Mwandishi akifanya mahojiano na Salim Rashid Katibu wa Kwanza wa Baraza la Mapinduzi 1964 TV Imaan Kipindi: Walioacha Alama Katika Historia |
[4/2, 6:12 PM] Mohamed Said: Kwa taarifa tu.
Salim Rashid hakupatapo kuwa kinara wa mapinduzi.
Kinara wa mapinduzi alikuwa Abdallah Kassim Hanga.
Hanga ndiye aliyekuwa kiongozi msaada mkubwa akipewa na Oscar Kambona kwa niaba ya serikali ya Tanganyika.
Kambona ndiye aliyeweka kambi ya askari mamluki wa Kimakonde wakata mkonge Sakura na Kipumbwi, Tanga.
Wengine katika mpango huu wa mapinduzi walikuwa Victor Mkello, Jumanne Abdallah, Ali Mwinyi Tambwe na Mohamed Omari Mkwawa. Mzanzibari aliyepata kujua njama hizi alikuwa Jimmy Ringo.
Waliobakia wote waliokuja kuwa Memba wa Baraza la Mapinduzi hawakuujua mpango huu.
Waliwashtukia Wamakonde wako mitaani na mapanga wakiua Wazanzibari.
Tulifanya kipindi cha TV Imaan na Salim Rashid 2012 nikamuuliza kuhusu jeshi kutoka Kipumbwi. Hakuwa anafahamu lolote.
[4/2, 6:12 PM] Mohamed Said: Mahojiano na Salim Rashid TV Imaan 2012.
[4/2, 6:12 PM] Mohamed Said: Baadhi ya magazeti yamemtaja Salim Rashid kuwa ni kinara wa mapinduzi. Naweka mambo sawa.
No comments:
Post a Comment