Tuesday 26 May 2015

KUTOKA JF: HAMZA KIBWANA MWAPACHU, ABDULWAHID KLEIST SYKES NA JULIUS KAMBARAGE NYERERE


Quote By Yericko Nyerere View Post
Mzee ukipewa heshima ni jukumu lako kuilinda,

Umepoteza hilo, umebaki kuilazimisha hesha.

Hoja yamsingi niliyokujibu hapo nikuwa Abdul Sykes hakuwahi "kuchaguliwa" kuwa rais wa Chama chochote duniani tangu azaliwe mpaka kufariki kwake.
Yericko,
Ikiwa unataka tumjadili Abdul Sykes na nafasi ya urais katika TAA sawa.

Abdul Sykes hakupata kuchaguliwa kuwa rais wa TAA na wala hili sikutegemea
kuwa ni jambo la kutaka kujadiliwa.

Baba yake Abdul Mzee Kleist Sykes hakupata kuwa rais wa African Association.

Hakuchaguliwa kuwa rais kwa sababu nafasi iliyomwenea ni ukatibu kwa sababu
ya kipaji chake cha kuoganaizi watu na mambo.

Pili hakuwa rais kwa sababu ya kipaji alichokuwanacho katika uandishi
na lugha.

Abdul Sykes kama baba yake na yeye alikuwa na kipaji kikubwa katika kuoganaizi
na alikuwa na ulimi mzuri sana wa kuzungumza Kiingereza.

Licha ya hayo alikuwa anajua kupiga taipu na kuandika hati mkato.
Hizi ndizo sifa zilizomfanya yeye siku zote achaguliwe nafasi ya ukatibu kuanzia
Dar es Salaam Dockworkers Union 1947 hadi TAA 1950.

Kleist akizungumza Kiingereza na Kijerumani.

                                                                                                                                           


#602   Report Post    
 By Mohamed Said View Post
Yericko,
Ikiwa unataka tumjadili Abdul Sykes na nafasi ya urais katika TAA sawa.

Abdul Sykes hakupata kuchaguliwa kuwa rais wa TAA na wala hili sikutegemea
kuwa ni jambo la kutaka kujadiliwa.

Baba yake Abdul Mzee Kleist Sykes hakupata kuwa rais wa African Associatio.

Hakuchaguliwa kuwa rais kwa sababu nafasi iliyomwenea ni ukatibu kwa sababu
ya kipaji chake cha kuoganaizi watu na mambo.

Pili hakuwa rais kwa sababu ya kipaji alichokuwanacho katika uandishi
na lugha.

Abdul Sykes kama baba yake na yeye alikuwa na kipaji kikubwa katika kuoganaizi
na alikuwa na ulimi mzuri sana wa kuzunguza Kiingereza.

Licha ya hayo alikuwa anajua kupiga taipu na kuandika hati mkato.
Hizi ndizo sifa zilizomfanya yeye siku zote achaguliwe nafasi ya ukatibu kuanzia
Dar es Salaam Dockworkers Union 1947 hadi TAA 1950.

Kleist akizungumza Kiingereza na Kijerumani.
Kwamuono wako unaamini hizo ndio sababu za yeye kutokuchaguliwa kuwa rais?

Hahaahaa mkuu hayo yalikuwa sehemu ya masharti ya fomu za uchaguzi?

Hebu tulia jibu hoja mkuu usiweke hisia zako. Klest Sykes mwaka 27 aligombea uchaguzi wa kwanza wa rais wa AA akishindani na Mwalim Cecil Motola, akaanguka na kwenda kuwa katibu,

mwaka 48 mtoto wa Klest ambaye ndiye Abdul Sykes naye licha ya kuongoza mapinduzi ya ngumi, katika vikumbo vya kuwania kuupata urais wa AA alijikuta akiangukia pua mbele ya Vedasto Kyaruzi ambae alikuja kuongoza mabadiliko ya chama kutoka AA hadi TAA aliyoikuta Julius Nyerere.

                                                                                                                                     


  1. Yericko, 
    Huijui historia ya TANU.

    TAA haikuasisiwa 1927 bali 1929 na wakati ule nafasi za uongozi
    hazigombewi.

    Msome Iliffe "Modern Tanzanians" Kleist Sykes the Townsman
    (Daisy Sykes) (1973) historia nzima ya AA imeandikwa mle.

    Nimekuwekea "note" ya JV kwa Edmund akieleza mkakati wa
    Nansio kati ya Hamza Mwapachu na Abdul Sykes vipi wabadili
    uongozi 1953.

    Kuhusu uchaguzi wa 1950 uliowatia madarakani Abdul na Kyaruzi
    msome Listowel (1965) "The Making of Tanganyika," utajifunza
    mengi na utajua kuwa juhudi kubwa ya kuwaingiza vijana hawa
    madarakani ilitoka kwa Schneider Abdillah Plantan na huyu
    alikuwa mmoja wa baba zake Abdul na aliyekuwa ametolewa
    madarakani alikuwa Mwl. Thomas Plantan kaka yake Schneider
    kwa hiyo ni baba yake mkubwa Abdul.

    Hebu soma hiki kipande na mtafute Dr. Kyaruzi katika uongozi wa
    TAA mwaka 1953 kabla TANU haijaasisiwa:

    Hayo hapo chini ni kutoka kitabu changu: "The Life and Times of
    Abdulwahid Sykes..." (1998):

    In June, TAA headquarters announced its executive committee with
    J.K. Nyerere, President; Abdulwahid Sykes, Vice-President; J.P.
    Kasella
     Bantu, General Secretary; Alexander M. Tobias and
    Waziri Dossa Aziz, Joint Minuting Secretary; John Rupia, Treasurer
    and Ally K. Sykes as Assistant Treasurer.

    Committee members were Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani,
    Tewa Said, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo

    and Patrick Aoko.[1]

    Yuko Kyaruzi hapo?

    Sasa ikiwa viongozi ndiyo hao 1953 mwaka mmoja kabla ya TANU
    kuasisiwa Kyaruzi katoa mchango kutoka chama kipi na katika
    mwakaupi?

    Mwisho tunarudi palepale tulipoanzia na mimi kupata sababu ya
    kuandika kitabu ambacho kwa miaka sasa kila uchao tunakizungumza
    hapa jamvini.

    Ikiwa historia ya uhuru wa Tanganyika ndiyo hii na historia ya TANU
    chama cha uhuru ndiyo hii...

    Imekuwaje historia ya TANU ikaja kuandikwa na ikawaacha nje wengi
    wa wazalendo hawa?

    Inawezekana Yericko Nyerere akaja na jibu.

    Ningependa kumweleza Yericko kuwa Abdul alikuwa Kaimu
    Rais TAA baada ya Dr. Kyaruzi kupewa uhamisho kwenda Kingolwira
    (ingawa Yericko anasema uhamisho ulikuwa Sengerema) na alikaimu
    nafasi hiyo toka 1951 - 1953.

    Baada ya uchaguzi wa 1953 uliomuingiza Nyerere madarakani kama
    rais wa TAA Abdul akawa makamu wa rais.

    Unapoandika historia ya TANU na ukaanza na Nyerere na kumtoa nje
    Abdul Sykes hapo mtafiti anakuwa kajipalia makaa.

    Historia hiyo haiwezi kusimama kwani mtafiti anakuwa si kama kajipunja
    yeye mwenyewe bali pia kaipunja historia ya uhuru wa Tanganyika.

    Jambo la kushangaza ni kuwa Dr. Kyaruzi alipatapo kueleza kuhusu
    historia yake ya siasa na akasema kuwa ilikuwa yeye ndiye aliyemwachia
    Nyerere chama.

    Katika makala nzima hakupata kumtaja Abdul Sykes wala uchaguzi wa
    1950 wala hakumtaja Schneider Plantan.

    Ilikuwa yeye Kyaruzi na Nyerere peke yao katika historia ya TANU.
    Hizi ndizo historia zetu.

    Wanamajlis,
    Anaetaka kumjua vizuri Dr. Kyaruzi aingie hapa:
    http://www.mohammedsaid.com/2013/12/...i-daktari.html







    [1] Tanganyika Standard, 19 th June 1953.
    Last edited by Mohamed Said; 21st May 2015 at 13:23.
  2. #604   Report Post    
    Yericko Nyerere's Avatar
    JF Senior Expert MemberArray
    Join Date : 22nd December 2010
    Location : Kigamboni, DSM
    Posts : 13,490
    Rep Power : 182646780









    Likes Received
    10340









    Likes Given
    479

    Default

    Quote 
  3. #605   Report Post    
    Mohamed Said's Avatar
    JF Senior Expert MemberArray
    Join Date : 2nd November 2008
    Posts : 6,697
    Rep Power : 340070









    Likes Received
    5773









    Likes Given
    277

    Default Re: Siri ya Malkia Elizabeth wa Usikochi (UK), Kanisa Katoliki, Nyerere na Uhuru wa Tanganyika

    Yericko,
    Kuna watu wamejaaliwa uelewa wa juu kabisa na kuna wengine
    uelewa wa chini.

    Narejea na kuongeza maelezo ili yule mzito wa akili na yeye apate
    kuelimika.

    Ndiyo kila nitoapo darsa huunganisha na darsa lingine kumuongezea
    msomaji maarifa.

    Ndipo hapo nimeweka kiungo cha Dr. Kyaruzi nikukumbushe kuwa
    uhamisho wake haukuwa Sengerema bali Kingolwira kisha Nzega.

    Nimekuwekea na gazeti la Tanganyika Standard la 19 June 1953
    kukuonyesha kuwa Abdul Sykes alikuwa Makamu wa Rais TAA chini
    ya Nyerere yote haya kuwaonyesha watu kuwa naijua vizuri sana
    historia ya TANU kwa ushahidi wa rejea za uhakika.

    Yote kukuhakikishia kuwa haikamiliki si historia ya TANU au ile ya
    Nyerere mwenyewe katika uuuru wa Tanganyika bila kumtaja Abdul
    Sykes
    .

    Kwa hakika napokea salaam nyingi sana za shukurani ya kuiokoa
    historia ya uhuru wa Tanganyika.

    Huna lolote la kusema kuhusu taarifa ya JV kwa Edmund kuhusu
    uchaguzi wa TAA 1953 uliomuingiza Nyerere madarakani?
    Last edited by Mohamed Said; Yesterday at 18:06.

  4.    Report Post    
    Yericko Nyerere's Avatar
    JF Senior Expert MemberArray
    Join Date : 22nd December 2010
    Location : Kigamboni, DSM
    Posts : 13,490
    Rep Power : 182646780









    Likes Received
    10340









    Likes Given
    479

    Default

    Quote By Mohamed Said View Post
    Yericko,
    Kuna watu wamejaaliwa uelewa wa juu kabisa na kuna wengine
    uelewa wa chini.

    Narejea na kuongeza maelezo ili yule mzito wa akili na yeye apate
    kuelimika.

    Ndiyo kila nitoapo darsa huunganisha na darsa lingine kumuongezea
    msomaji maarifa.

    Ndipo hapo nimeweka kiungo cha Dr. Kyaruzi nikukumbushe kuwa
    uhamisho wake haukuwa Sengerema bali Kingolwira kisha Nzega.

    Nimekuwekea na gazeti la Tanganyika Standard la 19 June 1953
    kukuonyesha kuwa Abdul Sykes alikuwa Makamu wa Rais TAA chini
    ya Nyerere yote haya kuwaonyesha watu kuwa naijua vizuri sana
    historia ya TANU kwa ushahidi wa rejea za uhakika.

    Yote kukuhakikishia kuwa haikamiliki si historia ya TANU au ile ya
    Nyerere mwenyewe katika uuuru wa Tanganyika bila kumtaja Abdul
    Sykes
    .

    Kwa hakika napokea salaam nyingi sana za shukurani ya kuiokoa
    historia ya uhuru wa Tanganyika.

    Huna lolote la kusema kuhusu taarifa ya JV kwa Edmund kuhusu
    uchaguzi wa TAA 1953 uliomuingiza Nyerere madarakani?
    Sijaona unakosoa wala kufundisha mkuu, ama kwamba ni Kingolwira na sio Sengerema?

    Kwamba Abdul Sykes alikuwa makamu wa Julius baada ya kuangushwa kwenye uchaguzi wa Anautoglo hapo mwaka hamsini na tatu hilo sio hoja. Hoja ya msingi nikuwa ukoo wa Sykes haukupata "kuchaguliwa" kwa nafasi ya urais ama uenyekiti wa chama chochote cha siasa nchini Tanganyika tangu utoke kwao Uzulu.
  5. #607   Report Post    
    Mohamed Said's Avatar
    JF Senior Expert MemberArray
    Join Date : 2nd November 2008
    Posts : 6,697
    Rep Power : 340070









    Likes Received
    5773









    Likes Given
    277

    Default Re: Siri ya Malkia Elizabeth wa Usikochi (UK), Kanisa Katoliki, Nyerere na Uhuru wa Tanganyika

    Yericko, 
    Hilo la Kleist kutokuwa rais wa African Association bali katibu na la
    mwanawe kutokuwa rais wa Tanganyika African Association (TAA)
    sidhani kama linabadilisha historia ya mchango wa Abdul na baba
    yake katika uhuru wa Tanganyika.

    Muhimu ni kuwa maisha ya Kleist yamehifadhiwa kwenye kitabu:
    Modern Tanzanians (1973)na kwenye Dictionary of African Biography
    (DAB) (2011) na maisha ya mwanae ndiyo kitabu nimeandika na ni
    mashuhuri kwenye vyuo vingi Ulaya na Marekani toka kilipochapwa
    London 1998.

    Kitabu hiki sasa kinakwenda toleo la nne Kiswahili na toleo la tatu
    Kiingereza.

    Sasa kwa nini Abdul hakuwa rais wa TAA 1950 nimejaribu kueleza
    na nikakuambia kuwa kutokea 1951 hadi 1953 alikuwa katibu na
    akakaimu na nafasi ya rais wa TAA na chama kilipata mafanikio
    makubwa sana.

    Tunaweza kuanzia hapa safari yetu nikakurejesha hadi Nansio mwaka
    1953 kwa Hamza Kibwana Mwapachu, Abdulwahid alipokwenda
    kumtaka ushauri kuhusu Nyerere.

    Sasa Yericko hebu jiulize kwa nini Abdul na Ali Mwinyi Tambwe 
    walifunga safari kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kisha wakavuka
    Lake Victoria hadi Nansio kwenda kupata kauli ya Hamza Mwapachu
    ilhali Hamza Mwapachu hana nafasi yoyote ya uongozi katika TAA?

    Nakuuliza swali hili kwa kuwa nakuona wewe umeshughulishwa
    sana na nafasi ya urais katika TAA ingawa nimekueleza kuwa kwa
    nyakati zile mtu hagombei uongozi kama ilivyo siku hizi.

    Wakati ule katika dimbwi la ukoloni uongozi wa chama cha siasa
    ilikuwa ni kubeba majukumu mazito sana na ya hatari.

    Kiongozi alitazamwa kwanza katika kukisaidia chama kwa fedha
    kutoka mfukoni kwake achilia hiyo hatari ya kufungwa jela.

    Abdul Sykes alikuwa kijana wa kujiweza sana kifedha na hakika
    alitoa fedha nyingi sana mfukoni kwake kuijenga TAA na baadae
    TANU.

    Turudi kwa Hamza Mwapachu.

    Hamza Mwapachu ana historia ya pekee katika historia ya ukombozi
    wa Tanganyika.

    Dr. Kyaruzi alipatapo kusema kumwambia mmoja wa watoto wa
    Mwapachu kuwa, "Kama si mipango aliyoweka baba yako na Abdul
    Sykes 
    Tanganyika isingepeta uhuru mwaka wa 1961."

    Jiulize kwa nini Nyerere alipojiuzulu ualimu alikwenda kuishi nyumbani
    kwa Abdu Sykes wakati ule Abdul hana nafasi yoyote ya uongozi
    katika TANU?

    Yericko yapo mengi sana katika historia ya nchi yetu wewe huyajui.
    Tuagane na Hamza Mwapachu.

    Baada ya uhuru Hamza alikuwa Dar es Salaam lakini siku hizo
    alikuwa mgonjwa.

    Wakati ule Bunge likikutana Karimjee Hall.

    Hamza alikuwa akija pale Bungeni akiwa kwenye "wheelchair,"
    akifuatilia mijadala yote mle ndani.

    Na Hamza hakuwa mbunge.
    Nyerere akataka kumteua awe balozi Uingereza.

    Hamza akakataa nafasi ile na Nyerere badala yake akamteua
    Kassanga Tumbo.

    Hebu hangaisha ubongo wako Yericko jiulize kwa nini Hamza
    alikataa uteuzi ule?

    Naamini umefadika na darsa hii.
    Kejeli hapa si pake.

    Jitahidi uwe na adabu lau ya kuvalia nguo.
    Usicheze na Abdul Sykes Mungu alimjaalia uwezo mkubwa sana.

    Hiyo 1953 akihangaika na TAA na kuunda TANU tayari mfukoni ana
    barua ya kujiunga na Princeton University, New Jersey.
    Last edited by Mohamed Said; Today at 14:28.

No comments: