Saturday, 24 January 2015

KLEIST SYKES (1894 - 1949) KATIKA DICTIONARY OF AFRICAN BIOGRAPHY (DAB) OXFORD UNIVERSITY PRESS, NEW YORK

Jengo Hili la African Asociation Lilijengwa kwa Kujitolea Kiongozi Akiwa Kleist Sykes 
Hapa Ndipo Palipokuja Kuzaliwa TANU Mwaka 1954

Msomaji nakuwekea hapa vipande kutoka Dictionary of African Biography (DAB) ambao ni mkusanyo kwa njia ya maandishi historia ya Waafrika walioacha alama katika maendeleo ya bara hili. 

Huu ulikuwa mradi wa Oxford University Press (OUP) na Chuo Cha Harvard na ulichukua miaka kadhaa kukamilika. 

Nilikuwa mmoja wa waandishi waliotakiwa kuwaandika baadhi ya Watanzania na Watanganyika waliofanya makubwa katika historia ya nchi yao. Mradi huu ulikuwa chini ya Prof. Emmanuel K. Akyeampong wa Harvard na ulikusanya wanahistoria 500 kutoka Afrika na kwengineko.

Nilimshauri Prof. Akyeampong akate baadhi ya majina aliyoniletea ya Watanzania kwa kuwa kwa hakika hawakuwa na mchango wowote wa maana isipokuwa labda baadhi walipata kuwa na vyeo katika serikali uhuru ulipopatikana mwaka wa 1961.  Nilifanya hivi kwa makusudi kabisa kwa kujua kuwa waliokuwa madarakani hawakutaka hata kidogo historia ya kweli ya waliopogania uhuru wa Tanganyika ifahamike na kuthaminiwa. Hii sasa ikawa nafasi yangu ambayo lau kwa uchache ningeliweza kuiweka sawa historia ya kweli ya Tanganyika.

Mimi nilisahau kabisa kuhusu kazi hii na hata ilipochapwa mwaka 2011 ilinichukua miaka minne kuja kukumbuka na kuanza kufuatilia nini ilikuwa hatima ya ule mradi na hapo ndipo nilipoona hii Dictionary of African Biography katika mtandao.

OUP wametoa volume  sita za kazi hii mwaka 2011. 

Volume hizi sita zinauzwa USD 1300 na vilevile zinapatikana kwenye mtandao kwa ''subscribers.'' Nimeletewa kutoka School of African Studies, London ukurasa ulio na makala niliyoandika kuhusu maisha ya Kleist Sykes (1894 - 1949) nami nimeona itakuwa vyema kama nitaweka hapa vipande vipande ili wasomaji wasome kwa faida ya kuhifadhi kumbukumbu za wazee wetu.

Labda msomaji utataka kujua kwa nini nilichagua kuandika maisha ya Kleist Sykes katika Dictionary of African Biography.

Nimemchagua Kleist Sykes kwa sababu hizi kubwa:
  1. Kwanza alikuwa ndiye katibu muasisi wa African Asociation mwaka 1929 na muasisi wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika 1933 akiwa katibu vilevile na kwa jinsi siasa za kiloloni zilivyokuwa wakati ule za ''wagawe uwatawale,'' yeye aliunganisha vyama hivi katika uongozi mmoja lau kama Al Jamiatul Islamiyya kilikuwa chama cha Waislam na wakati huo huo akaweza kuweka misingi ya kuwashirikisha Wakristo katika kupigania haki za Mwafrika wa Tanganyika katika African Association.
  2. Pili Kleist alifungua mlango wa Waislam wawe na shule zao wenyewe ili kukabiliana na shule za Wamishionari ambazo zilikuwa zikiwabatiza watoto wa Kiislam katika shule zao na hili liliwafanya wazazi wa Kiiislam  kusita kuwapeleka watoto wao shule.
  3. Tatu katika kutimiza hili alianzisha shule ya Kiislam - Al Jamiatul Islamiyya Muslim School ambayo ilisomesha masomo ya kisekula na Qur'an. Inasemekana ilikuwa ndoto ya Kleist kuona Qur'an inasomeshwa kwanye madarasa juu ya madawati na wanafunzi wamekaa katika viti kama shule badala ya zile madras za asili ambazo watoto wanakaa chini katika majamvi. Nia yake ikiwa kuwa katika shule mtoto atapata yote mawili - elimu ya dini yake na masomo ya kisekula. Ndoto hii ya Kleist sasa si ndoto tena kwani shule za Kiislam nyingi zimeanzishwa nchini pote miaka mingi baada ya yeye kutangulia mbele ya haki zikisomesha Qur'an na masomo ya kisekula kwenye darasa moja na mwalimu akiwa kasimama mbele ya ubao.
  4. Jambo la nne ni lile la kuuweka wazi mlango wa TANU kwa Wakristo ambao wakati wa vuguvugu la kuanzisha African Association mwaka 1929 serikali iliwatisha wasijiunge na chama hicho. Hii inatokana na yeye kuwa na akina Cecil Matola, Raikes Kusi na Rawson Watts katika uongozi wa African Association na kwa njia hii kujenga msingi wa umoja na ushirikiano kwa Waafrika wote bila kujali dini zao. TANU ilipokuja asisiwa na wanae Abdulwahid na Ally wazalendo wengine mwaka 1954 hali ilikuwa haijabadilika lakini uongozi wa Waislam ndani ya TANU uliweka mkakati maalum wa kuhakikisha kuwa TANU haivurugwi na hisia za Uislam kiasi cha kuwaweka pembeni ndugu zao Wakristo.
Hii ndiyo sababu ikawezekana Nyerere kuchaguliwa kuongoza TAA mwaka 1953 na TANU ilipokuja asisiwa mwaka 1954 watoto wake wawili Abdulwahid na Ally wakiwa kati ya waasisi 17 kutoka sehemu mbalimbali za Tanganyika haikuwa tabu kwake yeye kukabidhiwa jukumu la kuwaunganisha Waafrika chini ya bendera moja ya kudai uhuru. Itoshe tu safari ya kwanza ya TANU kujitangaza nje ya Dar es Salaam Nyerere aliifanya 1954 Morogoro akifuatana na Zuberi Mtemvu na nyingine ilikuwa 1955 Lindi akifuatana na Rajab Diwani na Ali Mwinyi Tambwe Katibu wa Al Jamiatul Islamiyya.

Hizi ndizo sababu nne zilizonipelekea kuandika maisha ya Klesit Sykes katika Dictionary of African Biography.

Zuberi Mtemvu Kama Alivyokuwa 1962
Picha Hii Ilipigwa Nyumbani kwa Abbas Sykes 
Shaaban Robert Street

Kushoto Abbas Kleist Sykes na Abbas  Zuberi Mtemvu 
Abbas Mtemvu Alipewa Jina Hili kwa Heshima ya Abbas Sykes

Abbas Sykes Wakati Akiwa Balozi Kulia ni Salim Ahmed Salim na Kushoto ni Bhoke Munanka

Utangulizi
Japhet Kirilo na Earle Seaton wameandika kitabu, ‘’The Meru Land Case,’’ kuhusu mgogoro wa ardhi ya Wameru ambayo ardhi yao ilichukuliwa na Wazungu bila fidia. Mimi nimekieleza kisa hiki kufuatana na jinsi Abdulwahid Sykes akiwa kiongozi wa TAA alivyokishughulikia akishirikiana na Earle Seaton na Japhet Kirilo kwa nia ya kuongeza ufahamu wa mkasa huu. Naweka hapo chini kipande kidogo kutoka kitabu cha maisha ya Abdul Sykes:
1951
Baada ya Dr Kyaruzi kuhamishiwa Nzega nafasi ya rais ikawa wazi. Abdulwahid akakaimu nafasi hiyo sasa akiwa katibu na kaimu rais wa TAA. Mgogoro wa ardhi ya Wameru ulikuwa umekwishaanza lakini bado haujalipuka kuwa suala lililowahusu Watanganyika wote. Umoja wa Mataifa ulipotuma ujumbe wake wa pili kuzuru Tanganyika mwaka wa 1950, Wameru waliwasilisha rasmi malalamiko yao kwa ujumbe huo. Abdulwahid aliwaomba wajumbe wa Baraza la Kutunga Sheria washirikiane na TAA katika kutatua baadhi ya matatizo yanayokabili jamii ya Waafrika. Abdulwahid alifadhaishwa na wajumbe Waafrika katika Baraza la Kutunga Sheria pale waliposhindwa kuipinga Wilson Report ambayo ilipendekeza kuondolewa kwa wananchi wa Meru kutoka kwenye ardhi yao. Katika barua aliyoiandikia Meru Citizenís Union, Abdulwahid, kwa niaba ya makao makuu ya TAA, aliwahakikishia watu wa Meru kuwa tatizo lao llilikuwa tatizo la Watanganyika wote.

Abdulwahid aliamua kutumia mgogoro wa ardhi ya Wameru kuwaunganisha Watanganyika wote dhidi ya serikali ya kikoloni. Uamuzi wa serikali juu ya mapendekezo ya TAA kwa Constitutional Development Committee ulikuwa bado umo akilini mwake. Alitambua kwamba uamuzi wa Gavana ulikuwa ni mpango wa muda mrefu wa kuwadhalilisha Waafrika katika utumwa wa daima. Abdulwahid sasa akiwa na ghera kubwa alianza kufanya kazi ya kuwahamasisha watu wa Tanganyika chini ya vuguvugu la kuunganisha umma dhidi ya utawala wa Waingereza. Abdulwahid aliwasiliana na Earle Seaton mjini Moshi kutaka ushauri wa kisheria juu ya tatizo la Meru. Seaton alikuja Dar es Salaam na kukutana na Abdulwahid na uongozi wa TAA. Ilikubaliwa na pande zote mbili kuwa makao makuu ya TAA, Meru Citizenís Union ikiongozwa na Japhet Kirilo na Seaton lazima waunganishe shughuli zao katika kesi hiyo na kwa pamoja watume rufaa yao kwenye Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa huko New York. Kwa sasa uongozi wa chama cha TAA ulitambua kwamba nusura yao ilitegemea uwezo wao wa kudhibiti na kushawishi matukio na maamuzi ndani ya Baraza la Kutunga Sheria.  Ili kuweza kufanya hayo shinikizo lilitakiwa kuwekwa katika Baraza la Udhamini huko New York, nchini Amerika na siyo katika Ofisi ya Makoloni pale London Uingereza.

Tawi la chama cha TAA la Tabora lilichukua changamoto hiyo kwa kupitia juhudi za Kandoro aliyeuona mgogoro wa ardhi ya Wameru kama jukumu lake binafsi. Kandoro aliitisha mkutano wa matawi ya TAA ya Mwanza, Kigoma na Tabora kujadili suala hilo. Mwanza iliwakilishwa na Bhoke Munanka, Mzee Mkama Mlaji na Mohamed Kihaka Kitenge; kutoka Kigoma mjumbe aliyekuja alikuwa Jumanne Mawimbi na Tabora iliwakilishwa na Sheikh Kinana, Kandoro na George Magembe kama rais wa TAA tawi la Tabora.  Mkutano wa Tabora uliahidi mshikamano wa pamoja na watu wa Meru katika mapambano dhidi ya walowezi.

Mgogoro wa ardhi ya Meru ni wa pekee katika historia ya Tanganyika. Ilikuwa kupitia katika mgogoro huo ndiyo Mtanganyika, Japhet Kirilo, akifuatana na Earle Seaton kama mkalimani na mshauri wa sheria, kwa mara ya kwanza alizungumza mbele ya Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa huko New York, na kuonyesha udhalimu wa ukoloni. Mnamo November, 1952 Kirilo alizungumza mbele ya Kamati ya Nne ya Baraza Kuu. Watu wa Tanganyika sasa walikuwa wanayachukua mapambano yao toka mipaka yao hadi kwenye kumbi za Umoja wa Mataifa, mjini New York kutafuta haki. Lakini Kirilo alirudi mikono mitupu. Rufaa ya mgogoro wa ardhi ya Wameru ilitupiliwa mbali. Kirilo aliuhakikishia Umoja wa Mataifa kuwa watu wake kamwe hawatachukua silaha kuikomboa ardhi yao kama Wakikuyu wa Kenya walivyojaribu kufanya. Kwa kweli hapakuwa na sababu ya kutoa kauli hii, kwa kuwa uhakikisho wa kutokuwepo mapambano uliwafanya walowezi washushe pumzi na kujiona wako salama. Tangu mwanzo wa mgogoro wazalendo nchini Kenya kama Fred Kubai na Kung'u Karumba walikuwa wakitoa ushauri kwa Meru Citizenís Union kwa kuwa wao walikuwa na ujuzi zaidi wa matatizo ya walowezi kuliko watu wa Tanganyika.

Kwa mtazamo wa juu juu mtu anaweza kudhani kuwa Abdulwahid alikuwa akipata kipigo kutoka sehemu zote alizojaribu kuipenyeza TAA kutoka mwaka wa 1948 katika enzi za chama cha makuli, kufikia marekebisho ya katiba hadi kumalizikia kwa mgogoro wa ardhi ya Wameru. Kushindwa huku si kwa sababu TAA ilikuwa ina viongozi dhaifu au ilikuwa haiuingwi mkono na umma. TAA ilikuwa haifanikiwa katika madai yake kwa sababu serikali ya kikoloni ilikuwa imeamua kutosikiliza lolote kuhusu matatizo ya Waafrika. Matokeo ya hali hii ilimfanya Abdulwahid aamue kuwa njia iliyobakia ya Tanganyika kujitoa katika makucha ya Waingereza ni kuuandaa umma wa Tanganyika chini ya chama cha siasa. Mara tu baada ya Kirilo kurejea kutoka New York, mpango wa kuanzisha chama cha siasa cha kushirikisha umma wote ulianza.

Uongozi wa TAA Makao Makuu ulianza kampeni ya nchi nzima kuueleza umma matokeo ya safari ya Kirilo kwenye Umoja wa Mataifa kuhusu mgogoro wa ardhi ya Wameru na vilevile kuchangisha fedha za kupeleka msafara mwingine katika Umoja wa Mataifa kuueleza umoja huo kuwa Tanganyika ilikuwa chini ya udhamini na Watanganyika walikuwa sasa na haki ya kudai uhuru wao. Kamati ya TAA ya watu watatu iliyowajumuisha Kandoro, Kirilo na Abbas Sykes iliundwa kwa ajili hiyo. Ally Sykes akiwa mweka hazina msaidizi wa TAA aliombwa ampelekee Kirilo hawala ya posta Usa River kama nauli ya kumwezesha kusafiri hadi Dodoma kujiunga na ile kamati ya watu watatu. Kulikuwa hakuna huduma ya fedha katika posta ya Usa River na fedha zile zilikaa hapo kwa muda bila ya kuchukuliwa hadi hapo zilipopelekwa posta ya Arusha mjini ambako Kirilo alizichukua.Kuanzia tarehe 26 Septemba, 1953 kwa takriban mwezi mmoja ile kamati ilitembelea na kuhutubia mikutano ya hadhara, ikikusanya fedha Dodoma, Mwanza, Bukoba, Ukerewe, Tarime, Musoma na Shinyanga. Rais wa chama cha TAA, kanda ya ziwa, Paul Bomani aliipokea ile kamati ya watu watatu na kuhutubia mikutano pamoja nao katika jimbo lote. Bomani aliwaambia wanachama wa TAA na wananchi wote mjini Mwanza kuhusu umuhimu wa kuchanga fedha kwa kwa kusudio hilo.

Kushoto Waliokaa: Kleist Sykes, na Abbas Kleist
Nyuma Waliosimama Ally Kleist na Abdul Kleist

Kushoto Kwenda Kulia: Dossa Aziz, Julius Nyerere, Abdulwahid Sykes na Lawi Sijaona
Picha Hii Ilipigwa Arnauotoglo Kwenye Dhifa ya Kumuaga Nyerere Akienda Safari ya Pili
UNO mwaka 1957

Photo
Kaburi la Kleist Sykes Makaburi ya Kisutu Dar es Salaam

No comments: