Friday, 9 December 2016

KUMBUKUMBU YA UHURU WA ZANZIBAR 10 DESEMBA 1963...NA MAPINDUZI YALIYOFUATIA BAADA YA MWEZI MMOJA

Utangulizi
Zanzibar ilipigania uhuru wake kama nchi zote duniani zilizokuwa chini ya utawala wa kikoloni. Duniani kote historia za kupambana na ukoloni ndizo zilizoibua mashujaa wa mataifa hayo ambao huwekewa kumbukumbu maalum. Bahati mbaya sana historia ya uhuru wa Zanzibar haienziwi ipasavyo. Historia inayopewa uzito ni historia ya mapinduzi. Kwa ajili hii basi siku ya uhuru wa Zanzibar ambayo ni siku adhimu iliyojaa historia yake ya kukunbukwa haiadhimishwi. Tarehe 10 Desemba siku Zanzibar ilipopata uhuru wake kutoka kwa Uingereza hupita kimya kimya kama siku nyingine yoyote ya mwaka. Hata hivyo hakuna awezaye kufuta historia. Historia ya Zanzibar ya kupambana na ukoloni ipo hai pamoja na vitimbi walivyokutananavyo wapigania uhuru wa Zanzibar. Halikadhalika mashujaa wa uhuru wanafahamika ingawa wengi wameshatangulia mbele ya haki. Jambo la kushukuriwa ni kuwa wazalendo hawa baadhi yao wameacha hazina kubwa ya kumbukumbu ya historia hiyo ambayo kwa kweli na kwa uhakika ndiyo historia ya uhuru wa Zanzibar ambayo hakuna atakaeweza kuifuta.

Zanzibar kama ilivyokuwa hapo kale

Juu kwenye ngazi Abeid Amani Karume, Hasnu Makame, Mohamed Shamte na Ali Muhsin


Ibun Saleh, Juma Alley, Mohamed Shamte, Dr. Idarus Baalawy na Ali Muhsin






Baadhi ya vitabu vya historia ya Zanzibar
Mwandishi akiwa pwani ya Kipumbwi  kijiji ambacho kulikuwa
na kambi ya askari mamluki kutoka mashamba ya mkonge ya Sakura
waliovushwa kutokea hapo kuingia Zanzibar kushiriki katika mapinduzi 1964

No comments: