Showing posts sorted by date for query Babu yangu salum abdallah. Sort by relevance Show all posts
Showing posts sorted by date for query Babu yangu salum abdallah. Sort by relevance Show all posts

Wednesday, 10 January 2018

SIKU BABU YANGU SALUM ABDALLAH ALIPOMKABILI FREDRICK MCHAURU KATIKA MGOMO WA WAFANYAKAZI WA TANGANYIKA RAILWAYS TABORA 1947

Frederick Mchauru

Ndani ya gazeti la Raia Mwema (Januari 3-9, 2018) kulikuwa na makala ya maisha ya Mzee Fredrick Mchauru. Kama kawaida yangu kupenda kusoma maisha ya Watanzania maarufu niliitupia jicho. Haikunipitikia kabisa kama Mzee Mchauru niliyemtaja katika kitabu change cha historia ya uhuru wa Tanganyika mwaka wa 1998 bado atakuwa hai. Jina hili likawa linajirudia akilini kwangu. Naam Mzee Mchauru yu hai akiwa sasa na umri wa miaka 97. Huyu Mchauru ndiye yule aliyekabiliana na na babu yangu Salum Abdallah katika uwanja wa mpira wa Town School Tabora chini ya miembe wakati wa kupambana na wakoloni, babu yangu akisimama na wananchi wa Tanganyika wakati Mchauru akiwa mtumishi wa serikali ya Waingereza? Naam ndiye yeye. Makala ile ilikuwa tamu haikuisha imekuja kuhitimishwa na toleo la juma hili la Raia Mwema (10 – 16 Januari 2018).

Katika toleo hili mwandishi Ezekiel Kamwaga kanitaja kwa jina kuwa nimemwandika Mzee Mchauru katika historia ya uhuru wa Tanganyika. Kamwaga akaeleza kuwa nimepata kusema kuwa Mzee Mchauru alipata shida kuelewana na wale waliokuwa wanapigania uhuru wa Tanganyika.


Raia Mwema (10 – 16 Januari 2018)


Dhulma ilikuwa imezidi sana na wafanyakazi wa bandarini Dar es Salaam wakiongozwa kwa siri na Abdul Sykes wakati ile kijana mdogo wa miaka 23 waliamua kufanya mgomo kudai haki zao. Mgomo wa Makuli kama ulivyokujafahamika ulienea Tanganyika nzima.

Lakini ili kuuelewa mgomo huu ni muhimu sana msomaji akasoma historia nzima ya mgomo huu chanzo chake na vipi wananchi waliweza kujiunga pamoja hadi kufikia kuwa na uwezo wa kuitingisha serikali kwa mgomo kuenea Tanganyika nzima.

Haiwezekani kwa hapa kueleza historia yenyewe nitakachifanya nitaweka link ili msomaji kwa wakati wake mwenyewe baadae aweze kusoma lakini kwa sasa napenda kukunyambulieni ilikuwaje hadi babu yangu akapambana uso kwa macho na Fredrick Mchauru katika mgomo wa wafanyakazi wa mwaka wa 1947:


Tabora, Western Province 11 Septemba, 1947
‘’…mgomo huo ulioenea kama moto wa makumbi ulikumba nchi nzima kwa kasi ya ajabu. Ilikuwa kama vile wafanyakazi wa nchi nzima wametaarifiana. Wafanyakazi wa Tanganyika Railways huko Tabora wakiongozwa na Salum Abdallah waliingia kwenye mgomo tarehe 11 Septemba. Chama cha African Association mjini Tabora kilimteua Mwalimu Pinda, aliyekuwa akifundisha shule ya St Mary, kuwa 'mshauri' wa wafanyakazi waliogoma.  Asubuhi ya siku ya mgomo wafanyakazi wa Tanganyika Railways walikusanyika kwenye kiwanja cha mpira chaTown School, wakakaa chini ya miembe kujikinga jua. Tabora ni maarufu kwa miti hiyo. Tangu siku hiyo kiwanja hiki kikawa ndicho uwanja maalum kwa mikutano yote ya siasa.

Serikali ilimtuma kijana mmoja kutoka Masasi aliyesoma katika shule za misheni, Frederick Mchauru kuwahutubia wafanyakazi na kuwaomba wasimamishe mgomo na warudi kazini.

Mchauru alikuwa Mmakonde kutoka Newala. Alielimishwa St. Josephís College, Chidya na St. Andrewís College, Minaki. Mwaka 1946, Mchauru alikuwa amerudi kutoka LondonUniversity akiwa amehitimu masomo yake na kuanza kazi mjini Tabora kama Assistant Social Development Officer. Wafanyakazi waliokuwa kwenye mgomo walimpigia kelele wakimtaka anyamaze huku wakimwita msaliti. Inashangaza namna shule za misheni zilivyowatengeneza watumishi wa serikalini walio wasomi wawe watiifu na waaminifu kwa dola. Wasomi hawa mara nyingi walijikuta wanasigana na wale waliokuwa wakipinga ukoloni na udhalimu.

Mchauru alishindwa kutambua hali halisi iliyokuwapo pale sike ile. Mchauru alipuuza zile kelele akaendelea kuzungumza akijaribu kuwasihi wafanyakazi warudi kazini kwao. Ghafla hali iligeuka.

Watu walipandwa na hasira na kusikia wakisema ashikishwe adabu. Watu waliokuwa wamehamaki wakaanza kumsogelea. Salum Abdallah, akiwa kiongozi wa watu wale, alihisi kuwa endapo hatachukua hatua ya kumnusuru Mchauru huenda watu wakamuadhibu.

Alienda pale aliposimama Mchauru. Aliinua mikono yake juu akawataka watu watulie. Salum Abdallah alikuwa mtu wa miraba minne na alikuwa na sauti kubwa.

Wanachama wengi wa TRAU wanamkumbuka kwa sauti yake, hasira zake na kwa umbo lake kubwa. Wafanyakazi walipomuona Salum Abdallah walitulia na Mchauru akaondoka pale kimya kimya kupeleka taarifa kwa hao waliomtuma kuwa watu wamegoma, hawasikii la muadhini wala la mnadi sala…’’

(Kutoka kitabu, ‘’Maisha na Nyakati za Abdulwahi Sykes (1924 – 1968)…’’)

Mwaka wa 1960 Salum Abdallah aliongoza tena mgomo wa wafanyakazi wa Railway uliodumu siku 82. Kwa miezi mitatu treni na mabasi ya Railway yalisimama hadi Waingereza waliposalimu amri na kuwaita viongozi wa wafanyakazi katika meza ya majadiliano.

Uhuru ulipopatikana babu yangu akapambana kwa fikra na msimamo wa Nyerere kuhusu vyama vya wafanyakazi Nyerere akitaka viwekwe chini ya TANU na viongozi wa vyama vya wafanyakazi pamoja na babu yangu wakipinga wazo hilo. Yalipotokea maasi ya wanajeshi tarehe 20 Januari 1964 baada ya maasi kuzimwa na jeshi la Waingereza, Nyerere aliwakamata viongozi wote wa vyama vya wafanyakazi na kuwaweka kizuizini. Babu yangu alizuiwa kwenye jela ya Uyui, Tabora na alipotoka kizuizini Tanganyika Railway African Union (TRAU) chama alichokiasisi mwaka wa 1955 kilikuwa kimepigwa marufuku pamoja na vyama vingine vya wafanyakazi na badala yake kimeundwa chama cha National Union of Tanganyika Workers (NUTA) kwa juhudi kubwa za Rashid Kawawa na Michael Kamaliza.

Babu yangu alihama Tabora na kwenda Urambo kupisha shari kwani zilienezwa taarifa za uongo kuwa yeye alikuwa katika kundi pamoja na Victor Mkello (kiongozi wa wafanyakazi wa mashamba ya mkonge) na Kassanga Tumbo walikuwa wamekula njama ya kupindua serikali na kumuua Rais Nyerere. Babu yangu akajikita katika ukulima wa tumbaku Urambo huku akiendelea na ukulima wake wa miaka yote Kakola na Uyui Tabora.

Fredrick Mchauru aliendelea na utumishi katika serikali ya kikoloni na uhuru ulipopatikana mwaka wa 1961 alishika nyadhifa mbalimbali katika serikali huru kama zilizvyoelezwa katika makala zilizochapwa na Raia Mwema. Kama mimi nisingeaandika kitabu cha Abdul Sykes huenda historia hii ya babu yangu na wazalendo wengine isingejulikana na historia ambazo zingesomwa ndiyo hizi za watu kama Fredrick Mchauru na wengineo.

Salum Abdallah alifariki mwaka wa 1974 akiwa na umri kama miaka 80 akiwa mkimya sana kwa kuwa hapakuwa tena pale mjini na barza zilizokuwa zikijadili siasa kama miaka ya 1950 wakati wa kudai uhuru. Siasa ilikuwa sasa jambo la kutisha watu wakihofu kukamatwa na kuwekwa gerezani. 

Babu yangu akiungulia ndani kwa ndani kwa chuki dhidi ya TANU chama alichokiendea mbio na kuhudhuria mikutano yake yote ya siri mwaka wa 1953 pamoja na wazee wenzake akina Maulidi na Abdallah Kivuruga, Rajab Saleh Tambwe, Abubakar Mwilima kuwataja wachache,  na kuwa mmoja wa waasisi wake mjini Tabora mwaka wa 1955.

Siku zote yeye baada ya kuona vyama vya wafanyakazi vimekwa chini ya TANU na serikali yake aliwaona viongozi wapya wa vyama hivi vibaraka wa serikali hawataweza kupigania haki za wafanyakazi kwa dhati.

Sunday, 31 December 2017











Nanren,
Aliyewekwa kizuizini si baba yangu.
Aliyewekwa kizuizini ni babu yangu Salum Abdallah.

Hakuwekwa kwa ajili ya dini.

Yeye alikuwa Mwenyekiti wa Tanganyika Railway African Union (TRAU)
chama alichokiasisi na kuwa mwenyekiti wake mwaka wa 1955 Kasanga
Tumbo akiwa katibu.

TRAU ilipigana bega kwa bega katika uhuru wa Tanganyika na babu yangu
ni katika wanachama wa mwanzo wa TANU Tabora.

Yeye alikuwa katika kamati ya siri iliyokuwa ikifanya mikutano mjini hapo
kwa matayarisho ya kuundwa TANU.

Salum Abdallah alipigana kwa hali na mali katika kupambana na ukoloni.
Mwaka wa 1947 aliongoza General Strike halikadhalika mwaka wa 1949.

Mwaka wa 1960 aliongoza mgomo wa Railway uliodumu siku 82 kuvunja
rekodi ya mgomo wa siku 62 ulioongozwa na Makhan Singh Kenya.

Salum Abdallah alikamatwa na kuwekwa kizuizini baada ya maasi ya KAR 
ya mwaka wa 1964 pamoja na viongozi wengine wa vyama vya wafanyakazi.

Lakini kesi ile ya waasi ilipokwenda mahakamani hawa viongozi wa vyama vya 
wafanyakazi hawakushitakiwa kwa uasi.

Kuwekwa kwao ndani ilikuwa Mwalimu Nyerere anatafuta nafasi ya kuunda 
chama kimoja cha wafanyakazi kitakachowekwa chini ya TANU.

Ule mgomo wa mwaka wa 1960 ndiyo uliomtia hofu Mwalimu Nyerere kwa 
kudhihirikiwa kuwa kulikuwa na viongozi wa watu kama yeye ambao walikuwa 
wakisikilizwa na wananchi.

Mara tu baada ya uhuru mwaka wa 1962 Nyerere aliitisha mkutano Moshi wa 
viongozi wa wafanyakazi agenda ikiwa kuwa na chama kimoja chini ya TANU.

Babu yangu alikuwa mmoja wa watu waliompinga katika wazo hilo kwa hoja nzito.

Nyerere hakufurahishwa na yeye.

Babu yangu alipotoka kizuizini alijitoa katika siasa na kujikita katika biashara na 
kilimo cha tumbuku Urambo.

Alipokufa mwaka wa 1974 TANU ilifika mazikoni na walisoma taazia ya kumsifia
wakisema kuwa Salum Abdallah aliweka mfuko wake wazi kwa TANU wakati
wa kupigania uhuru.

Babu yangu hakupata kujiunga na AMNUT yeye alikuwa TANU hadi alipohisi usaliti
ndani ya chama uliosababisha yeye kuwekwa kizuizini kwa shutuma za uongo.

Bahati mbaya sana umekuwa ukiamini kuwa babu yangu aliwekwa ndani kwa ajili
ya Uislam.

Naamini kuanzia sasa unampa babu yangu heshima anayostahili kama mpigania
haki na uhuru wa Tanganyika.

Itapendeza kama ndugu zangu mkajizuia kuandika mambo ambayo hamyajui.

Hiyo unayoita ''chokochoko,'' ukiwa unataka kuelewa historia yake fungua uzi In 
Shaallah nitakuja na nitatoa darsa.


Hii nyaraka hapo chini ambayo inasema kuwa viongozi wa wafanyakazi akiwamo 
babu yangu walihusika katika maasi, kesi ilipofikishwa mahakamani hakuna hata
kiongozi mmoja wa wafanyakazi alishtakiwa.

Viongozi hawa walibakia wameshikiliwa katika jela tofauti kisha wakaachiwa bila
ya mashtaka.



Tuesday, 1 August 2017



Dessa Makoko Kaka sijui kama una akiba ya picha hizi ziko Patwas Restaurant Tanga, kwenye hii nawatambua watu watano Mwalm JK Nyerere na Bw. Patwas kualia kwake unapoitazama picha. Kulia mwenye koti na kofia mzee Rashid Makoko Babu yangu na wa piliake baba ngu Mamboleo Makoko na kushoto mwenye koti na kofia mzee Makata Mwinyimtwana, baadhi ya Waasisi na wapigania Uhuru waTanganyika.


LikeShow more reactions
Reply1 hr
Remove
Hafidh Kido Picha nzuri sana hii Mjomba. Pale Patwas pana historia Kubwa inabidi pafanywe makumbusho

LikeShow more reactions
Reply
1
52 mins
Remove
Mohamed Said Salum Kaka Dessa hii ni hazina kubwa na hidaya nzuri kwangu umeniletea. In Shaa Allah naingia Maktaba nitaweka hapa kitu makhhusi...

LikeShow more reactions
Reply
2
31 mins
Manage
Dessa Makoko Insha Allah na Asante

LikeShow more reactions
Reply
1
19 mins
Remove
Dessa Makoko Usemayo ni kweli mjomba Hafidh Kido

LikeShow more reactions
Reply
1
19 mins
Remove
Mohamed Said Salum Tarehe 23 Oktoba,1955 wanachama wa mwanzo wa TANU huko Tanga walikutana kuchagua uongozi wao chama. Hamisi Heri alichaguliwa kuwa mwenyekiti na Peter Mhando katibu. Jumla ya watu arobaini na tano walihudhuria mkutano huo na wakapewa kadi za TANU. Mwalimu Kihere alihudhuria mkutano ule lakini hakuchaguliwa katika nafasi yoyote ya uongozi. Kamati ya wanachama iliundwa kutokana na wale wanachama kumi na moja waasisi waliokutana katika ule mkutano wa kwanza mwezi uliopita. Kamati hiyo ilikuwa na wajumbe wafuatao: Abdallah Rashid Sembe, Mohamed Kajembe, Victor Mkello, Dhili Mgunya, Ali Mohamed, Abdallah Mohamed na Mohamed Sadik. Peter Mhando alijitolea nyumba yake kuwa ofisi ya kwanza ya tawi la TANU mjini Tanga. Mara tu baada ya mkutano huu wazee wa Tanga wakiongozwa na Makoko Rashid, mwanachama wa zamani wa TAA walianza kufanya kampeni kwa ajili ya TANU. Chama kilipata msukumo mwingine na kuongezeka nguvu wakati Sadik Ali Patwa Muasia tajiri alipoingia TANU.

Patwa alikuwa Muislam wa madhehebu ya Shia. Patwa alikuwa amehamia Tanganyika kutoka Zanzibar mwaka 1918 baada ya kumalizika kwa Vita Kuu ya Kwanza. Pale Tanga Patwa alianzisha kiwanda cha soda na akatajirika. Wakati huo wa zama za ukoloni wakati Waasia wenzake walikuwa wakiwabagua Waafrika, Patwa alikuwa akikaa na Waafrika wa rika lake akinywa nao kahawa. Halikadhalika watoto wake wakawa wanacheza kandanda na vijana wenzao wa Kiafrika katika vilabu vya Tanga. Hili lilikuwa jambo geni na lisilokuwa la kawaida kutoka kwa familia ya Kiasia wakati wa ukoloni. Patwa alisaidia harakati za kudai uhuru kwa hali na mali, na akaifanyia kampeni TANU miongoni mwa jamii yake mwenyewe ya Kiasia. Wakati wa harakati Nyerere alikuwa akifanyiana maskhara na Patwa akimwambia, ‘’Mzee Patwa baada ya kupata uhuru nadhani tukuteuwe uwe balozi wetu India.’’ Lakini Patwa hakuiona Tanganyika huru, alifariki kabla ya uhuru kupatikana. 

Baada ya kufungua tawi la TANU mjini Tanga, uongozi wa chama ulimwalika Julius Nyerere, Bibi Titi Mohamed, John Rupia na Mbutta Milando kufanya ziara Tanga. Nyerere alifikia nyumbani kwa Hamisi Heri. Ujumbe huu kutoka makao makuu ya TANU ulipata makaribisho makubwa yaliyoandaliwa na vyama vya lelemama ambavyo kwa kawaida vilikuwa vingi sana katika pwani ya Afrika ya Mashariki kutoka Mombasa nchini Kenya hadi Mikindani, Tanganyika. Kiongozi wa akina mama hawa mjini Tanga aliyesaidia kuieneza TANU alikuwa Bibi Mwanamwema bint Sultan, ndugu wa mbali wa mwenyekiti wa TANU Tanga, Hamisi Heri. 

Matokeo ya ziara ya Nyerere Tanga ilikuwa ni kumrudisha Mwalimu Kihere katika siasa. Baada ya kushindwa kupata nafasi yoyote katika chama, Mwalimu Kihere alipoteza shauku ya siasa. Nyerere alipokuja Tanga kuifanyia kampeni TANU ndipo Mwalimu Kihere alikaribishwa kujiunga na chama. Mwalimu Kihere alifahamiana na Nyerere mwaka 1946 walipokutana Dar es Salaam katika mkutano wa mwaka wa African Association. Nyerere alipozuru Tanga Mwalimu Kihere alitaka kufanya dhifa nyumbani kwake kwa heshima yake. Uongozi wa TANU, hususan Hamisi Heri na Mzee Makoko walikataa kumruhusu Nyerere kuhudhuria dhifa hiyo kwa sababu Mwalimu Kihere alikuwa hajaonesha kuiunga mkono TANU. Nyerere akitambua utu uzima wa Mwalimu Kihere, uzoefu na sifa yake ya uongozi katika African Association, alishauri uongozi wa TANU Tanga usiache fursa ile ipite bure. Nyerere alitoa hoja kuwa, ilikuwa muhimu kukubali mwaliko wa Mwalimu Kihere na kutumia fursa hiyo kumuomba arudi kwenye harakati kwa kuwa TANU ingefaidika kutokana na uzoefu wake alioupata katika African Association. Kwa ajili ya nasaa hiyo TANU ilikubali mwaliko wa Mwalimu Kihere na Nyerere alihudhuria dhifa ile nyumbani kwa Mwalimu Kihere pamoja na wanachama wengine.

Mwalimu Kihere alikuwa mwanasiasa wa msimamo wa wastani, alikuwa mbali na msimamo mkali dhidi ya serikali. Kwa ajili hii Mwalimu Kihere alielewana vizuri na utawala wa kikoloni. Hii ilikuwa kinyume kabisa na wazalendo wengine kama Mzee Makoko Rashid ambaye kwa miaka mingi alijulikana kwa chuki yake dhidi ya Waingereza. Inasadikiwa kwamba watu wawili wataingia katika historia kwa chuki zao mahsusi dhidi ya Waingereza, mtu wa kwanza ni Abdillah Schneider Plantan na wa pili ni Mzee Makoko Rashid. Wote wawili walifungwa gerezani kwa sababu ya msimamo wao dhidi ya serikali ya kikoloni. PC na DC wake wote wawili walikukubali mwaliko wa Mwalimu Kihere. Mwalimu Kihere alimtambulisha Nyerere kwa wageni mashuhuri na alimuomba azungumze maneno machache. Nyerere kwa kipaji chake cha ufasaha wa kuzungumza alitoa hotuba kuhusu lengo la TANU na kanuni za kidemokrasia kama zilivyoelezwa na Umoja wa Mataifa. P.C. alisimama baada ya Nyerere kuzungumza na akatoa hotuba kwa niaba ya serikali. P.C. alimsifu Nyerere kuwa ni mwanasiasa mzuri kinyume na vile alivyosikia kabla ya kukutana naye. Hapo hapo alitoa ruhusa kwa Nyerere na TANU kufanya mikutano ya hadhara katika wilaya zote za jimbo hilo. Lakini uhusiano huu haukudumu, serkali iliyapiga marufuku matawi kadhaa ya TANU Tanga mara tu baada ya kuundwa kwa UTP.

Siku iliyofuata mabingwa wa hotuba wa TANU, Julius Nyerere na Bibi Titi Mohamed walihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Tangamano. Hii ilikuwa hatua kubwa sana kwa TANU, na kwa harakati dhidi ya ukoloni pale Tanga. Ilikuwa muda mrefu umepita tangu zile siku za zile siasa za wasomi katika Discussion Group, kikundi cha majadiliano; na ile mizozo baina yao na ule uongozi Waarabu katika TAA. Baada ya hapo, Mwalimu Kihere alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa TANU Tanga badala ya Hamisi Heri na Amos Kissenge alichaguliwa katibu. Abdallah Rashid Sembe mmoja wa wanachama waasisi wa mwanzo kabisa wa TANU alichaguliwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya TANU akiwakilisha Jimbo la Tanga.Ilikuwa chini ya hali ya hewa ya kisiasa kama hii ndipo TANU iliingia kwenye uchaguzi wake wa kwanza katika Tanganyika, chaguzi wa Kura tatu wa mwaka wa 1958 Tanga ambako United Tanganyika Party (UTP) ilikuwa imara, TANU iliwachagua John Keto, B. Krishna na R. N. Donaldson kama wagombea wake. John Keto akiwa miongoni mwa walimu wa St. Mary’s School, Minaki na alikuwa amefanya kazi kubwa katika siku za mwanzo kufungua matawi ya TANU huko Kisarawe. TANU iliamua kumteua Keto kusimama Tanga ambako ndiyo kulikuwa kwao. Katika uchaguzi huu serikali iliacha uandikishaji wa wapiga kura kwa vyama vyenyewe. Mzee Makoko Rashid, mwanasiasa wa makamo mwenye msimamo thabiti wa chama na kijana Mmaka Omari walikuwa maofisa waandikishaji wa wapiga kura katika wa TANU mjini Tanga. Makoko na Mmaka walikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la kuwaandikisha watu ambao hawakutimiza masharti yaliyoelezwa na ilani ya uchaguzi. Katika ghera yao kwa TANU kushinda ule uchaguzi muhimu, Mzee Makoko alimsajili Mwafrika yoyote aliyetaka kuipigia kura TANU bila kujali sifa zake. Bhoke Munanka alikamatwa vilevile kule Mwanza kwa kosa hilo hilo. Hakukuwa na ushahidi wa kutosha dhidi ya Mmaka Omari kwa hiyo aliachiwa huru mara tu baada ya kukamatwa kwake. Mzee Makoko Rashid alipatikana na hatia na alihukumiwa kufungwa jela. Adhabu ya kifungo ilidhoofisha sana afya yake na mara baada ya kufunguliwa kutoka gereza baya sana la Maweni Mzee Makoko alifariki.

LikeShow more reactions
Reply
1
12 minsEdited
Manage
Mohamed Said Salum ...ilikuwa chini ya hali ya hewa ya kisiasa kama hii ndipo TANU iliingia kwenye uchaguzi wake wa kwanza katika Tanganyika, chaguzi wa Kura tatu wa mwaka wa 1958 Tanga ambako United Tanganyika Party (UTP) ilikuwa imara, TANU iliwachagua John Keto, B. Krishna na R. N. Donaldson kama wagombea wake. John Keto akiwa miongoni mwa walimu wa St. Mary’s School, Minaki na alikuwa amefanya kazi kubwa katika siku za mwanzo kufungua matawi ya TANU huko Kisarawe. TANU iliamua kumteua Keto kusimama Tanga ambako ndiyo kulikuwa kwao. Katika uchaguzi huu serikali iliacha uandikishaji wa wapiga kura kwa vyama vyenyewe. Mzee Makoko Rashid, mwanasiasa wa makamo mwenye msimamo thabiti wa chama na kijana Mmaka Omari walikuwa maofisa waandikishaji wa wapiga kura katika wa TANU mjini Tanga. Makoko na Mmaka walikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la kuwaandikisha watu ambao hawakutimiza masharti yaliyoelezwa na ilani ya uchaguzi. Katika ghera yao kwa TANU kushinda ule uchaguzi muhimu, Mzee Makoko alimsajili Mwafrika yoyote aliyetaka kuipigia kura TANU bila kujali sifa zake. Bhoke Munanka alikamatwa vilevile kule Mwanza kwa kosa hilo hilo. Hakukuwa na ushahidi wa kutosha dhidi ya Mmaka Omari kwa hiyo aliachiwa huru mara tu baada ya kukamatwa kwake. Mzee Makoko Rashid alipatikana na hatia na alihukumiwa kufungwa jela. Adhabu ya kifungo ilidhoofisha sana afya yake na mara baada ya kufunguliwa kutoka gereza baya sana la Maweni Mzee Makoko alifariki.

LikeShow more reactions
Reply
1
11 mins
Manage
Mohamed Said Salum Mwalimu Kihere huyo hapo chini

LikeShow more reactions
Reply9 mins
Manage
Mohamed Said Salum Sheikh Rashid Sembe

Image may contain: 1 person

Mohamed Said Salum Mkutano wa Tabora ulitishia kuigawa TANU katika makundi hasimu yaliyokuwa yakivutana, kama isingekuwa kwa ule makakati uliopangwa kule Mnyanjani, kijiji kidogo nje ya mji wa Tanga. Waliopanga mkakati huo - Nyerere mwenyewe, Amos Kisenge, Hamisi Heri, mwenyekiti wa TANU Tanga, Mwalim Kihere mwanasiasa mkongwe wa African Association, Sheikh Abdallah Rashid Sembe, Ng’anzi Mohamed, Mustafa Shauri na Abdallah Makata - Hawa ndiyo waliinusuru TANU isinase katika mtego uliotegwa na wakoloni ambao ungeifanya TANU igawike katika mapande mawili na kila moja dhaifu kuweza peke yake kuikabili serikali ya kikoloni. Kwa mtazamo wa suala jipya la dini lililoanzishwa na Sheikh Suleiman Takadir mara tu baada ya ule mkutano mkuu wa Tabora, akidai uwakilishi ulio sawa baina ya Waislam na Wakristo, ni wazi siasa katika Tanganyika ingechukua sura ya kutisha. Kutokana na hayo hakuna kundi lolote katika makundi haya mawili ambalo lingeweza kuibuka mshindi isipokuwa serikali ya kikoloni na UTP.

LikeShow more reactions
Reply
1
7 mins
Manage
Hafidh Kido Mashallah

LikeShow more reactions
Reply4 mins
Remove
Mohamed Said Salum Sheikh Dessa iweje leo hawa mashujaa hakuna kumbukumbu zao Tanga ukitoa Makoko Road. Hivi ule Mtaa wa Maua pale katika ya mji una akisi kitu gani? Dessa una sauti CCM wakumbushe na wazindue kuhusu historia hii kama hawaijui mimi nitakuja kwa nauli yangu kuja kutoa mhadhara In Shaa Allah.


Mohamed Said Salum Mkutano wa Tabora ulitishia kuigawa TANU katika makundi hasimu yaliyokuwa yakivutana, kama isingekuwa kwa ule mkakati uliopangwa kule Mnyanjani, kijiji kidogo nje ya mji wa Tanga. Waliopanga mkakati huo - Nyerere mwenyewe, Amos Kisenge, Hamisi Heri, mwenyekiti wa TANU Tanga, Mwalim Kihere mwanasiasa mkongwe wa African Association, Sheikh Abdallah Rashid Sembe, Ng’anzi Mohamed, Mustafa Shauri na Abdallah Makata - Hawa ndiyo waliinusuru TANU isinase katika mtego uliotegwa na wakoloni ambao ungeifanya TANU igawike katika mapande mawili na kila moja dhaifu kuweza peke yake kuikabili serikali ya kikoloni. Kwa mtazamo wa suala jipya la dini lililoanzishwa na Sheikh Suleiman Takadir mara tu baada ya ule mkutano mkuu wa Tabora, akidai uwakilishi ulio sawa baina ya Waislam na Wakristo, ni wazi siasa katika Tanganyika ingechukua sura ya kutisha. Kutokana na hayo hakuna kundi lolote katika makundi haya mawili ambalo lingeweza kuibuka mshindi isipokuwa serikali ya kikoloni na UTP.

LikeShow more reactions
Reply3 mins