Wednesday 17 February 2016

KUTOKA JF: BR. GR. HASHIM MBITA




JokaKuu,
Hii project mimi nikiijua zaidi ya miaka 15 sasa.
Mtu wa kwanza kunifahamisha alikuwa marehemu Mzee Kanyama Chiume.

Alikuja na ''write up'' yake ofisini kwa marehemu Ally Sykes na mimi nilikuwapo.
Nilikuwa na nakala yake.

Siku zikapita nikasikia kuwa ipo project hii ya sasa na Hashim Mbita anaishughulikia.

Saigon Club kwenye khitma mwaka jana nikasimamishwa tena mbele ya kadamnasi
wakiwemo wakubwa wa nchi hii wastaafu nikapewa jukumu la kuandika ''biography''
ya Hashim Mbita kama nilivyoiandika ya Abdulwahid Sykes.




Khitma Saigon

Leo nilikuwa napita A Novel idea Bookshop ndipo nikaktaafu uta hizo volume za Hashim
Mbita 
SADC Southern African Liberation Struggles.

Ziko volume 9 bei 1.2m.

Kuweka historia kwa kweli ni jukumu la taifa na kuna watu wameajiriwa kwa kazi hii.
Itabidi tuwawekee shiikizo wafanye kazi yao vizuri.






Gwakisa,
Sijui kwa nini umesema ''sijalitendea haki JWTZ'' ilhali mimi nilichofanya hapa
Majlis ni kuweka hii mada na inatoka katika blog yangu:

Mohamed Said: SADC HASHIM MBITA PROJECT: SOUTHERN AFRICAN LIBERATION STRUGGLES

Mimi nimepita A Novel Idea Bookshop Slip Way, Masaki nikakuta hizo volume 9
basi nikaomba ruksa kwa mwenye duka nipige picha akaniruhusu bila shida.

Nilipofika nyumbani nikamuuliza Prof. Google na yeye akanipa hayo yote hapa.
Joka Kuu yeye kalaumu pia kuwa hatuthamini historia yetu.

Ngoja nikupe kisa cha mapenzi ya watu wa Msumbiji kwa Watanzania.
Mwaka wa 1990 mimi na wenzangu tulikwenda Msumbiji kwa ajili ya mafunzo.

Ndege ilotupeleka ni Royal Swazi.

Kwa mastaajabu tukakuta watu kutoka Wizara ya Nchi za Nje ya Msumbiji wako
uwanjani wanatusubiri kutupokea.

Sisi tulikuwa vijana kutoka Bandarini tunakwenda kusoma kozi fupi ya usafirishaji.
Hatukuwa na hadhi yoyote ya kupokelewa kiserikali.

Maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wakawa wanagombana hawataki sisi
tupite Customs kwao wao ni sie Watanzania kuvunjiwa heshima na wao wako pale
kuhakikisha hadhi yetu inalindwa.

Ugomvi mkubwa ukatokea hadi mimi nilipofungua sanduku langu kwa khiyari yangu
na wenzangu wakafatia ndipo ikapatikana salama tukapita kwenda Hotel Cardoso.

Hii ndiyo ilikuwa hadhi yetu kwa hawa ndugu zetu wa Msumbiji.
Sijui leo mambo yakoje.

Kisa kingine nilikwenda kula chakula hoteli ambayo speciality yao ni samaki na beer.
Mimi hilo silijui kuwa hakuna vinywaji baridi hapo.

Kijana mmoja kuona vile akanyanyuka akaacha chakula akenda nje mtaa wa pili na
akarudi na chupa ya Coke akaniwekea mezani.

Akanambia wewe ni ndugu yetu.

Mmemwaga damu zenu kwa ajili ya uhuru wetu sisi na hadi leo ndugu zako wamelala
katika ardhi yetu.

Eduardo Mondlane aliuliwa nyumbani kwake Msasani.

Marehemu Hamza Aziz amenambia kuwa mara kadhaa alikuwa
akimtahadharisha Mondlane kuhusu kufungua barua.

Hamza Aziz na Mondlane walikuwa majirani.

Mwaka 2011 nilialikwa Chuo Kikuu Cha Northwestern University, Chicago kufanya
mhadhara.

Hiki ndicho chuo alichosoma Mondlane na mkewe walifahamiana hapo.

Habari hizo ananieleza mwenyeji wangu Jonathon Glassman tukiwa kwenye
ukumbi ambao picha ya Mondlane imetundikwa pamoja na mapambo ya
vinyago vya Kimakonde kutoka Mozambique.

Katika ukumbi huu wa Mondlane ndipo nilipofanya mhadhara wangu.
Sina zaidi la kuongeza.

[​IMG]




Sooth,
Tatizo la udini halikuanza awamu ya nne.

Tatizo la udini limenza toka enzi ya Tanganyika na unaweza ukaligawa
katika sehemu tofauti.

Udini wakati wa ukoloni mtupu
Udini wakati Tanganyika inapigania uhuru wake, na
Udini baada ya Tanganyika kuwa huru.

Nikimjua vyema marehemu Hashim Mbita na msimamo wake.

Si kumjua tu niliwahi hata kufanya na yeye mjadala mkali tukiwa Madina
Saudi Arabia Hijja ya mwaka wa 1998.

Mjadala wetu ulisikilizwa na takriban Watanzania wote tuliokwenda hija
mwaka ule chini ya Tanzania Muslim Haj Trust.

Suala la udini katika nchi yetu si jepesi.

No comments: