Siku chache zilizopita katika Bunge Waziri Mdogo wa Mambo ya Ndani Mheshimiwa Hamad Masauni alisema kuwa hana taarifa za Mazombie.
Swali hili liliulizwa na Mheshimiwa Ally Saleh Mbunge wa Malindi.
Leo Kamishina wa Polizi Zanzibar anasema Mazombie wanafahamika na ni katika moja mkakati wa wa kutunza amani visiwani.
Mtu unaweza kabisa kuamini kama unachosoma ndiyo hicho kilichoandikwa.
Mazombie sasa ni polisi shirikishi:
''Ni uongo na uzandiki Kamishna wa Polisi Zanzibar kudai hawajawahi kuripotiwa rasmi UHARAMIA unaofanywa na MAZOMBI. CUF kimemuandikia rasmi yeye Kamishna wa Polisi Zanzibar barua kadhaa toka mwaka jana kumueleza juu ya UHARAMIA wa MAZOMBI lakini hakuna hatua zozote alizochukua na katika mkutano mmoja uliofanywa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na mwengine ambao viongozi wa CUF wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu, Mheshimiwa Nassor Ahmed Mazrui, Polisi wakakiri kuwatambua MAZOMBI na kusema ni sehemu ya mikakati yao ya kulinda usalama.''
No comments:
Post a Comment