JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM (T)
BARAZA
KUU
Assalam Alaykum
Warahamtul llah Wabarakaatuh
TAARIFA
NA MWALIKO WA KONGAMANO LA WAZI LA WAISLAM WOTE LITAKALOFANYIKA KATIKA KIWANJA
CHA NURUL YAKINI MKABALA NA MWEMBE YANGA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 22/02/2015 SAA
NANE ADHUHUR HADI SAA KUMI NA MOJA JIONI.
Taafadhali husika na
kichwa cha habari hapo juu.
Ndugu katika iman tunachukua
fursa hii kukutaarifu na kukuomba uwatangazie Waislam wote kuhudhuria katika
Kongamano tajwa hapo juu. Mambo muhimu na mazito yanayohusu Uislamu na Waislam
nchini yatazungumzwa na kutoa muelekeo wa Ummah katika kipindi hiki nyeti na
kigumu kwa mustaqabali wa Ummah.
Miongoni mwa mambo muhimu
yatakayozungumzwa ni pamoja na:
1) Mahakama ya Kadhi: Tokea Ilani ya CCM
mwaka 2005, Rasimu ya Warioba, Bunge la
Katiba na leo
hii Muswada wa Mahakama ya Kadhi. “Hii danadana na Hadaa dhidi ya Waislam”.
2) Mashekh wetu kuteswa na kudhalilishwa
mahabusu (kisiasa) bila ya kosa la kisheria.
3) Propaganda za “Ugaidi” dhidi ya Uislam na
Waislam nchini.
4) Katiba Pendekezwa iliyokataa Mahakama ya
Kadhi na kura za maoni mwezi wa nne.
5) Mustakabali wa Ummah kuelekea Uchaguzi Mkuu
Octoba 2015
Haya ni miongoni yale
yatayozungumzwa na kupata mustaqabali wa pamoja wa Ummah ili kuweza kutoka kuwa
watu wa daraja la tatu ndani ya ardhi yetu, ambayo wazee wetu walipambana
kuwaondoa wakoloni kwa ajili ya vizazi vyao.
Tunataraji utawatangazie Waislam
na kuwasisitiza kuhudhuria katika Kongamano hili la kihistoria kila baada ya
swala ya faradhi, na ikiwezekana kupata usafiri wa pamoja.
WABILLAH TAWFIQ
KAIMU KATIBU
………………….
JUMUIYA NA TAASISI (T)
No comments:
Post a Comment