Monday, 4 January 2016

KUTOKA JF: AMAN THANI


  1. uyui kwetuJF-Expert Member

    #2
    Today at 4:21 PM
    Joined: Oct 23, 2013
    Messages: 587
     
    Likes Received: 10
     
    Trophy Points: 18
    New
    Inamaana hawa viongozi hawaoni riwaya zako au ni kiburi
     
  2. M

    Mohamed SaidJF-Expert Member

    #3
    7 minutes ago
    Joined: Nov 2, 2008
    Messages: 6,994
     
    Likes Received: 9
     
    Trophy Points: 38

    Uyui Kwetu
    ,
    Hayo maneno niliyoweka hapo si riwaya kwa maana ya hadith za kubuni.
    Wala mimi sifahamiki kama mwandishi wa riwaya.

    Inaelekea wewe ni mgeni hapa Majlis.

    Soma tena na angalia chini utaona ni maneno kutoka kalamu ya Aman Thani
    kutoka kitabu chake, ''Ukweli ni Huu.''

    Aman Than ni Mzanzibari na alikuwa Katibu Mkuu wa Zanzibar Nationalist Party
    (ZNP) baada ya Abdulrahman Babu kujitoa ZNP mwaka wa 1963.

    Aman Thani ni hazina kwa mwanafunzi yeyote wa historia ya Zanzibar na Afrika.

    Ameyaona yote yaliyopita katika siasa za Zanzibar kuanzia 1957 wakati wa kupigania
    uhuru hadi yalipotokea mapinduzi mwaka wa 1964.

    Baada ya mapinduzi Aman Thani aliwekwa kizuizini na baadae kuhukumiwa kifungo
    cha miaka10 jela kazi ngumu Zanzibar kama mfungwa wa siasa.

    Nimejifunza mengi katika nyaraka zake na kumbukumbu nilizoziona na namshukuru
    kwa kunipa ilm ambayo sikupatapo kuwa nayo kabla.

    Sidhani kama viongozi wetu wanakataza watu kufanya utafiti, kujifunza mapya na
    kuandika kwa faida ya jamii.

No comments: