Nasaluka,
Wala usiitabishe akili yako kuhusu historia ya uhuru wa Tanganyika
na historia ya Mapinduzi ya Zanzibar 1964.
Hatajapata ujasiri wa kuandika historia ya kweli ya Tanzania sasa
zaidi ya miaka 50.
Nimesoma historia ya uhuru wa Tanganyika Chuo Kikuu Cha
Dar es Salaam.
Kila siku nilikuwa nagongana na mwalimu wangu kwa kumueleza
kuwa hilo silo hili silo.
Nikamfahamisha kuwa naitoa makosa historia hiyo kwa kuwa wazee
wangu ndiyo walioasisi hizo harakati za uhuru na hapa sioni kutajwa.
Ingia hapa:
Mohamed Said: KUTOKA JF: BABU YANGU SALUM ABDALLAH
Nikawa katika semina wakati mwingine naachiwa nieleze historia ya
TANU na mambo yalivyokuwa.
Mwisho wa yote kwa kuchelea historia ya kweli isije kupotea nikaandika
kitabu, ''The Life and Times of
Abdulwahid Sykes (1924-1968) The
Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in
Tanganyika,'' Minerva, London 1998.
Kuhusu historia ya Mapinduzi ya Zanzibar, kitabu kilichoeleza ukweli ni
cha
Dr. Harith Ghassany, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,'' USA,
2010.
Ingia hapa:
Free Downloading ya Kitabu
Click to expand...
No comments:
Post a Comment