Mohamed SaidVerified User ✅
Mastermind wa mapinduzi kinara alikuwa Mtanganyika yeye ndiye
aliyetoa kila kitu kuanzia fedha, askari mamluki, silaha, mafunzo na
''logistic,'' zote.
Unaweza kuisoma historia yote ya mapinduzi katika kitabu hicho hapo chini:
HISTORIA YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KATIKA KITABU CHA ''KWAHERI UKOLONI KWAHERI UHURU,'' NA HARITH GHASSANY
Mohamed Omari Mkwawa
Mohamed Said: HISTORIA YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KATIKA KITABU CHA KWAHERI UKOLONI KWAHERI UHURU
Mmh basi vitabu nilivyovisoma vyote wameelezea kuwa ndio sababu mojawapo ya mapinduzi
Mohamed SaidVerified User ✅
Wenye mapinduzi yao wanasema walimvisha Okello blanketi na
likamwenea na akawa, ''Filed Marshal,'' na yeye mwenyewe kwa
ujinga aliokuwanao akaamini kweli yeye ni, ''Field Marshal.''
Yaani yeye na Field Marshal Josip Broz Tito aliyeongoza jeshi
la Partisan, Yugoslavia wakati wa Vita Vya Pili Vya Dunia dhidi ya
Hitler vyeo vyao ni sawa.
Hakujua kama yeye ni, ''Field Marshal,'' wa Mamluki wa Kimakonde
kutoka mashamba ya mkonge ya Sakura na Kipumbwi kutoka
Tanga.
Historia za viongozi wa Afrika zina matatizo makubwa sana.
Kushoto Dk. Harith Ghassany na Mohamed Omar Mkwawa wakati wa utafiti wa kitabu, ''Kwaheri Ukoloni
Kwaheri Uhuru.''
- New
Mohamed SaidVerified User ✅
New
Nami nakushukuru wewe kwa kuniletea John Okello.
Nakuwekea zawadi kidogo hapo chini na maelezo yake:
Kushoto ni Mohamed Omar Mkwawa, Juma Duni na Prof. Lipumba.
Picha hii nimeipiga mwaka Tanga 1995 wakati wa uchaguzi wa
kwanza wa vyama vingi Prof. Lipumba akigombea kwa tiketi ya CUF.
Mzee Mkwawa amevaa fulana yenye picha ya Lipumba.
Katika siasa za kudai uhuru wa Zanzibar Mzee Mkwawa wakati huo
kijana alikuwa ASP mkubwa kiasi Mzee Karume akampa jina, ''Tindo.''
Jina hili la ''Tindo,'' alipewa na Karume kwa kuwa kazi ya tindo ni kuvunja
mawe na Mzee Mkwawa alikuwa akipelekwa na ASP zile sehemu ngumu.
Hapa ilikuwa nyumbani kwa Mama Ummie Anzuani mwanachama
shupavu wa CUF Tanga Mjini.
Nilipopiga picha hii sikuwa namjua Mzee Mkwawa.
Nilikuja kujuananae miaka mitatu baadae nilipohamia Tanga kikazi.
Alinifanya mwanae na ndipo akanieleza mengi katika historia ya
mapinduzi ya Zanzibar kuwa kulikuwa na kambi ya mamluki na yeye
akiisimamia kwa msaada wa Ali Mwinyi Tambwe na Jumanne
Abdallah.
Ali Mwinyi Tambwe alikuwa Mkuu wa Wilaya na Jumanne Abdallah
yeye alikuwa Mkuu wa Mkoa.
Kambi hii ilikuwa Kipumbwi.
Hii ilikuwa siri kubwa iliyofichwa kwa takriban miaka 40.
Mamluki hawa wengi wao wakiwa Wamakonde aliwavusha yeye kwa
majahazi kwenda Zanzibar kwa ajili ya kuipigia kura ASP na mwaka 1964
kushiriki katika mapinduzi.
Victor Mkello
Katika kazi hii Mzee Mkwawa alishirikiana na Victor Mkello kiongozi wa
chama cha Wafanyakazi katika mashamba ya mkonge.
Hawa Wamakonde ndiyo walioua Waarabu wengi sana katika mapinduzi.
Saturday, 19 November 2016
KUTOKA JF: JOHN OKELLO
About Mohamed Said Historia, Siasa na Maendeleo Tanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment