Utangulizi
Jamal Yassin |
Tarehe 17 February 2016
niliweka katika hii blog habari za Jamal Yassin nikieleza kuwa alikamatwa na
polisi kwa tuhuma za ugaidi na akafanyiwa unyama mkubwa usioelezeka ambao
ulisababisha yeye baada ya kuachiwa kutokwa na damu sehemu zake za siri mbele
na nyuma. Kwa masikitiko makubwa sana napenda kusema kuwa imedhihirika kuwa
hayo yote aliyoeleza na mimi kuyatangaza ni habari za uongo. Jamal Yassin
imedhihirika ni tapeli mwenye kipaji cha juu cha udanganyifu. Naomba radhi kwa
wote.
Jamal Yassin na Sheikh Ali Mbaruk |
Mizani Ijumaa 15 Januari 2016 |
Mwandishi akifanya mahojiano na Jamal Yassin tarehe 17 Februari 2016 akiwa ameongozana na Sheikh Ali Mbaruk |
Ndugu zangu hivi
punde asubuhi hii nimezungumza na Sheikh Ali Mbaruk kuhusu Jamal Yassin.
Mazungumzo yetu
yamechukua kiasi cha dakika 20. Kanithibitishia kuwa Jamal ni tapeli wa kipaji
cha juu sana.
Jamal si Mpemba bali
ni Muha kutoka Kigoma na nduguze wamelithibitisha hilo mbele ya Imam Msikiti wa
Chihota Sheikh Ali Mbaruk akiwepo.
Kufupisha...
Katika mahojiano
alikimbia akaruka ukuta wa msikiti.
Akipigiwa wito wa
"mwizi" akakimbizwa na kutiwa mkononi.
Alipata kipigo.
Waislam walimfikisha
hospital kumtibu na kubwa walilofanya ni kuomba daktari amvue pampers ili waone
kama kweli anavuja damu sehemu zake za siri.
Daktari
alithibitisha kuwa hana athari yoyote.
Jamal alipelekwa
hadi Mtambani na akaomba radhi.
Lakini zipo taarifa hivi sasa yuko Zanzibar
anaendelea na utapeli wake.
No comments:
Post a Comment