Tuesday, 24 May 2016

MTAA WA MSHUME KIYATE ZAMANI MTAA WA TANDAMTI



Ukweli ni kuwa Mtaa wa Mshute Kiyate haupo kwa sababu wahusika wamekataa kubadili kibao cha jina sasa yapata zaidi ya miaka 20. Kitwana Kondo alipokuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam ndiye aliyefanya mabadiliko ya majina ya mitaa kuwaenzi wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika kwa kuipa majna yao ile mitaa waliokuwa wakiishi. Hivyo ndivyo Mtaa wa Kipata ujabadilishwa na kuitwa Mtaa wa Kleist Sykes, Mtaa wa Somali ukaitwa Omari Londo, Mtaa wa Aggrey ukaitwa Max Mbwana, Pugu Road ikaitwa Barabara ya Mwalimu Nyerere, Bi. Tatu binti Mzee akapata mtaa Ilala na Mtaa wa Tandamti ukabadilishwa jina na kuitwa Mtaa wa Mshume Kiyate. Lakini palizuka malalamiko kuwa kilichomsukuka Kitwana Kondo kubadili majina ni hisia za udini. Hii ni baada ya kuonekana wazalendo wengi waliopewa majina ya mitaa ni Waislam. Magazeti yakahoji ni michango gani wazalendo hawa walitoa? Kitwana Kondo katika mahojiano aliyofanya na marehemu Sarah Dumba wa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) alijibu kwa kusema, ''Ikiwa hamjui michango ya watu hawa ulizeni mtaelezwa.''


Kulia wa pili ni Mshume Kiyate

Kushoto: Mwinjuma Mwinyikambi, Max Mbwana Julius Nyerere na Mshume Kiyate
Uchaguzi Mkuu wa 1962



Mzee Mshume Kiyate akimfariji Mwalimu Nyerere baada ya maasi ya wanajeshi
20 Januari 1964
Photo
Mtaa wa Mshume Kiyate katika mihangaiko ya kutafuta rizki nyakati za mchana wakati  wa kutafuta rizki

Photo
Mtaa wa Mshume Kiyate karibu na Soko la Kariakoo kama unavyoonekana hivi sasa

Photo

No comments: