CrocodiletoothJF-Expert Member
NewJe ni nini kitatokea, je uchaguzi huo utakuwa halali?
Endapo wapiga kura watakuwa 1/4, yaani watu 300,000 au 400,000. tu na watu 1mil kupuuzia.SIGNATUREMKWEPA KODIJF-Expert Member
NewTayari uchaguzi huo si halali, hayo mengine ni kujazia nyama tu
SIGNATURE- New
Mfumo wetu wa uchaguzi ni wa simple majority na sio quota system, ambapo the winner takes it all, hata akishinda kwa kura moja!, hivyo hata kama waliojiandikisha kupiga kura ni watu milioni moja, lakini waliojitokeza ni watu watatu, na wawili kati yao wakaichagua CCM, itatangazwa imeshinda katika uchaguzi uliokuwa huru na wa haki na ushindi huo ni ushindi halali! kwa sababu kujiandikisha kupiga kura ni jambo la hiari, na ukiishajiandikisha, kujitokeza kupiga kura pia ni hiyari, hivyo CUF watautumia hiyari yao kihalali kwa kutokujitokeza kupiga kura, na CCM, wataitumia hiyari yao kujitokeza kwa wingi na kujipatia ushindi wa mezani!.
Pasco - New
Pasco material zako zinawapasua kichwa cuf,nahisi yule aliekua mtu wako ameliona hili na amemshauri looser mwenzake na jana wamelegeza kamba
HansssJF-Expert Member
NewMaalim kweli amenyoosha mikono Jana anasema, kuna kikundi kina piga watu, kinachukua vitambulixho vya kupigia kura wakat SERIKALI IPO IMEKAA KIMYA hapa nikajiuliza serikali hiyo ni ipi ambayo yy mwanzoni alishindwa kuitambua na sasa ameitambua rasmi.
GeechieSenior Member
NewKuna watu wanamhujumu Maalim kwa kumshauri vibaya ili aanguke kisiasa halafu kibaki chama kimoja tu chenye nguvu Tanzania .Swala LA kutoitambua serikali halafu unapowaongelea mazombi unauliza serikali inafanya nini kuzuia haya huu ni mfadhaiko Wa kisiasa yani kapwelepweta sasa.Naamini CCM hawatarudi mezani kamwe yeye asuse Hamad Rashid aukwae umakamu hata kama atapata kura kumi.
Pia zanziar kuwa na watu milioni moja na nusu wengine ni under age.Hawajajiandikisha wala hawapigi kura.Pasco ameelezea vizuri huko juu namna mshindi anavyopatikana.Hivyo Maalim bado ana mwezi mzima Wa kusuka au kunyoa.- New
Chaguzi zetu iwe chini ya zec au nec hazitumii mfumo wa percent bali hutumia kwa lugha lahisi wengi wape hata kama ukichaguliwa na watu 5 kati 20 waliojiandikisha utakuwa umeshinda. Ni mfumo ambao si mzuri sana
AveroesJF-Expert Member
New
Waliopiga kura wote ni 503,000+ sasa huyu anaesema kama watu 1.5 million kawasahau watoto wako idadi gani na wakaazi waso na sifa ya kupiga kura wangapi. Asitubbaishe kibano kimewabana wasipige mateke hewani.Mohamed SaidVerified User ✅
New
Unaweza kujiongezea maarifa kwa kusoma kitu kinachoitwa ''sham election.''
Hii ni moja katika masomo ya sayansi ya siasa.
Ukimaliza somo hilo utaelewa kwa nini kwa hali iliyopo Zanzibar hivi sasa huo
uchaguzi utakuwa kichekesho.- There are more posts to display. View them?
Bobwe2JF-Expert Member
NewSIGNATUREkat.phJF-Expert Member
NewHata CUF wakishiriki, wapiga kura huwa ni wachache sana.
Mohamed SaidVerified User ✅
New
Shida kubwa tuliyonayo hapa barzani ni kuwa na wachangiaji ambao
huenda wana nia nzuri ya kutoa fikra zao lakini hawana ujuzi wa somo
wanalochangia.
Tuanze na hili ''chama kimoja chenye nguvu.''
CCM Zanzibar imepoteza nguvu muda mrefu na ndiyo maana unaona
haijaweza kushinda uchaguzi toka chaguzi za vyama vingi zilipoanza
mwaka wa 1995.
CUF katika miaka hiyo 20 imewekeza katika siasa za ushindani na sasa
wana ''election machinery'' inayoweza kuwashinda CCM Zanzibar bila
tabu juu ya vikwazo wanavyowekewa.
Matokeo yake ndiyo haya sasa Dr. Shein na wenzake wanang'ang'ania
madaraka kwa nguvu juu ya kuwa hawakushinda uchaguzi.
Tuje kwa Hamad Rashid.
Huyu wala hastahili hata kuzungumzwa kwa sababu hicho chama chake
ADC katika uchaguzi uliopita hakikupata hata 1% ya kura.
Nadhani unatambua kuwa ili kushiriki katika SUK unahitaji kura asilimia
fulani (sikutajii nataka usome ili ukirudi kuichangia uwe una elimu).
Mwisho kuhusu Mazombie.
Hili si jambo la kufanyia maskhara ni kitu kibaya kinachoweza kuiangamiza
Zanzibar.
Soma hii makala itakupa mwanga wa tatizo la Mazombie:
Mohamed Said: COMPARE AND CONTRAST BETWEEN TON TON MACOUTE IN PAPA DOC's HAITI AND THE ZOMBIES IN ZANZIBAR
Soma makala hizi itakuonyesha kuwa ukifananisha masultani na viongozi wa
mapinduzi masultani walikuwa watawala wema ambao wameondoka bila ya
damu mikononi mwao:
Mohamed Said: MASULTANI WALIPATAPO KUUA, KUWEKA JELA ZA MATESO NA KUFANYA DHULMA NYINGINEZO DHIDI YA WAZANZIBARI?
Mohamed Said: MAZOMBIE ''POLISI SHIRIKISHI'' WANAPOFANANA NA SS ASKARI WATESAJI WA ADOLF HITLER
Geechie,
Inachohitaji CCM Zanzibar ni uongozi mpya wenye fikra za kuwaleta watu pamoja na hili
litaweza tu kufanyika kwa wao kuukubali ukweli kuwa Wazanzibari wamewakataa wakakubali
kushindwa na wakachagua viongozi wapya ambao watakuwa na mvuto kwa Wazanzibari.
Saturday, 13 February 2016
KUTOKA JF: UCHAGUZI WA MAREJEO ZANZIBAR
About Mohamed Said Historia, Siasa na Maendeleo Tanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment