Sheikh Salim
Mtambo ametufanyia hisani ya kuweka katika ''Group'' yetu ya Barza taarifa hii ya hawli ya
mwanazuoni mkubwa sana Habib Swaleh nami nimeona itapendeza kuiweka hapa ili
jamaa sote tuisome. Hii mosi na pili katika taarifa hii katajwa Sheikh Muhammad
El Beidh ambae kwetu alikuwa ni kipenzi. Kila mwezi wa Ramadhani tuna kawaida
ya kuweka darsa baada ya tarweh na yeye Sheikh El Beidh ikiwa atakuwa Dar es
Salaam alikuwa akitupitia na kutupa moja au mawili katika darsa letu. Chini
mwisho nimeweka picha yake akipokelewa na Abdallah Jabir Mwenyekiti wa
Barza yetu Maalim wetu Sheikh Burhani.
[10:11 PM, 9/27/2016] Salim Mtambo: Tumjue huyu mwanachuoni mkubwa
kabisa kutoka lamu
[10:11 PM, 9/27/2016] Salim Mtambo: Jina lake ni
sayyid Hassan bin sayyid Ahmad badawy bin habib Swaleh jamali leily
[10:11 PM, 9/27/2016] Salim Mtambo: Huyu alikua
ni mwanachuoni mkubwa sana lakini ni wachache waliomtambua manake alikua na
tabia ya kukaa kimya maa shaa llah
[10:11 PM, 9/27/2016] Salim Mtambo: Lakini pale
anapoanza utajua kwamba yeye ni mtu aloshiba elimu
[10:11 PM, 9/27/2016] Salim Mtambo: Katika zama
zake alikua ni nyota isiokua na mfano
[10:11 PM, 9/27/2016] Salim Mtambo: Itoshe tu
kwa uchache kwamba sayyid muhammad Al beidh ni katika wanafunzi walio pitia
mikononi mwake pamoja ya kua alikua ni mjombake
[10:11 PM, 9/27/2016] Salim Mtambo:
Walikisikizana sana na ustadh muhammad maa shaa llah na pia ustadh akimtambua
sana kwamba nikatika wanazuoni
[10:11 PM, 9/27/2016] Salim Mtambo: Na
anaekubaliwa na ustadh kwamba ni mtu basi huwa ni mtu kweli manake ustadh
hakuwa na mudaahana
[10:11 PM, 9/27/2016] Salim Mtambo:
kukujalizia:huyu sio ilikua ni wachache walomtambua bali ni wengi walomtambua
tena sana ila yeye mwenyewe alikua hataki kutambulikana na hizo ni katika
asraari na khawaais za mawalii....kuna aqtwaab,amjaad na awtaad....kinyume na
sisi yeo twataka kuyulikanwa kuwa tuna ilimu au ni wanazuoni....
[10:11 PM, 9/27/2016] Salim Mtambo: alikua na
maktaba ya ajabu pale pale amu kwa waliomtembelea waliiona kazi yake ni kusoma
zuo.
[10:11 PM, 9/27/2016] Salim Mtambo: lakini kandu
avaao na kijibao ni baswiit mno...kofia wakati mwengine akiya mamburui kwenye
hafla udtadhi alikimtengeza...
[10:11 PM, 9/27/2016] Salim Mtambo: aliamua
kufanya zuhdi na kuto uona ulimwengu kuwa si chochote au lolote...
[10:11 PM, 9/27/2016] Salim Mtambo: kitabu chake
alokitunga(النور الساطع لمن يخبط في عيد التاسع cha matlai ni kitabu cha ajabu kitoto kikurasa kipana kimaana...
[10:11 PM, 9/27/2016] Salim Mtambo: kwake kwa
mwanawe ustadh twalib ukenda yao sasa atakuonesha diwani lake aloandika siwengi
walo liona bali wameona baadhi ya qaswaaid zake...
[10:11 PM, 9/27/2016] Salim Mtambo: huyu
aliamkuliwa(الحسن المثقف المتفنن hakuna bahari ambao hakuiingia...
[10:11 PM, 9/27/2016] Salim Mtambo: na hilo hata
nduu zake ni mashahidi mimi baada kuondoka al allaama asyyd ali badawy
sikumuona tena kama yeye kwa riyadhwa na kila mmoya una maono yake....
[10:11 PM, 9/27/2016] Salim Mtambo: nashukuru
kuwa nilipata kutabaruku kwake somo la usuuli na miiqati na baadhi ya masaail
mbalimbali nilimkubali sana na hasa lilonitia raghba ni kusifiwa na ustadh sana
japo ustadh amedomeshwa na mashekhe wengi zuma kisawa kisawa lakini saa zote
alikimtaya bwana huyu na misamiati yake akiniambia kwa sasa ilimu ya miiqaat
hakuna ayuwae zaidi yake...na syd abdallah saggaaf wa siu nanilikwenda
nikashuhudia tena ashakua mtu mzima na hakupiswa...
[10:11 PM, 9/27/2016] Salim Mtambo: mungu
amrahamu na atupe barka zake na asraari zake.aamiin...wallaahi leo ni mefurahi
sana ustadh husein...
Kulia ni Sheikh Salim Mtambo |
Darsa la Mwezi Mtukufu wa Ramadhani baada ya Tarweh |
Kushoto Sheikh Muhammad El Beidh, Sheikh Burhani na Sheikh Abdallah Jabir |
No comments:
Post a Comment