Ali Sykes alikuwa na marafiki
wengi Zanzibar.Kati ya hao wawili ambao wamo kwenye picha hii, No 5 Abdillahi
Masoud Smuts aliekaa na No 16 Himid Msoma aliesimama na ambae ni baba yangu
walikuwa wakisikilizana sana na mzee Ali Sykes.
Huyu Abdillahi alianza urafiki na
A.Sykes kule Burma wakati wa Vita Kuu ya Pili.Vile vile anafanana na kina Sykes
na Machado kwa vile alikuwa na jina la Kizungu kwasababu mzazi wake alijiunga na
jeshi la General Smuts wakati wa vita kati ya Waingereza na Makaburu(Boers) kule
South Africa.Alipewa jina la Smuts na Waingereza kwa kutambua ushujaa wake kwani
pia alipewa cheo kikubwa jeshini na mara kadha aliongoza paredi
za askari huku akiwa kapanda farasi.
za askari huku akiwa kapanda farasi.
Wote wawili baba yangu na baba Smuts
walikuwa pia wakicheza hockey na mzee Ali kila pale timu za D'salaam
zilipocheza dhidi ya Zbar wakati wa msimu wa Sports.

No comments:
Post a Comment