Mzee Said na familia yake nje ya nyumba yake na. 81 Mtaa wa Stanley Picha hii imepigwa March 1958 |
Picha hii kaniletea rafiki yangu toka utoto Juma
Khube. Kaniambia kuwa huyo aliyesimama ni Mzee Said na mkewe (kulia) na
katikati ni Shaban Sudi ambae alikuwa mfanyakazi wa bandari na amestaafu kazi
mwaka 2015 na kulia kwake ni binti yake. Hapo ilipokuwa nyumba hii hivi sasa
kuna ofisi ya CCM. Mimi na Juma sote tulipozaliwa hatukuikuta nyumba hii
iliyokuwa Mtaa wa Stanley (baadae ukaitwa Aggrey na kisha Max Mbwana). Jirani ya nyumba hii sisi tumekuta
nyumba bora zaidi ya Mzee Maleta, nyumba ya Mzee Kleist na nyumba nyingine
zilizokuwa katika hali nzuri kupita hii. Nyumba ya Mzee Khube ilikuwa hapo Stanley na ilikuwa nyumba nzuri. Nyumba hii hivi sasa ni gorofa ndefu na
inakabiliana na Msikiti wa Kiblatein moja ya misikiti maarufu ya Dar es Salaam.
Waasisi wawili wa TANU Abdulwahid Sykes na Tewa Said Tewa walikuwa
wanaishi mtaa huo majirani na si mbali na nyumba hii. Jirani na nyumba hii kwenye kona ya
Mtaa wa Stanley na Sikukuu sisi tulipozaliwa tulikuta jengo zuri la fahari kwa
nyakati zile ambalo baadae ikajakuwa ofisi ya Tanganyika Federation of Labour
(TFL) na makao ya Nuta Jazz Band. Ikitazamana na nyumba hii kwa pembeni kidogo ilikuwa nyumba ya mmoja wa
bibi zangu Bi. Debora. Hii nyumba ipo hadi leo lakini imejengwa upya.
Nuta Jazz Band katika miaka ya 1960 aliyechutama kulia ni Juma Akida na nyuma yake ni Abel Balthasar, Mabruki Hondohondo, Muhidin Gurumo. Waliosimama aliyeshika saxphone ni Mnenge Ramadhani, Hussein Kizza na Ahmad Omari (Aliyeshika clarinet jina lake halifahamiki) |
Mtaa wa Kipata (sasa Mtaa wa Kleist Sykes) Mwandishi alizaliwa nyumba ya tatu no. 32 kutoka kushoto mtaa wa mbele unaokatisha ni Mtaa wa Nyamwezi |
Kariakoo ilivyokuwa katika miaka ya 1950 |
Mtaa wa Max Mbwana kama ulivyo hivi sasa angalia ghorofa zinazojengwa Kariakoo Picha imepigwa 2014 |
No comments:
Post a Comment