatizo hili serikalini na serikali ya Rais Mwinyi haikuona tabu yoyote kutoa fursa kwa Waislam kujiweka pamoja na kuweka mipango ya kusafirisha Waislam kufanya safari ya Hijja. Mwaka 1991 Waislam kutoka taasisi na misikiti mbalimbali walikutana chini ya uongozi wa Abdallah Jabir na wakaunda Kamati ya Hijja ambayo kazi yake kubwa ilikuwa kuhudumia mahujaji. Kamati hii ya Hijja ilikusanya madhehebu zote na ilianza vyema. Matatizo yote ambayo kwa miaka mingi ilikuwa imewakumba Waislam ilifikia kikomo. Mwaka wa 1992 Tanzania Muslim Hajj Trust ikaanzishwa na ikapata tasjila Mwenyekiti akiwa Sheikh Nurdin Hussein na Katibu Abdalah Jabir. Kwa miaka mingi safari ya Hijja ikawa iko chini ya taasisi tatu, BAKWATA, Tanzania Muslim Hajj Trust na Zanzibar ikiwasilishwa na Wakfu na Mali ya  Amana. .Kadri miaka ilivyozidi kupita vikundi vipya vimepata tasjila ya kuhudumia mahujaji hadi kufikia vikundi 32 na hii imesaidia sana kurahisisha ibada ya Hijja.

Baadhi ya Mahujaji Watarajiwa Wakiswali Sala ya Maghrib Uwanja wa Ndege
wa Mwalimu Nyerere tarehe 17 September 2014 Kabla ya Safari ya Kwenda Makka.

Picha ya Chini wanawake mahujaji watarajiwa wakipumzika kusubiri kupanda ndege.







Picha Hii Imepigwa Moshi Katika Siku ya Eid Baada ya Sala ya Eid Iliyosaliwa Katika Uwanja wa Wazi



Rais Jakaya Mrisho Kikwete Akisalimiana na Waumini  Baada ya Sala ya Eid El Haj Msikiti wa Maamur 2013

HAFLA YA KUUAGANA NA MAHUJUAJI ILIYOTAYARISHWA NA TANZANIA MUSLIM HAJ TRUST
22 SEPTEMBER 2014/27 MFUNGO PILI 1435






Mwandishi Akimkabidhi Kitabu cha Maisha ya Abdulwahid Sykes Mgeni Rasmi Katika Hafla ya Kuagana na Mahujaji  Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Sheikh Ali Hassan Mwinyi


 Kushoto Kwenda Kulia: Shaukat Jaffer , Sheikh Saleh Issa Miskry, Sheikh Ali Hassan Mwinyi, 
Sheikh Mohamed Ismail, Sheikh Mahmoud Bin Sheikh Nurdin Hussein

Mahujaji Wasafiri Kuelekea Makka
23 September 2014/28 Mfungo Pili 1435
 



 
 

 


No comments: