Mijadala hii inahitaji ustahamilivu sana kwa kuwa wengi wanaokuja
kuchangia huwa wanakuja wakiwa tayari wameshaathirika sana na
historia ya aina ya Chuo Cha Kivukoni.
Anapoelezwa historia ambayo inapingana na ile na khasa anaposoma
majina ya Waislam hamaki zinampanda na kuanza kwa kweli wakati
mwingine kutoa hata matusi.
Lakni mimi najua kuwa hayo ninayomueleza ndiyo kweli yenyewe hata
kama kwake ndiyo mara ya kwanza kaisikia.
Hapo inataka utaratibu na jambo lolote likitanguliwa na upole jambo
hupendeza.
Kuna mtu kaja hapa barzani ananidai mimi nimpe data za shule ngapi
Waislam wanazo.
Yeye anataka hizo data ili afananishe na takwimu za vyuo ambavyo
Kanisa limejenga.
Yeye anajuna wazi na fika kuwa Waislam mayatima hawana lolote la
kuonyesha.
Nikamwambia ukitaka kujua tatizo hili tusianze na data kutoka kwa
Waislam tuanze na data kutoka vyanzo vya kanisa vipi limeweza kuwa
kama lilivyo Tanzania.
Nikawa nampa rejea za kusoma.
Akawa anajibu kwa kejeli na kibri na kusoma hizo rejea hataki na hapo
nilimtahadharisha uzito wa hilo somo.
Lakini mimi sikuwa na haraka na yeye kwani najua wapi utakuwa ukomo
wake.
Katika kujibu maswali ya wachangiaji wengine waliotaka kujua kulikoni na
mimi nikawa najibu sasa yeye akaanza kuelewa kuwa lipo jambo kwani
serikali yenyewe ilipiga marufuku kitabu cha Hamza Njozi, ''Mwembechai
Killings...'' baada ya kuja na ushahidi ambao Mkapa aliudai kutoka kwa
Waislam kuwa ipo dhulma.
Mkapa alipoingia madarakani aliomba apewe ''ushahidi wa kisayansi,''
kutoka kwa Waislam kuwa katika serikali kuna watu wanatumia nafasi
zao kuwakandamiza Waislam.
Hii ilikuwa Ukumbi wa Diamond akijibu hotuba ya Islamic Club iliyosomwa na
Ramadhani Madabida.
Usia wangu kwenu nyote ni kuwa tusiache kueleza ukweli taratibu hili jambo
litaeleweka.
Katika kueleweka hili tatizo dawa yake In Shaallah itapatikana.
Prof. Njozi na Mwandishi Johannesburg 2006
No comments:
Post a Comment