Sunday, 18 October 2015

MBUNGE MTARAJIWA WA NEWALA: MWALIMU JAFFAR MNEKE KIJANA MDOGO MSOMI WA MASUALA YA DIPLOMASIA



Jaffar Mneke: Mwalimu, Mwanadiplomasia mwenye majibu ya kero za Newala. Ni kijana ambaye anaamini matatizo yote ya Newala yanatokana na uongozi mbovu. Aja na Safari ya Mabadiliko ya kweli kuelekea ujenzi wa Newala mpya, Newala yenye neema, akiwa na mwarobaini wa kero za wananchi.


Na Mwandishi Wetu
KATIKA mataifa mengi duniani linapokuja suala la ukombozi wa jamiii kisiasa na kiuchumi.  Mmara nyingi historia inaonesha ukweli uliowazi kabisa kwamba vijana wamekuwa chachu muhimu ya mabadiliko hayo.
Iliichukua Tanzania wakati huo ikiitwa Tanganyika hadi kupata ujio wa kijana wakati huo mwalimu wa Sekondari ya Pugu, Julius Kambarage Nyerere, kuweza kuanzisha Safari yake ya Mabadiliko.
 Iliwachukua wananchi wa Afrika Kusini kumpata kijana mwanasheria wakati huo Nelson Mandela kuanzisha vuguvugu la kweli la kupambana na hatimaye kuushinda ubaguzi wa rangi.
‘’Kama kuna wakati jimbo la Newala mkoani Mtwara nchini Tanzania linapita katika fursa ya aina hiyo basi ni sasa,’’ anasema mwanasiasa kijana na mwenye damu ya mageuzi Jaffar Mneke mgombea ubunge aliyeidhinishwa na muungano wa upinzani (Ukawa) kupitia chama cha wananchi (CUF).
Anasema wana Newala mwaka huu wana machaguo mawili rahisi sana., Mosi ni kukubali kuendelea na kero, kudhulumiwa, kudharauliwa na kutaabika vilevile na kupewa sababu zile zile za udanganyifu au kukubali kuungana naye katika kile anachokiita Safari ya Mabadiliko ya kweli ya ujenzi wa Newala mpya. (Samane)!
“Nimeamua kuanzisha Ssafari hii ikiwa ni baada ya kuzaliwa nayaona matatizo ya Newala. Nakua nayaona matatizo yale yale. Nasoma na kumaliza Newala imebaki na matatizo yale yale.
“Tafakuri yangu baada ya kipindi kirefu ni kwamba matatizo waliyonayo wana Newala, wana Mtwara, wana Kusini si mapya wala mageni. Yalikuwepo sehemu nyinginezo nchini na duniani lakini yakatatuliwa kupitia viongozi makini wenye uzalendo wa dhati na watu wao.’’
“Kwa nini Newala imebaki na kero zake?” aAnahoji Bw. Mneke na kisha anajibu: “Niliwaambia wananchi wakati wa kura za maoni na wakanielewa na nitaendelea kulisemea hili wakati wa kampeni kwamba-Newala sio kisiwa ingeweza kutatua changamoto hizi na kisha kupambana na mpya, lakini Bbahati mbaya tatizo kubwa limekuwa ni kukosa uongozi wenye ubunifu na uzalendo.”

Matatizo ya Newala
Mneke anasema kwa kuwa amekua, amesoma na sasa anaishi akiyaona matatizo ya Newala,  ameamua kuyaainisha ili kuomba nguvu ya wananchi ifikapo Oktoba mwaka huu aweze kuungana nao katika Ssafari ya ujenzi wa Newala mpya kwa kuyabadili matatizo hayo kuwa fursa za maendeleo. Akiyachambua matatizo hayo, Mneke anasema:
Mosi, anaona kuwa tatizo kubwa la kwanza kwa wananchi wa Newala ni kukosekana viongozi makini, wabunifu na wenye dhamira ya dhati ya kusimamia maslahi ya wana Newala.
“Bila uongozi makini Newala haiwezi kusonga mbele. Ni kama vile bila uongozi makini wa Mwalimu Nyerere tusingekuwa huru leo. Ni kama vile bila uongozi makini wa Mahatma Gandhi India isingekuwa huru na isingeachana na ubaguzi wa rangi na pia bila uongozi makini wa Nelson Mandela Afrika Kusini ingebaki chini ya uMakaburu milele.’’
“Nitachotaka hapa wananchi wajue na waniamini ni kwamba matatizo waliyonayo yanahitaji uongozi makini wenye uzalendo wa dhati. Hili ndilo suluhisho la kwanza wanalopaswa kuwa nalo. Uongozi makini pekee ni asilimia 70 ya kutatua matatizo yao. Waungane nami na Ukawa wakati ukifika katika Oparesheni hii ya Safari ya Ukombozi na  ujenzi wa Newala mpya ili tuondokane na tatizo hili,” anasema msomi huyu kijana mwanadiplomasia akionesha kujiamini.
Kero ya pili, kwa mujibu wa Mneke ni kwamba ni mkusanyiko wa mambo yanayotokana na kero ya kwanza hapo juu ambapo imechangia kudorora kwa huduma muhimu kama vile za maji safi na salama,wakati wilaya hiyo imebarikiwa kwa kuwa na vyanzo vingi vikubwa vya maji kama vile mto Ruvuma, chanzo cha maji Makondeko na chanzo cha maji Mitema. uUbovu wa huduma za afya, ukosefu wa soko la uhakika la korosho na mazao mengine kama vile njugu na mbaazi, elimu na uhaba wa umeme ni kati ya matatzo yanayoikabili Newala.
“Ukiyaangalia matatizo haya ya pili kimsingi ni matokeo ya tatizo la kwanza kwa sehemu kubwa. Kama una mbunge na viongozi wengine wa Serikali wasioweza kuisukuma Serikali iboreshe haya au wasioweza kushirikiana na wadau wa sekta binafsi kutatua mambo hayo basi kero ni uongozi mbovu.
“Nikipewa fursa nitawaunganisha viongozi wote tuwe na msimamo na nguvu ya pamoja ya kudai haki za wana Newala kuondolewa kero hizi. Nitashirikiana pia na asasi za kijamii za ndani na nje ya nchi kutatua kero hizi. Ni kero za kiuongozi tu. Ndio maana nasema na kuwaomba ndugu zangu Wana Newala wake kwa waume pamoja na vijana wenzangu  waungane nami katika Safari ya Ukombozi na ujenzi wa Newala mpya,” anasisitiza Bw. Mneke.
Akizungumzia suala la uongozi kama moja ya chanzo kikubwa cha umaskini wa wana Newala, Mneke anasema kwa sasa yeye na wataalamu wake wanaainisha mkakati mpana wa kitaalamu wa kuondoa kero za jimbo hilo kwa kutumia mawazo makuu.
“Kwa sasa sitaainisha mikakati yangu. Najua wapo wapinzani wangu ambao hawana sera wataiba na kuanza kuimba na mwishowe watashindwa kuzitekeleza na kuwaumiza zaidi wananchi. Wananchi wa Newala wajue tu kuwa matatizo yao yamelimbikizwa kutokana na uongozi mbovu. Nawaletea uongozi makini. Nawaletea mabadiliko ya kiutendaji,” anasema.
Anasema bila kutaja undani wa mikakati anayoianisha hivi sasa, kwa ujumla akiwa mwanadiplomasia pia atatumia taaluma yake hiyo kuzungumza na wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi ili nao wawe sehemu ya safari ya mabadiliko ya Newala kwa faida ya wana Newala.
“Ili kuipa nchi yetu uhuru ambao leo tunaufurahia Mwalimu Nyerere alikusanya nguvu ya Watanzania na wasio wWatanzania, wWaislamu na wasio wWaislamu, Waafrika na wasio Waafrika; hatimaye leo Tanzania iko huru. Umoja ni ushindi.
“Nitakapoanza kampeni nitawaeleza wana Newala kwa namna gani nami kupitia Safari ya Mabadiliko ya Newala nitatumia mbinu za medani za kidiplomasia kuwaondoa hapa walipo,” anasema Mneke.
Alikotokea
Mneke ni kiongozi makini, jasiri na mtetezi wa wanyonge na anayechanganyika vyema na watu wa dini zote hasa kutokana na sehemu kubwa ya maisha yake kusoma katika shule na/au vyuo vya kKiislamu na vya kKikristo.
“Kuishi na watu wa dini zote mbili kuu hapa nchini kumenipa maadili ya uongozi, ari ya kuchangamana na watu na zaidi kufahamu umuhimu wa umoja katika kupigania maslahi ya kijamii,” anakumbuka akieleza historia yake ya kitaaluma.
Mneke amepata elimu ya msingi katika shule ya msingi Nakahako Newala Mtwara, elimu ya Sekondari katika shule ya Seminari  Mhumbu mkoani Shinyanga  na kidato cha tano na sita katika Sekondari ya Kiislamu Mudio mkoani Kilimanjaro. Na alipata elimu ya juu katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana (St. John University of Tanzania) ambako alitahasusi katika masuala ya Elimu na kutunukiwa shahada ya kwanza ya Uwalimu.
“Katika Chuo cha St. John tumejifunza uongozi na saikolojia ya kutatua matatizo ya sekta ya elimu na kijamii kwa ujumla na pamoja na elimu ya Kiroho (Christian Wisdom) ambapo nikiwa na watu wa rangi, dini na asili tofauti nilijifunza pia kuwa maendeleo ni umoja.,” Kkatika chuo hiki kauli mbiu ilikuwa ni “Kusoma na kutumikia Jamii” “TO LEARN TO SERVE” kauli mbiu hii imenifanya muda wote nihisi kuwa kwa elimu niliyopata nina deni kwa jamii. ambapo anapaswa maisha yake  yote yangu yote anitumikie jamii ili kulipa deni hilo na kubaki salama., “Mneke anasema”.
Alianza kutumia taaluma yake ya elimu kwa kuwafundisha vijana katika shule mbalimbali nchini ikiwemo sekondari ya kKiislam Ilala (Ilala Islamic Secondary School) kama makamu mkuu wa shule. aAlifika mahali akatafakari na kuona auongezee taaluma zaidi ya kidiplomasia ili aweze kuzungumza na dunia kwa umakini anapokuwa katika Safari ya Mabadiliko.

Hivyo kati ya mwaka 2013 na 2014 Mneke alijiunga na Chuo cha Diplomasia kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam na kujipatia sShahada ya Umahiri (Post-Graduate in Management of Foreign Relations) ambako alihitimu kwa kiwango cha mwanadiplomasia wa daraja la kwanza (first class).

“Katika Chuo cha Diplomasia nimejifunza fani za Uongozi, Utawala, Siasa na Mahusiano ya Kimataifa. Nimefahamu kwa nini zipo sehemu duniani maisha ni mazuri na kwinginezo ni taabu. Nimejifunza mbinu za utatuzi wa migogoro na kero za watu kwa vkiwango cha kijamii, kitaifa na kimataifa. Nitawaomba Wana Newala waungane nami katika safari hii, nitatumia ujuzi huo kwa faida yao,” na kuijenga Newala mpya.,’’ ameongeza.

Uzowefu katika Uongozi.

Mneke amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi katika taasisi za kielimu na kijamii kama vile mwenyekiti wa wanafunzi mMkoa wa Shinyanga mwaka 2005-2006, Mwenyekiti wa wanafunzi mMkoa wa Kilimanjaro 2008-2009, Rais wa wanafunzi na vijana wa vyuo na mashule Tanzania kupitia Jumuiya ya wanafunzi na vijana wa kKiislam Tanzania (Tanzania Muslim Students and Youth Association) 2009-2012, Mjumbe wa sShirikisho la vVijana wa vVyuo vVikuu Afrika Mashariki, Mjumbe mMteule wa kKamati mMaalum ya wasomi (task force ) iliyoalikwa na Kamati ya bBunge ya kKatiba, sSheria na uUtawala katika kuchambua na kutoa maoni ya kitaalam katika muswada wa written Law wa mabadiliko ya sheria mbalimbali (Miscellaneous Amendment )(No. 2) Act wa 2014) 2014-2015.

Mneke anazungumza kwa ufasaha lugha tatu za kimataifa za Kiswahili, Kiingereza na Kiarabu akisema hiyo ni fursa nyingine kwake kuwaletea wananchi wa Newala uongozi makini wenye ubunifu na uwezo wa kutafuta na kutumia fursa za maendeleo. kwani anao uwezo wa kuzungumza na wadau wowote wa maendeleo wa hapa nchini na popote duniani na kuwashawishi kuja kuwekeza miradi mbalimbali ya kimaendeleo Newala.

Uwajibikaji katika jamii.

Mwandishi aliweza kuwauliza watu mbalimbali vipi wanaomfahamu Mneke.
Kennedy ambaye alisoma nae na alikuwa kiongozi wake katika cChuo cCha dDiplomasia alimzungumza Mneke kuwa ni kijana makini, jasiri mwenye kupenda kujitolea kwa maslahi ya wengi kwani alikuwa anawahi chuoni mapema kila siku akiwa ametupigia kopi  Madesa na vitini vya kujisomea sote tulimpenda sana kwa moyo wake wa kujitolea kwa kweli Mneke ni Jembe la kazi na ndio maana aliweza kufaulu kwa daraja la kwanza (first class).

Aidha, watu wengi wanamzungumza Mneke kuwa ni kiongozi makini jasiri aliyeweza kusimamia haki za wanafunzi na vijana mashuleni na vyuoni bila ya woga sambamba na kutatua na kusuluhisha migogoro ya wanafunzi na vijana nchini kwa njia mbalimbali kama vile kidiplomasia laini na ngumu(soft and hard diplomacy) ikiwa ni pamoja na kuwalipia ada wanafunzi wanaotoka familia duni kwa kuwatafutia wafadhili. Wengi wanamkumbuka kwa namna alivyoweza kutatua na kusuluhisha mgogoro wa shule ya sekondari Ndanda ambao ulivuma na kutikisa taifa mwaka 2011-2012. Kwa busara na hekima alizotumia katika kutatua mgogoro huo kumepelekea wanafunzi waliobaki shuleni hapo kuishi kwa upendo, kuhurumiana, kuheshimiana na kupendana wao kwa wao pamoja na walimu wao.“Damu yangu inachemka kuiona Newala siku moja nayo ikipaa na kuwa moja ya wilaya bora na za mfano hapa nchini. Sina mengi ya kuwaambia wana Newala kwa sasa bali neno langu la utangulizi kwao ni kuwataka wawe tayari na wajipange kwa kuungana nami katika Safari hii ya Mabadiliko ya kweli na ujenzi wa Newala mpya,” anasisitiza na anamaliza kwa kusema “Newala tuna jambo letu, Mtwara tuna jambo letu, Kusini tuna jambo letu, tumeamua na tunaweza.”

No comments: