Utangulizi
Marehemu Mzee Aman Thani
hakuingia kaburini na elimu yake. Kaacha nyuma elimu katika historia ya siasa za
Zanzibar kama hidaya kwa vizazi vijavyo. Kwanza kwa kuandika na kitabu chake
mashuhuri ni ‘’Ukweli ni Huu.’’ Pili, kwa kutoa mihadhara mingi. Katika moja ya
mihadhara yake inayosisimua, kuelimisha na kufikirisha ni huu mhadhara aliotoa
wa maisha ya kinara wa mapinduzi ya Zanzibar, Abdallah Kassim Hanga. Hanga ni
katika historia ya kusikitisha sana katika Mapinduzi ya Zanzibar kiasi kwamba
hata wanamapinduzi wenzake kwa nusu karne walikuwa kimya hakuna aliyependa
kumtaja. Hata katika kusheherekea miaka 50 ya mapinduzi, walipotoa medali za
waliofanikisha mapinduzi yale, jina la Abdallah Kassim Hanga, halikuwako. Naona
fahari kuwakilisha sehemu ya kwanza ya mhadhara wa marehemu Aman Thani mmoja wa
wazalendo waliopigania uhuru wa Zanzibar. Mhadhara huu aliufanya nyumbani kwake
Dubai, Rashidiya.


Abdallah Kassim Hanga alipoletwa Mnazi Mmoja kwenye mkutano wa hadhara aliohutubia
Nyerere na Hanga akafedheheshwa hadharani
No comments:
Post a Comment