Utangulizi
Watu hutaka kujua Maalim Seif Ijumaa hii atasali msikiti gani. Inapopatikana fununu tu kuwa Ijumaa hii atasali msikiti fulani basi dalili utaziona mapema kwa watu kufurika kwenda kusali huko na kuacha ile misikiti yao ya kawaida.
Hii ni dalili njema ya mapenzi ya wananchi kwa kiongozi wao.
Mohamed Said
Maalim Seif bado awataka vijana kuwa watulivu.
Maalim Seif Sharif Hamad ambaye anaaminika kuwa ndiye mshindi wa uchaguzi mkuu halali wa Zanzibar, uliofanyika tarehe 28 Oktoba mwaka jana leo tarehe 15/04/2016 amesali sala ya ijumaa katika Msikiti wa Msumbiji.
Maalim Seif baada ya swala aliombwa na imamu asimame aongee na waumini wa dini hiyo ya Kiislam, hivyo kwa heshima kubwa aliyonayo kwa waumini wa dini hiyo na Wazanzibari kwa ujumla alikubali kufanya hivyo.
Katika mazungumzo yake Maalim Seif kwanza alimsifu khatib kwa nasaha alizotoa kwa waumini, kisha aliweza kuelezea kwamba afya yake iko vizuri sana na kumshukuru Allah.
Maalim Seif Pia hakusita kuelelezea jinsi watu baadhi ya watu wachache wanavomlaumu kwa kuwawazuiya katika kutafta haki haki yao ya uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka jana ambao Jecha Salum Jecha alitangaza kufuta mnamo tarehe 28/10/2015, baada ya kuonekana dhahiri kwamba Chama cha Mapinduzi kinaeleka kushindwa katika uchaguzi huo.
Maalim Seif alisema "Ninajua kwamba vijana walikuwa tayari kupambana kwa hali yoyote ili kudai haki yao, lakini nasema mwisho wamapambano mwishowe ni msiba"
"Nyinyi nyote ni mashahidi duniani kulivokuwa hakuna amani nchi nyingi kunamachafuko, mimi ni kiongozi mkubwa wa kisiasa kamwe sitoweza kuitia nchi yangu kwenye matatizo na machafuko makubwa, hivyo bado nasema watu wavute subra, haki itapatikana Inshallah, naam naamini itapatikana haki haipotei na itakuja juu tu haizami" alimalizia Maalim Seif.
No comments:
Post a Comment