Tuesday, 12 April 2016

KIJEMBE KUTOKA JF: SIJAMUADHIMISHA SOKOINE KWA KUWA SI MUISLAM


Moringe Sokoine



Kituko,
Hunijui na hujanisoma na ndiyo maana unakuja na fikra kuwa mimi
hutafiti Waislam tu na kuandika habari zao.

Sokoine mimi nimemwandika kwa kupita tu yumo kwenye mswada
wangu, ''Christian Hegemony and the Rise of Muslim Militancy in
Tanzania.

Kwa sasa hii ni ''mimeo,'' inapatikana Zentrum Moderner Orient (ZMO)
Berlin, Germany.

Nimewaandika Wakristo wengi katika historia ya uhuru wa Tanganyika
pamoja na Nyerere.

Hakuna mwandishi aliyemueleza Nyerere kwa undani wakati anaanza
siasa Dar es Salaam 1953 kama mimi.
Ingia hapa:
  1. Mohamed Said: LAMECK BUGOHE MUASISI WA TANU 1954 KAFARIKI NA KUZIKWA KIMYA KIMYA
  2. Mohamed Said: KUTOKA JF: HISTORIA YA TANU - DK. VEDASTO KYARUZI, KASELLA BANTU NA JULIUS NYERERE
  3. Mohamed Said: KUTOKA JF: DK. WBK MWANJISI, CHIEF DAVID KIDAHA MAKWAIA NA JK NYERERE
[​IMG]
Chief David Kidaha Makwaia

Kituko,

Nadhani link hizo hapo juu zinakutosha kwa leo.

Mimi nimefanya juhudi kubwa ili wengine waliokuwa katika siasa
za kupigania uhuru watajwe.

Nakufahamisha kuwa hiyo hapo juu ndiyo picha ya kwanza baada
ya uhuru ya Chief Kidaha kuwekwa hadharani na nimejitahidi pia
kueleza habari zake.

Mwisho napenda nikifahamishe kuwa mimi nilipata kumuandikia barua
Sokoine wakati wa ile kampeni ya kila mtu afanyekazi.

Kulikuwa na taarifa kuwa walimu wa madras za vibarazani hawatambuliki
kuwa wanafanyakazi inayotambulika.

Nilimwandikia barua kumfahamisha kuwa hivyo ndivyo elimu ya Kiislam
inavyotolewa na tumekuwa tukisomeshana namna hii toka azal.

Sokoine hakunijibu yeye binafsi bali barua yangu ilijibiwa na mtu mwingine
katika CCM ni miaka mingi simkumbuki jina lake.

Alinambia niende ofisini kwao Lumumba kwa maelezo.

Nikamjibu kuwa hili si la mimi kupata maelezo kwake bali hili ni la Waislam
yeye atoe hayo maelezo Waislam wasikie.

Huu ndiyo ukawa mwisho wa majibizano yetu.
Hii ndiyo kumbukumbu yangu na marehemu Sokoine.

Mwalimu Nyerere na Mama Maria wakiomboleza kifo cha Sokoine

No comments: