Wednesday 24 May 2017

KUTOKA JF: KITWANA KONDO NA OLIVER CROMWELL



Abudist,
Ingetosha kwa mimi kukunyamazia kimya lakini nimeona vyema nikufahamishe
lile ambalo wewe hulijui.

Mzee Kondo amekaa darasani vizuri yeye ni mhitimu wa Howard University,
Marekani.

Mzee Kondo bila shaka kwa yale mafunzo yake katika Idara ya Usalama ya
Kiingereza alikuwa bingwa wa kumpoteza yeyote asimjue.

Nakueleza haya kwa kuwa mimi Mzee Kondo alikuwa baba yangu kwa hiyo
nimekuwa karibu na yeye, nimemfahamu vizuri na nimejifunza mengi kutoka
kwake.

Kwanza alikuwa na ujuzi mkubwa sana wa lugha ya Kiingereza lakini hakupenda
watu walijue hili.

Mzee Kondo alikuwa anaijua vyema historia ''ancient,'' na ''modern.''

Nakumbuka siku moja alipotushangaza mimi na wenzangu alipotupa historia ya 
Oliver Cromwell

Siku nyingine alitushangaza tena alipotupa historia ya Saddam Hussein na Abdul
Karim Kassim
 aliyekuwa Waziri Mkuu wa Iraq.

Mzee Kondo alikuwa hodari wa kuhifadhi nukuu za wasomi wakubwa neno kwa neno
kwa lugha zote, Kiingereza na Kiswahili.

Mzee Kondo akimpenda sana mshairi, Muyaka bin Haj (1776 - 1840) na alihifadhi 
beti zake nyingi.

Ajabu ni kuwa Kitwana Kondo ukimchukulia kuwa, ''hamna kitu,'' hatokukatisha tamaa
alipenda, kile Waingereza wanaita, ''to play dumb,'' yaani kujifanya mbumbu, ikiwa wewe 
utamchukulia hivyo. 

Abdudist, wewe kama wengi wa mfano wako umelambwa kichogo na baba yangu.
Mwisho ningependa kukunasihi kuwa maiti haisemwi vibaya.

Tumwache mzee wetu apumzike kwa amani.

No comments: